Nape mnafiki? Sasa amsifu Rostam hadharani huko Igunga

kapotolo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2010
Messages
3,728
Points
1,225

kapotolo

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2010
3,728 1,225
Nape Moses Nnauye ambaye siku za hivi karibuni alikuwa akipita huku na kule akiwananga mapacha watatu kwamba ni magamba, ndio yamechangia kuipa CCM ushindi mdogo, na kwamba lazima waondoke CCM. Moja ya magamba hayo ni Rostam Aziz.

Katika hatua inayoonyesha unafiki wa Nape na uongo wake uliotukuka wa kuwahadaa wananchi wa Igunga, Nape ameanza kumsifia Rostam Aziz huku akiomba watu wasimbeze kwa kuwa amefanya makubwa huko Igunga. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo, Nape amesema kazi aliyoifanya Rostam ndio kigezo cha ushindi wao huo Igunga.

Naomba watu wa Igunga msidanganyike tafadhali, huu uongo wa CCM wa kujipendekeza siku za uchaguzi unatakiwa ukataliwe kwa vitendo kwa kuwakataa huko Igunga. Nape anawafanya watanzania ni wajinga, kwamba anaweza kusema chochote leo na kesho akasema kingine na watu wakamsikiliza. Nape siasa za kuhadaa watu hazina nafasi kwenye dunia ya sasa, acha unafiki wako.
 

Maarko

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
1,150
Points
1,500

Maarko

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
1,150 1,500
Tatizo siyo Nape bali ni CcM kwa Ujumla,wamezoea kuwadanganya watanzania hata kwa jambo ambalo haliwezekani kila kipindi cha uchaguzi,hebu fikiri Ahadi za uchaguzi za ccm zimefanywaa?
Wanawafanya watanzania wajinga mno,ili kukataa kuonekana wajinga wana Igunga msiichague ccm kabisa.
 

Rejao

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2010
Messages
9,243
Points
1,500

Rejao

JF-Expert Member
Joined May 4, 2010
9,243 1,500
Hapo sioni Unafiki wowote!
Rostam aliamua kuwa Accoutable (ni watanzania wachache sana wanaoweza kuachia madaraka-Oly Rostam & Lowasa hav done that)
Alifanya mambo mengi sana Igunga na kila mwana Igunga anayakubali- ndio maana tulishuhudia vilio siku ile alipokuwa anatangaza kung'atuka.
Kitendo cha Nape kumsifia kwa aliyoyafanya ni sahihi kabisa.
Ulitaka amponde kwa aliyowafanyia watu wa Igunga ambayo yanaonekana wazi wazi?
Wewe ulianzaisha hii thread ndio mnafiki mkubwa na hujui unalozungumza.
 

Rugaijamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2010
Messages
2,930
Points
2,000

Rugaijamu

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2010
2,930 2,000
Hapo sioni Unafiki wowote!
Rostam aliamua kuwa Accoutable (ni watanzania wachache sana wanaoweza kuachia madaraka-Oly Rostam & Lowasa hav done that)
Alifanya mambo mengi sana Igunga na kila mwana Igunga anayakubali- ndio maana tulishuhudia vilio siku ile alipokuwa anatangaza kung'atuka.
Kitendo cha Nape kumsifia kwa aliyoyafanya ni sahihi kabisa.
Ulitaka amponde kwa aliyowafanyia watu wa Igunga ambayo yanaonekana wazi wazi?
Wewe ulianzaisha hii thread ndio mnafiki mkubwa na hujui unalozungumza.
Kama haya uliyoyaandika ni ya kweli....ubaya wake ndani ya chama ni upi hata mkamwita gamba na kumshinikiza/kutishia kumtimua chamani?ama kweli Jaguar hakukosea kuimba "ccm vigeugeu!"...
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,178
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,178 2,000
Sasa sababu ya kumpa siku 90 ajiondoe CCM au watamfukuza ilikuwa nini kama aliyofanya ni mazuri na si ya kubeza? Chama sasa kimejionyesha wazi kuwa kinaendesha siasa uchwara au kina viongozi wehu wasioweza kukumbuka jana walisema nini au kina wanachama na washabiki wasiweza kutambua mwanga na giza vinatofauti gani.
Hivi ni kweli kuwa bado kuna Watanzania wanaotaka hatma yao itafutwe kwa masihara kama haya?
 

