Nape ni nani mbaguzi hapa?

Nape ni nani mbaguzi hapa?

jamani huyu mbunge wa arumeru bado ni dogo....so tujue kua zipogi siku atachemsha wakati anaongea..he will learn from his mistakes..akina obama na cameron wanachemshaga kwenye kampeni zao itakuja kua nassari its all part of learning
 
kwani alichokosea nape kipi kweli ukipenda unaona chongo

alichokosea na pe ni kuita chadema ni wabaguzi kwa nasari kusema heri wajitenge wakati mery nagu alishawaambia majimbo yaliyoko chini upinzani serikali ya ccm imeyapeleka likizo.
na ukienda kwenye ansard za bunge komba alishadai watu wa jimbo lake wajiunge malawi kwa sababu ndipo wanapopata huduma.

sasa hawa wa ccm mbona hawahojiwi?
 
NAPE NNAUYE KATIBU MWENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NAOMBA UNIFAFANULIE PAMOJA NA WATANZANIA WENZETU HUHUSU HUU UTATA WA MISIMAMO YAKO.
TOKA JUZI UPO KWENYE VYOMBO VYA HABARI UKITOA UFAFANUZI KUHUSU MANENO ALIYOYATAMKA MBUNGE WA ARUMERU NDG JOSHUA NASARI NA KUUITA NDIO MSIMAMO WA CHADEMA KWA HIYO CHADEMA NI WABAGUZI,SASA NAOMBA TUANGALIE HIZI KAULI MBILI TU HALAFU TUJE NA JIBU LA JUMLA KWA WATANZANIA.
NA KWENYE JIBU UTAKALOTOA HAPA WATANZANIA WATAKUHUKUMU NALO.

A.WAKATI AKIWA KWENYE KAMPENI MERY NAGU AMBAYE NI WAZIRI MWENYE DHAMANA KATIKA SERIKALI AKIHUTUBIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KULE ARUMERU ALIWAAMBIA WANA ARUMERU WAAMUE KUICHAGUA CHADEMA JIMBO LIENDE LIKIZO AU WAICHAGUE CCM WAPATE MAENDELEO.
KUMBUKA NAGU HAKUYASEMA HAYA KWA BAHATI MBAYA NA HAJAWAHI MAHALA POPOTE KUOMBA RADHI,HUYU NI MTU WAJIKONI KWENYE SERIKALI NA CHAMA,ANAYAJUA YALIYOPANGWA NA CHAMA NA SERIKALI.
SASA KWA KAULI YAKE AMBAYO HAJAIPINGA NI KUWA MAJIMBO YOTE YALIYO CHINI YA CHADEMA YAPO LIKIZO.

B.TAFUTA KAULI ZA WASIRA NA OLE MEDEYE NA LUSINDE NA MKAPA.

C.CHUKUA NA KAULI YA JOSHUA NASARI AMBAYE ALISIKIA KAULI ZA MAKADA WA CCM NA KUJA NA MAJIBU HAYO.

MAONI YANGU;
MAMA AKISEMA AKIWABAGUA WATOTO WAKE KWA MAMBO YALIYOKUBALIKA KIFAMILIA NA MTOTO ALIYEUNGANISHA WALE WENZAKE WALIOBAGULIWA NI NANI ATAKAYEKUWA KATENDA KOSA HAPO.
KUMBUKA AKIULIZWA SWALI BUNGENI WAZIRI MKUU ALIMTETEA NAGU NA WASIRA AKIZIITA KAULI ZILE KUWA NI ZA KWENYE KAMPENI TU.
MBOWE BILA KUULIZWA NA MTU YEYOTE PALEPALE JUKWAANI ALISEMA ULE HAUKUWA MSIMAMO WA CHADEMA,SASA BWANA NAPE UNATAKA KUTUAMBIA NINI KWENYE HILI?
AU TUKIULIZA KWA NINI HATUJASIKIA MERY NAGU AMEHOJIWA NA POLISI KWA UHAINI WA KUIGAWA NCHI?
KWA NINI AHOJIWE NASARI KWA KUPIGIA MSTARI JIBU LA MAWAZIRI NA RAIS MSTAAFU?
KWA NINI HAJAHOJIWA LUSINDE KWA MANENO YA UCHOCHEZI DHIDI YA VIONGOZI WALIOPO KIKATIBA?

naomba majibu utakayotoa hapa yawe ndio msimamo wa ccm ili watanzania tujue.

nakutakia kazi njema.

Two wrongs doesn't make one right
 
Jamani kelele za Nape zilikuwa ni kutafuta Ukuu wa Wilaya. Ma-DC wameishateuliwa, sasa hutamwona akichonga tena hadi muda upite kwanza. Dhambi yake ya kutaka kujiunga CCJ bado inamtafuna.
 
Chanzo cha kauli hizi
  1. Kubaguliwa kwa watu wa kaskazini kisiasa ( hata UVCCM waliwahi kusema rais hawezi kutoka kaskz)
  2. Matumizi mabaya ya rasilimali za nchi
  3. Kutengwa kwa baadhi ya maeneo kimaendeleo ( Kama Mt, Lindi, Tabora, Singida nk) sasa hawa wakiomba kuhamia msumbiji kwa mfano watu wa mtwara na lindi kosa? Badala ya kuijenga bandari ile unawapa walebanon kwakuwa serikali imeshindwa kulipa deni la ATC wakati huo huo bagamoyo linatengwa eneo la kujenga bandari mpya.nk
Hitimisho: Sisi wote ni watanzania tuna haki sawa kikatiba basi serikali na CCM waache unyanyasaji ili kuzuia haya kutokea. Ufahamu na uelewa wa tanzania unakuwa kwa kasi sana..
 
Hata mimi nataka niwe rais wa jimbo la Ulanga Magharibi halafu nitangaze uhuru wa kweli wa Mkoa wa Morogoro kwakuwa maendeleo ni duni sana mkoa huu.Mfano:Tangu enzi za Ukoloni hadi leo,Ulanga Magharibi hakuna Umeme,hakuna barabara na huduma za Afya ni duni sana.
 
Kauli ya Nassari is no winner for CCM. Kwa kuwa Mbowe aliisha itolea ufafanuzi palepale jukwaani, CCM na Polisi wake hawakuwa na sababu wala haja ya kuanza kucheza hii poilitical football, they will lose. CCM inatakiwa kujikita katika kukabiliana na hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira. Kutoka nje ya mambo haya ni kukubali kuwa distracted na Nassari, the big loser is CCM.

Tukianza kujadili kauli hapa basi CCM itakuwa ni victim mkubwa sana wa kauli za makada wake. Na ninashangaa hata polisi na DPP kukubali kucheza mchezo wa siasa. Wanaimaliza CCM, japo mioyoni mwao wanajifariji kama vile anavyojifariji mgonjwa wa terminal cancer anapopatiwa morphine huku akijua wazi kuwa dawa hiyo haifanyi lolote kumuondolea kifo kinachomkabili bali kumpunguzia machungu kabla ya kifo.
 
Nape akirudi humu anatakiwa kupiga hodi,kama ameshindwa kulisemea hili kwa sababu najua amelsoma hapa.
 
Back
Top Bottom