Nape na mafisadi wa CHADEMA

Kuna taarifa kua Nape nnnayuye atatoa list ya mafisadi ndani ya chadema,..
naomba mwenye updates atupatie huko aliko,...

Amesema tu kwamba mshahara wa dk. Slaa ni ufisadi kwa sababu ni mkubwa. Pia kwamba CDM wanatumia fedha nyingi kwenye maandamano ambazo zingesaidia kuwaondolea wananchi umasikini
 
Hivi kweli tumeshindwa kabisa kuamshana na kushindana kwa hoja? Nadhani nape ni makini sana, sidhani kama na yeye ataingia katika mtego wa orodha maana katika mazingira ya azimio la zanzibar, there is a very thin line between fisadi na tajiri. Let us focus on key issues zinazowagusa wananchi jamani, ufisadi upigwe vita but usisimamishe mambo mengine muhimu, kama vita inanoga hivyo, basi tuunde vitengo kwenye vyama vyetu kupiga vita ufisadi e.g. katibu idara ya kupiga vita ufisadi:) ili wengine waendelee na mambo mengine muhimu (sina maana vita dhidi ya ufisadi sio muhimu).


Uko sahihi ila baadhi tumeumia sana na ufisadi kiwango sawa na kovu lililo kwenye uso kila ukipita ni kama tangazo kwa jamii. Kwa vile nina uhakika uko ndani ya mfumo wa chama letu la kifisadi chukua nafasi yako kuwanyamazisha akina nape wasiropokee ufisadi kama ndiyo jibu kwa azimio la CDM kuushambulia ufisadi kwa kuwasema mafisadi hadharani. kwa bahati mbaya mafisadi wenyewe hawajibu.

Sisi wengine tunaliona kama mazingira fulani yalitengenezwa kufacilitate manufaa fulani ya kundi fulani. Kundi hilo halikujikita kuangalia athari zake zitakuwa na madhara na reaction zipi katika taswira ya taifa. Ni vema kundi hili la wenye kutuamlia mstakabali wa taifa likiri tu na kuchukua hatua kufuta hizi hisia kali zilizopo kwa vitendo. Liutazame upya mfumo uliozaa ufisadi na kusahihisha pale panapotukera wananchi na nchi kwa ujumla. Kuwaelekezea zigo hilo kwa baadhi ya viongozi wenu kwa kuwatawadha ni kama kutawadha mbwa.
 
Amesema tu kwamba mshahara wa dk. Slaa ni ufisadi kwa sababu ni mkubwa. Pia kwamba CDM wanatumia fedha nyingi kwenye maandamano ambazo zingesaidia kuwaondolea wananchi umasikini

yaani nape kumbe ni kichaa sana eh?
maandamano ya chadema na semina elekezi za kunywa chai za ccm ipi inatumia
hela nyingi?
dah,...kuhusu mshahara wataongelea wao wenyewe chadema ila point ya
pili ni ya kipimbi kabisa
 
Wanatafuta la kuongea bila kupima .Nape atuambie kama kuna sheria ya nchi inakataza vyama kinunua vitu chakavu.

Au atuambie hayo magari yamenunuliwa kwa bei ya magari mapya ?

Wabunge wanapata mshahara m 12 si ndio m 7 ni zaidi kidogo ya nusu ya mshahara wa mbunge cha ajabu ni nini ?

Halafu yeye wala hasemi anapata ngapi na raisi wake
 
Kwani alifanya mkutano wa hadhara au alikuwa anaongea na makada wenzeka mafisadi? Mbona hakuna aliyemsikia akiongea au kashikwa na kwikwi kama wenzeka, CCM wazee wa ahadi utekelezaji zerooooooooooooooooooooooooooooo
 
Jamani tujaribu kujiuliza huyu Np kawekwa pale kwa kazi ipi, "Job Description" yake ni kuongea kwa niaba ya Chama, na asipoonea halipwi mshahara kwa hiyo ataongea hata kama kitu ni cha kijinga ili mradi aonekane anafanya kazi.

Mbaya zaidi katika kipindi hiki alichopigwa stop kuwazungumzia Mapacha Wa3, ataongea vitu vingi mpaka atawaboa waliompa hii kazi na soon atastepishwa down.
 
Nataka kujua kama ufisadi unaweza kukomeshwa kwa kuweka walinzi na virungu ama maandamano hasa katika ulimwengu wa kisayansi? Lakini pia watanzania wenzengu mafisadi ni watu na mbaya zaidi ni wenzetu na mara kadhaa wamekuwa wakitumia raslimali ndogo tulizonazo kwa manufaa binafsi, mfano kujichukulia umaarufu wa kibinafsi.
 
Amesema tu kwamba mshahara wa dk. Slaa ni ufisadi kwa sababu ni mkubwa. Pia kwamba CDM wanatumia fedha nyingi kwenye maandamano ambazo zingesaidia kuwaondolea wananchi umasikini

Mshahara wa Dkt Slaa ni mkubwa ukilinganisha na wa nani? Kwani mishahara inatakiwa isizidi kiwango gani jamani? Poor Nape, nilimuona mtu wa maana kumbe ni vuvuzela tu! Na huo ukuu wa Wilaya anautumikia saa ngapi maana kila silu yuko majukwaani/magazetini kujibu hoja za cdm!
 
Chadema naomba tuchape kazi tuache longolongo - ccm waige kwetu
 
Ndugu wadau;

Taarifa za habari za jana usiku leo asubuhi na pia vichwa vya habari vya magazeti kadhaa vimekuwa vikimnukuu katibu mkuu mpya wa CCM Nape Nnauye akisema kwamba leo angeeleza ufisadi wa CHADEMA katika kile kilichoelezwa na wakereketwa wa ccm kama kujibu mapigo ya CHADEMA.

