Hivi kweli tumeshindwa kabisa kuamshana na kushindana kwa hoja? Nadhani nape ni makini sana, sidhani kama na yeye ataingia katika mtego wa orodha maana katika mazingira ya azimio la zanzibar, there is a very thin line between fisadi na tajiri. Let us focus on key issues zinazowagusa wananchi jamani, ufisadi upigwe vita but usisimamishe mambo mengine muhimu, kama vita inanoga hivyo, basi tuunde vitengo kwenye vyama vyetu kupiga vita ufisadi e.g. katibu idara ya kupiga vita ufisadi🙂 ili wengine waendelee na mambo mengine muhimu (sina maana vita dhidi ya ufisadi sio muhimu).
Mchambuzi heshimu mkuu,
Kwanza Nape sio makini kabisa, angekuwa makini na ujana wake asinge ropoka, kama kweli hawakujadiliana kuwafukuza mafisadi , kwanini aje na uzushi, sasa mafisadi hawafukuzwi na bado mnamwita makini labda umakini CCM unamaana nyingine.
Ndugu Mchambuzi, ukiwa mtaalamu wa uchumi nafikiri unajua kabisa huwezi kuendelea kuendesha nchi kwa kukusanya mapato kama kuna wizi, rushwa, mikataba mibovu na uzembe unaosababisha serikali kushindwa kujiendesha na kuletea wananchi wake maendeleo. Kukataa kuliongelea hili tatizo ni kuficha maradhi.
Wizi, rushwa, mikataba mibovu na aina yote ya ufisadi ndio vinasababisha hasara kubwa sana ya mapato ya taifa. Rushwa imesababisha mpaka leo nchi ipo gizani ikisaidiwa na mikabata mibovu, angali IPTL, Richmond nk. Na Rushwa hii inazaa kukataa miradi yote ya kudumu ya nishati kwani wanakula kwenye mikataba ya mlipuko hawako tayari kuiona serikali wanayoitumikia ikitatua tatizo.
Kama umewahi kungalia ripoti ya CAG utaona fedha nyingi zinavyopotea kwenye mikono ya mafisadi, ukusanyaji wa ushuru, matumizi mabovu ya halamashauri, ikulu, na wizara karibu zote. Nchi ingeweza kujiendesha kwa asilimia kubwa kama tungeziba mianya ya ufisadi wa aina yote kwa asilimia angalau 75.
Mfumuko wa bei unasababishwa na fedha chafu za ufisadi. Leo mtu kaiba bilioni kadhaa anataka kiwanja kwa bei yeyote, wanapandisha bei ya bidhaa kwani hawana jasho na fedha, na tuposema ufisadi tunamaanisha kuanzia rushwa za bandari, TRA, Polisi, mahakama, wizara, hospitali nk. Kama wengi wenye akili wang'eishi kwa pato halali mfumoko wa bei using'ekuwa mkubwa hivyo. Ila kubwa zaidi ni pale serikali inaposhindwa kuziba mianya ya wizi, rushwa, na uzembe hata pale ilipowazi kuona.
Kwa hiyo mheshimiwa mchambuzi, unataka tuakae kimya haya yote yakitokea ukitegemea nchi kuendelea. Kweli mchambuzi nawe hutaki kuwa bilionea kwa pato halali kwa miaka minne kama Riz1? Kwanini tusiambiwe hizo biashara halali au ni kodi za wananchi? Fedha zinazopotea kwa wasteful spending zinaweza kuifanya nchi indelee hata centimeters kadhaa kwa mwaka.
Mtaalalumu yeyote au mshauri yeyote kabla hajashauri lazima ajue matatizo yako kwa kina kabla hajakusaidia kuyatatua. na ni kawaida ya wanaoshindwa kuogopa kusema nini matatizo na wanayaogopa hata kuyataja.
Mchambuzi naomba utuletee kitu zaidi kinachotufanya masikini zaidi ya Rushwa, uzembe, wizi, mikataba mibovu, ubakaji wa demokrasia na kutokuwajibika na kwa neno moja tunaita UFISADI.