mpondamali

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2011
Messages
441
Points
225

mpondamali

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2011
441 225
hahahahahaha siasa nchi hii (Tanzania)zinastaajabisha sana.na zinakuwa na mvuto kila siku na straring ni NAPE v ROSTAM v LOWASSA v WANANCHI.juzi tuu hapa alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa huyu jamaaa ni fisadi ni gamba na adhma yake imepata kutimia sasa kwa yule fisadi au gamba kujiondoa katika nyadhifa zote ndani na nje ya chama.Sasa anaanza kujikomba tena kwa Fisadi au Gamba alilokuwa analipigia kelele liachie ngazi jamani WHAT IZ WRONG WITH THIS NAPE?JAMAA WALIDHANI UCHAGUZI KWASASA HIVI NI RAHISI KUSHINDA BILA HUYO MTU?JAMANI TUEPUKE NA UNAFIKI WA CCM PALE INAAPOANZA KUWA KATIKA HALI YA UCHAGUZI.
 

AlamaZA NYAKATI

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
274
Points
0

AlamaZA NYAKATI

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
274 0
kwanza nape kwa jinsi alivochafua hali ya hewa ndani ya ccm sikutegemea kama angetia mguu igunga. Naamini watanzania wa leo si wajinga kiasi hicho, nape anataka kutuambia nini tena wakati amewadhalilisha RA na EL mpaka kuwavua nguo, na RA aliposhindwa kuvumilia kashifa za nape akaamua kuachana na sia za uchwara za ccm. Leo anakwenda igunga kuwaambia nini watanzania. sasa kwa jinsi wanavyojichanganya naamini ni wazi aanguko lao ni kubwa sana hapo igunga na kwingineko
 

JENSENE

Member
Joined
Mar 7, 2011
Messages
52
Points
0

JENSENE

Member
Joined Mar 7, 2011
52 0
Katibu mwenezi wa CCM amedai kuwa wananchi/vyama vya siasa wasimbeze ex -mp of Igunga kwani amefanya mambo makubwa kama kuchimba visima na kupandisha bei ya pamba. Nape amesahau kuwa ni miongon mwa watu ambao walimponda Rostam na kumshawishi kujihudhuru kwake. Iwaje leo aonekane tena mtu mwema? Tusidanganyike,hii ni njia ya kuokoa Igunga. Tutafakari pamoja tunasonga au tunarudi nyuma?
 

Michael Scofield

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Messages
1,225
Points
1,195

Michael Scofield

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2011
1,225 1,195
Rostam naye kama si mnafiki kwa kusema ameachana na siasa uchwara tutaona reaction yake
Rostam hawezi kuepuka kumpigia debe mgombea wa chama chake, amelazimishwa atake, asitake.

Kamati kuu ya ccm ilimwambia kama atakataa kumkampenia mgombea wa ccm, itaanika mambo yake hadharani. Kwahiyo mtakavyomuona Rostam kapanda jukwaani Igunga ni kwa sababu ya kuiridhisha ccm.

Lakini jamaa hana hamu na CC ya chama chake na hakutaka kabisa kushiriki ila hana jinsi, isipokuwa kuitegemea ccm ili madhambi yake yawekwe pending.
 

NDOFU

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Messages
656
Points
195

NDOFU

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2009
656 195
Kila kitu kinakwenda kuwa wazi juu ya ccm' hakika ni mpango wa Mungu kuudhihirisha umma unafiki wa ccm' kuwasili kwa Nape Igunga ni katika kuendelea kuibua tu unafiki wa ccm maneno yake hasa yatakuwa na maana kubwa sana katika hili' nyinyi subilien mtaona mengi yanakuja.

Hakika ni ajabu' upande wa kulia anamtaja RA kama fisadi gamba na mtu ambaye ameipa taabu ccm katika kupata ushindi wake,upande wa kushoto anamuona RA kama mtu safi mwanasiasa makini na mhimu ndani ya ccm aliyeleta maendeleo ndani ya Igunga!

Haya bana.
 

Mwita25

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Messages
3,838
Points
0

Mwita25

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2011
3,838 0
You have to give the devil his due. Rostam alikuwa fisadi upande mmoja lakini upande mwingine ni mwanamaendeleo na mchangiaji mkubwa sana. Amesidia miradi mingi sana ndani ya Igunga na hata nje yake. Kwahiyo sidhani kama kuna tatizo tukimpa sifa zake ingawa ni kweli ameshiriki kwenye ufisadi mkubwa sana.
 

Forum statistics

Threads 1,379,573
Members 525,451
Posts 33,749,512
Top