Cha ajabu,

Hajatoa na hatujaisikia taarifa aliyoahidi kuitoa kupitia vyombo vya habari

Maswali ya kjiuliza

Je alikuwa anajaribu kutikisa kiberiti?
Je amelewa madaraka kiasi cha kutaka kusikika kila siku kwenye vyombo vya habari
Je kama ameshindwa kutekeleza lililo chini ya uwezo wake atawezaje kufukuza mafisadi baada ya siku 90 kama anavyoahidi ilhali yeye si mtendaji?

Au amezuiwa na wakubwa ili kupunguza moto baada ya kulipukiwa na bomu la CHADEMA waliosema kuwa wapo tayari kutoa ushahidi wa kwamba serikali imeishiwa na imekopa kutoka katika mabenki taarifa inayoonekana kuwa tishio kwa CCM na serikali kwani jana waziri wa fedha (Mkulo) alikanusha taarifa hii bila takwimu za kisayansi,

Nini hatma ya kijana Nape kama ameanza kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki akiwa kijana?
 
Mimi najiuliza wanajamvi kama chadema kufanya maandamano na kutoa hotuba za
mwamko kwa wtz ni matumizi mabaya yafedha za umma,je pesa za ccm zinatumika
kufanya nini.
Ingekuwa vyema Nape akatuonesha mfano kwamba wao badala ya kufanya maandamano
pesa zao wamezitumia kuleta maendeleo fulani.
 
Ama kweli CCM imepata msemaje. namshauri Mchambuzi amakalishe chini kijana mwenzeka amsaidie kupanga mikakati na jinsi ya kuongea. CDM ni wa wazi hakuna kitu chini ya uvungu.

Mikutano ya hadhara na maandamano ya CDM ni muhimu sana kwani inaelimisha jamii na kujua umuhimu wa kulinda kodi zao na kuijua katiba ya nchi yao, haki, usawa na wajibu wa kiongozi wa umma. Ni wazi CCM ilifikiri wananchi wataendelea kuwa wajinga siku zote. Ni aibu sana kijana Nape anakosa vijana wenzake hata kuongea nao kwenye mikutano.

Mapacha at work. Zao la ufisadi ni fisadi.Serikali ya mafisadi huteua mafisadi na hulea ufisadi hufikiri kifisadi na huishia kwa ufisadi. mwisho wa ubaya aibu.
 
Nape asiwasumbue kwa propaganda za uongo. Huu ni ujanja wa kukimbia hoja ya kuvuana magamba na siku 90.
Shame on you Nape. Siku zako zina hesabika ndani ya chama cha magamba. Hutasamehewa hata kama ukila matapishi na mavi yako, sasa umeshikwa pabaya na unacheza zumari lao.
Tueleze wale uliowataja mmewapa barua!
 
Magamba yamegoma kuvuka. Anatafuta consolation.
"Maji ukiyavulia ......."
Poleeeeeeee
 
Kama wanashindwa kulipa mishahara, fedha ya kutimizia zile ahadi za trilioni 90(ikiwa ni pamoja na kuufanya mji wa Kigoma kuwa kama Dubai) itatoka wapi?
Wanasikitisha hawa magamba!
 
Mji wa Singida leo ulitekwa na CCM ndani ya Stendi ya Zamani ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa -CCM Nape Nnauye alitoa tuhuma mbali mbali zinazofanywa na Viongozi wakuu wa CHADEMA ndani ya Chama hicho na Kuelezea kuwa Viongozi hawa kwanza waangalie usafi wa Nyumba yao badala ya Kujinadi kwa usafi nje!
Jumla ya Wanachama 153 walirudisha Kadi za CHADEMA na bendera 87 za CHADEMA zilirudishwa! Ni pale mmoja wa walio rudisha bendera na Kadi za CHADEMA kukiri kuwa tangu ajiunge na CHADEMA amekuwa akiweweseka usiku na kujihisi ana ishi na kitu cha hatari ndani ya maisha yake kwani hata akigombana na majirani zake basi anajihisi kuandamana! Aliwavunja mbavu watu kwa kusema Chadema ni Chama cha Wahuni ambao hata Katibu wao Mkuu akiamanisha Dr Slaa hajaoa hadi leo na kusema kama mtu familia inamshinda kuishi na mwanamke ni ajabu kwa wanao mfuata kwani kwa Mila za Kiafirika Slaa bado anatakiwa asipewe siri za mambo ya nyumba hadi pale atakapo kua na kujitambua na kuoa!
Baada ya Mkutano huo vijana walizagaa mitaani na kuanza kushusha bendera zote za CHADEMA na kuharibu kila kitu chenye nembo ya CHADEMA. Kutokana na Uvunjifu huo wa amani polisi waliingilia kati na kuna vijana walikamatwa na hadi jioni walikua wameshikiliwa na polisi. Mkutano huu uliendelea huku kukiwa na mvua kubwa Mkoani Singida! Nape amesema Vijana wana haki ya kulinda Taifa na amani ya Nchi yao na kuendelea kuichagua CCM!
 
Waichague ccm???una akili timamu au kula yako ipo ccm?hakuna kitu hakuna mtanzania mwenye akili timamu wa leo anayeitaka ccm,kwa lipi haswa?sijui kwa wana singida maana ki umaskini ndio mkoa unaongoza pamoja na kuwa na ngombe,alizeti,vitungu,asali,mbao na mbunge muhindi toka bombay!
 
Back
Top Bottom