Nape Masasi kamuacha nani?

Napata wasi wasi kama DC wa Masasi bw Nape Mnauye anawataumikia ipasavyo wananchi wa huko kwa mujibu wa uteuzi wake,maana kila kukicha yeye na vyombo vya habari tu kupiga propaganda za chama.Ni vema basi angechagua moja (kama bado ni DC) kikutumikia chama chake kuliko kupoteza resources (maana analipwa mshahara,marupuru,usafiri etc) kutoka kwenye kodi zetu kwa kazi asiyoifanya.

Ni wazo tu.

Acha kufuatilia maslahi ya watu, hivi unafahamu kwamba nafasi za ukuu wa mkoa au wilaya hata zikifutwa hakuna litakaloharibika japokuwa wanatumia pesa kubwa sana ya walipa kodi, mimi ninavyo fahamu ni kwamba hizo nafasi zilikuwa created kisiasa zaidi ili kila ofisi ya serikali ipate muwakilishi wa chama kama ilivyo kwa mawizara, kila wazara lazima iwe na waziri na kila mkoa au wilaya lazima kuwe na mkuu wa mkoa au wa wilaya. Ukitaka uthibitishe hilo hebu angalia mkoa wa Dsm hauna mkuu wa mkoa kwa mda sasa lakini hakuna lililoharibika au nenda Masasi kawaulize kama kuna kitu kimesimama kwasababu yake.
 
Mamlaka ya uteuzi haijateua mtu mwingine kushika u-DC vinginevyo anaweza kushika nafasi zote- moja ya kisiasa na nyingine ni ajira
 
Kwa mwendo huu kazi tunayo kuelimisha umma mtu anatetea ulimbikizaji wa vyeo pasipo kujua ufanisi na ajira zinavyobanwa mfano hebu angalia Mh Lukuvi ni mkuu wa mkoa wa dar,mbunge na waziri eti hakuna hasara labda wanalipwa mawe
 
Wanajamvi Nape kazi yake ya uDC ni kitu gani iwapo hata mkuu wa Kaya anaweza akamaliza muda wake mwingi wa kazi anatembeza bakuli na kubembea tu ughaibuni akiwa na msafara wa maofisa kibao Kwa ufupi nchi hii inajiendesha yenyewe kila sekta kama ndege za kijasusi
 
Kwa mtindo huu wa lundo la wateuliwa unamnufaisha mteuwaji mara nyingi. TZ hatutoki ng'o.
 
Mswahili ukitaka ukamuue kiwango kisiasa akaboronge mpaka apate kusahaulika haraka kama king'ora cha gari la zimamoto linalokuja kwenye tukio bila maji, wewe kamrundikie tu mi-vyeo baasi kwisha kabisa.

Kama unaona vipi hebu kamtazame Nape mwenyewe, Zitto Kabwe, Mhe Kikwete, Bashe, ... basi shida tupu na wala hutosikia wakikukatalia kwamba kwa sasa ninayo majukumu mengi sana hivyo sitoweza kukubali kupewa vyeo zaidi.

Huyu nnape ni dc ila takribani wiki 2 sasa yupo kwenye siasa je huo u-dc kampa nani?maana muda wote huo sijasikia anatangazwa kuzindua mradi wowote wilayani masasi.na je itakuwaje mwanasiasa kama huyu mambo wilayani yaemde vizuri kama sio kisiasa zaidi?wana masasi mpo wapi?peoples power
 
Viongozi wafike mahala wajenge uwezo wa kukataa vyeo zaidi ili kulinda usalama, tija na ufanisi wa utendaji wao katika eneo moja bila kuathiri eneo nyingine; wasiongozwe to na mvuto wa fedha zaidi katika kila cheo kinachoongezeka.
 
Ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi wa nchi yenye uchumi dhaifu kama wa kwetu. Lakini kuna yeyote anayeliona hilo?????????? Utadhani tulivyorithishwa mifumo fulani na wakoloni basi kuna baadhi ya maeneo walitupiga biti tusiyatazame kiubunifu zaidi ili kuhakikisha ufanishi zaidi lakini kwa unafuu zaidi wa gharama.

Nadhani hatuhitaji Ma RC wala MDC ni matumizi mabaya ya Serikali kwa kweli.
 
hivi dc akienda likizo nani huwa anabaki? i mean sisemi kwamba ni sahihi kuzunguka huko katika gamba la CCM lakini haimaanishi hamna mtu

Kwa taharifa yako unapo kaimu unakuwa figure tu na uwezi kufanya serious maamuzi. Kuna kiwango cha kuamua mengine mpaka jamaa awepo physically. Na ndo maana mambo mengi ya kiutendaji uchelewa kwa sababu mhusika mpaka arudi. So wana Masasi wanayo haki ya kumtaka mkuu wao wa wilaya awepo kufanya shughuli za maendeleo.
 
Kazi ya uDC aliiacha mara tu alipochaguliwa kuwa katibu wa itikadi.

Naomba ufute hii thread kwa kuwa haina faida kwa maslahi ya Taifa.
 
Kazi ya uDC aliiacha mara tu alipochaguliwa kuwa katibu wa itikadi.

Naomba ufute hii thread kwa kuwa haina faida kwa maslahi ya Taifa.

Uko sahihi kabisa, lakini kuhusu maslahi ya Taifa sijawahi kuona wewe ukianzisha thread yenye maslahi ya Taifa.
Ndugu blooklyn ondoa hii thread haina tija.
 
Back
Top Bottom