William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Hii mada imenifurahisha kidogo labda na mimi nitoe mchango wangu kidogo.moja kwa moja nakubaliana na wale wanaomuona Nape Mnafiki kwa sababu.
1.Unapokua hukubaliani na sera za upande mmoja unachotakiwa ni kutundika madaruga yako na kwenda kule ambako unafikiri mtaongea lugha moja,na ndio maana sina shida na wale wanaohama kwa either kunyimwa madaraka ndani ya chama kwa kuonewa au vinginevyo.
2.Unapokua ndani ya fungate ya chama fulani maana yake ni kwamba umekubaliana nacho hivyo yapasa uendane na sera hizo,kama kuna usiyokubaliana basi uyamalizie humo.
3.Unapokua unatumikia chama,mwajiri au ni sehemu ya familia fulani yapasa kulinda haki ya kupata na kutotoa siri za upande uliopo kwani kwa kufanya vinginevyo wewe si mwaminifu,ni mtu hatari katika hiyo jamii.
Ujumbe wangu;
Nape kama hakukubaliana na CCM alipaswa kuachana nao(kuvua Gamba-maana halisi)halafu akaenda upande mmoja CCJ,au CDM tukajua anachokipigania,lakini sio kutoa siri za CCM ukazipeleka kuzianzishia CCJ,(hapo hakuna confidentility,)na huo sio uongozi.Unafiki ni kitu kibaya sana.Huwa unabeba kitu kinaitwa undumila kuwili.Unaloliongea sio unalolitenda na kumaanisha ,bali kuna jingine nyuma ya pazia.Kwa hiyo napata shida na wale wanaotaka kumpa ushujaa kijana huyu.
Na ndio maana kwa mwajiri mzuri unapotaka kazi kwako moja atataka kujua uzoefu wako,maana ya kwanza kujua kama umekutana na challenges kiasi gani ambazo utamsaidia pindi ukianza kazi,lakini la pili na la muhimu ulikotoka uliondokaje? Hapo ndio kwenye umuhimu mkubwa,kwani unapokua huendani na mwajiri wako utaomba kuacha kazi kwa kufuata taratibu husika bila kuharibu sifa ya mwajiri wako kwa sababu ulikua sehemu ya ile familia,mabaya au mazuri ni sehemu ya maisha yale,unatakiwa kuyaacha na kwenda kuanza maisha mapya.kama unapiga mawe piga ukiwa nje sio ndani,na ukipiga ukiwa ndani tuna haki ya kukufukuza.
Naomba nisiwachoshe nina mengi ya ku-mtima tutaongea wakati mwingine.kina NAPE NI WATU HATARI KWA TAIFA LETU.
- Not really kama kuna ambayo hukubaliani na chama chako you create a political crisis as what CCJ did, Mwalimu alipoona CCM inaanza kukosa mweleko aliwapigia kampeni kina Mrema, sasa utaita ule unafiki? No that is how National politics is played, unaweza ukatoka chama au ukabaki na kutafuta njia za kisiasa za kupata attention ya chama chako, Mpendazoe ndiye mtu wa hatari sana now ninaelewa kwa nini CCM walimtema!
ES!