Chadema hakuna mafisadi,Nape anapoteza mjadala wa mapacha watatu kwa kuingiza chadema. Hajatuambia kama barua za mafisadi zimetoka au la.
Ama kweli newala wamepata Dc kihiyo Nape,ndo huyu huyu Dc aliyemuamuru OCD amkamate mwanakijiji aliyeshindwa kulima shamba la mihogo,gamba dogo linalokua kwa kasii hana jipya huyu mtoto anajua kubwabwaja tuuuuuu!
Kijana naona umepofuka, ufisadi ni akifanya CCM tu? Hata kama mtajitetea kwa nguvu huo ndo ukweli, tatizo ni definition ya ufisadi ila trust me mkipata serikali viongozi wako watafanya hayo hayo. Mbona Mbowe hajakaa shangingi la mil200 kule bungeni? then Slaa anamvaa W/Mkuu kuwa anatembelea magari mazuri. Mbona la Mbowe halisemei? Huyu Dr. asipoangalia atakuwa kama akina Mrema, alisema sana sa hivi yuko wapi? Kemea ufisa na tenda kulingana na unavosema na si unafiki.
Hili la barua za mafisadi si lenu CHADEMA. Lenu ni hili: Mnamlipa Dr Slaa sh milioni7 na nusu kwa mwezi? Dr Slaa ndiye Yaya Toure, Lionel Messi wenu? Katibu wako wa Jimbo la Ubungo analipwaje?
Mimi sio Nape. Simfahamu wala sijawahi kutana naye. Kwa nini Dr Slaa alipwe hivi? Kwa kutaja mafisadi? Mzee wetu Mengi analipwa na nani?Unaweza kuwa ndiye Nape mwenyewe kwa hizi hoja zako...what is 7.5m na kazi anayoifanya....au waitamani uipate weye?
Dr Slaa anafanya kazi zaidi ya hiyo pesa. Watu wengi tu kwenye mashirika wanalipwa pesa zaidi ya hiyo kwa sasa. Ni pesa ya kawaida kabisa. Nenda GGM, nenda makampuni makubwa ya benki, nenda kampuni za madini watu wanalipwa pesa zaidi ya 10M kwa mwezi na si kwamba ni ufisadi make kazi unayofanya ni sawa na hiyo pesa kampuni inatengeneza faida. Mi viongozi wa kampuni nilizowahi fanyia kazi wanalipa pesa zaidi ya hiyo mameneja. Dr haibi cha mtu anakula jasho lake halali. Kuna mtz hapa Geita aliyekuwa meneja wa kampuni ya umeme hapa alikuwa akilipwa mil 25 kwa mwezi na wala hana umuhimu kwa nchi kama Dr Slaa kulinganisha.Watanzania wenzangu,
Dr Slaa aliwahi kunukuliwa akisema mishahara ya Wabunge ni mikubwa sana haiendani na vipato halisi vya Watanzania walio wengi. Tukamshangilia sana humu. Leo tunaambiwa mshahara wake ni zaidi ya milioni7. Tunamtetea kwa nguvu zote. Tunamlaani na kumkejeli Nape. Ni kweli Dr Slaa kachangia pakubwa ruzuku ya sasa ya CHADEMA. Hili halihalalishi mshahara huu.
Labda ni kwa kuwa mkewe wa sasa anatarajia kujifungua! Kwa umri wa Dr Slaa kuzaa mtoto sasa ni shughuli pevu huko mbele.
Hatutachoka milele, kama wewe umechoka endelea kujadili mambo unayoona yanakufaa wewe!
wewe kilaza eeeh sasa ulitaka aikatae kama pinda halafu liende wapi!?? Mfumo unaruhusu hayo!kijana naona umepofuka, ufisadi ni akifanya ccm tu? Hata kama mtajitetea kwa nguvu huo ndo ukweli, tatizo ni definition ya ufisadi ila trust me mkipata serikali viongozi wako watafanya hayo hayo. Mbona mbowe hajakaa shangingi la mil200 kule bungeni? Then slaa anamvaa w/mkuu kuwa anatembelea magari mazuri. Mbona la mbowe halisemei? Huyu dr. Asipoangalia atakuwa kama akina mrema, alisema sana sa hivi yuko wapi? Kemea ufisa na tenda kulingana na unavosema na si unafiki.
Azimio la Zanzibar limeletwa na wazee wako ili waifisadi nchi hii,wewe hushabikii tu ila una maslahi na kundi hilo.Mimi ni mwana CCM ila kwa ufahamu nilionao siwezi kushabikia ujinga wa kuita 7mil za Dr. ni ufisadi nikaacha mamillioni wanayokwiba ndani ya nchi yetu,Na pia mamilioni wanayomwagiwa wabunge kwa kazi hewa na kusinzia ovyo ovyo bungeni.Sitaki ushabiki usio na tija kwa taifa na watanzania kwa ujumla wake.CCm twende na wakati na Tujifunze Yanayotokea Duniani.Maana historia itatuhukumu. Byeeeeeeeeeeee😛ound:😛ound:😛ound:
Chama cha siasa masikini kama ilivyo CHADEMA hakiwezi kulinganishwa na migodi. CHADEMA kina miradi gani mbali ya RUZUKU?Dr Slaa anafanya kazi zaidi ya hiyo pesa. Watu wengi tu kwenye mashirika wanalipwa pesa zaidi ya hiyo kwa sasa. Ni pesa ya kawaida kabisa. Nenda GGM, nenda makampuni makubwa ya benki, nenda kampuni za madini watu wanalipwa pesa zaidi ya 10M kwa mwezi na si kwamba ni ufisadi make kazi unayofanya ni sawa na hiyo pesa kampuni inatengeneza faida. Mi viongozi wa kampuni nilizowahi fanyia kazi wanalipa pesa zaidi ya hiyo mameneja. Dr haibi cha mtu anakula jasho lake halali. Kuna mtz hapa Geita aliyekuwa meneja wa kampuni ya umeme hapa alikuwa akilipwa mil 25 kwa mwezi na wala hana umuhimu kwa nchi kama Dr Slaa kulinganisha.
Mkuu PJ, huyu kakulia katika CCM nyingine sio ile ya babayeBaba wa huyu kijana Nape alikuwa na busara sana akiwa serikalini, japokuwa ilikuwa enzi ya chama kimoja!...na inasemekana kuwa ndiye aliyetunga wimbo maarufu wa "Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa Moyo Wote"!
Nashangaa kwanini huyu mwanae hajarithi kitu toka kwa babaye!
Ni bora ya Yusufu MAKAMBA kuliko mwanataarabu na kiduku huyu!
hivi bado analipwa mshahara na malupulupu ya DC?
huenda ni kweli manake sijasikia kajiuzulu au mtu mwingine kateuliwa mahali pake! sasa nini maana ya kuwajibika? huyu anawajibika saa ngapi kama DC? au anatumia simu/remote control? na likatiba letu hili hatuwezi kumwajibisha JK, jamani kweli watanzania tumenasa, sijui nani atatukwamua na matope haya mazito yenye magamba.
kwa kweli hapa duniani siasa za aina hii huenda zinapatikana tanzania pekee, halafu tunashangaa kwa nini hatpigi hatua kwenda mbele!
Mzee wetu Mengi analipwa na nani?