DOKEZO Matumizi mabaya ya ofisi na maandalizi ya upigaji pesa za miradi ya maji-Mpanda

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Anonytz

New Member
Nov 12, 2022
3
2

MATENGENEZO YA GARI TOYOTA HILUX VIGOR DFP 6939

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mpanda (Eng Hussein Salum Nyemba) aliyepewa usukani na wizara ya Maji kuiongoza taasisi hiyo muhimu kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa Mpanda kuanzia tarehe 31-08-2022. Wiki moja baada ya kuanza majukumu yake mapya ofisini (Tarehe 06-09-2022) akaagiza gari namba (Toyota Hilux Vigor DFP 6939) kupelekwa Tabora kwa ajili ya matengenezo, akielekeza jina la gereji inayoitwa (Supreme Garage) bila afisa manunuzi Bi Grace Christopher Sinkamba wala bodi ya manunuzi kujua chochote. Taarifa kwamba gari ipo Tabora kwa ajili ya matengenezo ilikuja na hati ya madai (Invoice) ya Tsh milioni 38, hata hivyo gari mpaka sasa haijarudi na hakuna anayejua ilipo zaidi yake yeye na dereva aliyemuagiza kuipeleka.

Utaratibu wa Matengenezo ya Gari ya Taasisi ya Umma kutoka katika mwongozo wa matengenezo ya magari.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ndio uliokasimishwa dhamana ya kusimamia matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo ya serikali kupitia kanuni za Sheria ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kanuni ya 137 ya mwaka 2013 na marekebisho yake ya mwaka 2016, ambayo inazitaka Wizara, Idara, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Taasisi za Umma, Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji, Wilaya na Sekretarieti za Mikoa na Wilaya au Taasisi yoyote, pamoja na watu binafsi watakaohitaji kupatiwa huduma na TEMESA kufuata muongozo/sheria hiyo.

Hata hivyo pamoja na kuwepo Sheria ya Ununuzi wa Umma kama muhimili wa kusimamia taratibu za matengenezoya magari, pikipiki na mitambo ya serikali, kuna baadhi ya Taasisi za serikali zinatafsiri isivyo sahihi na kujenga dhana kuwa sheria ya Ununuzi wa Umma imeruhusu matengenezo kufanyika bila idhini ya TEMESA, dhana ambayo sio sahihi. Hali hiyo ya kutotumia TEMESA imesababisha kazi na huduma zinazotolewa kwa taasisi za Serikali kufanywa kinyume na matakwa ya sheria na baadhi kutumia vipuri feki ambavyo vina viwango hafifu visivyoendana na thamani halisi ya fedha iliyotumika.


(Home | TEMESA)

Hata baada ya kuelekezwa na management yake kuhusu utaratibu wa matengenezo ya gari ya taasisi, alikataa gari isirudi kwa ajili ya utaratibu kufuatwa, akasisitiza na kushinikiza gari itengenezwe Tabora katika gereji aliyoagiza. Baada ya malalamiko ya chini ya wafanyakazi, bado aligoma na kutoa vitisho vya kuwaondoa kazini watumishi au kuwahamisha kwa nguvu wale ambao hawaendani na matakwa yake.

MSHAHARA WA MKURUGENZI WENYE UTATA

Mara baada tu ya Mkurugenzi kuanza kazi aliagiza alipwe mshahara kupitia mishahara inayolipwa ofisini, bila kushirikisha bodi, Mhasibu aliamuliwa na Mkurugenzi kumlipa mshahara kupitia akaunti namba 0152315647300 wa Tsh 3,791,000/= baada ya makato bila barua wala kufwata muongozo wa ofisi wala bajeti ya taasisi hiyo. Mshahara huo wa Mkurugenzi ni nje ya kulipiwa nyumba, mawasiliano na posho mbalimbali. Mtumishi anayemfuatia Mkurugenzi kwa mshahara analipwa Tsh laki saba (Tsh 700,000/=).

Historia

Mamlaka ya Maji Mpanda haijawahi kulipa mshahara Mkurugenzi, hii ni kutokana na sababu mbili kubwa
 • Mamlaka kutokuwa na uwezo wa kuajiri Mkurugenzi wake
 • Mkurugenzi kutoajiliwa na bodi ya wakurugenzi, huletwa kutoka wizarani. Hivyo wizara imekuwa ikilipa mishahara wakurugenzi wote kabla ya sasa.
Uwezekano wa Mkurugenzi kulipwa mishahara zaidi ya mara moja

Kama Mkurugenzi (Eng Nyemba) ni mwajiliwa wa wizara tangu tarehe 02-06-2009 akiwa wilaya ya Ludewa akilipwa mshahara kwa ngazi ya TGS C (Tsh 193,340), kwa nini sasa amedai mshahara mwingine Mamlaka ya maji Mpanda bila barua yoyote na amekataa swala hili kujadiliwa na bodi ya wakurugenzi? Je, wizara ilisitisha lini kumlipa mkuu huyo mshahara? Nani kapanga mshahara wa Mkurugenzi?

UNUNUZI WA PIKIPIKI 30

Mnamo mwezi wa kumi mwaka 2022, Mkurugenzi aliagiza ununuzi wa pikipiki 15. Afisa manunuzi alitangaza TANEPS kama utaratibu unavyotaka. Kwa sababu ambazo anazijua Mkurugenzi na afisa manunuzi wake, pikipiki hazikununuliwa kupitia ushindani wa TANEPS kama utaratibu unavyotaka.

Tarehe 24-10-2022 zilinunuliwa pikipiki 30 badala ya pikipiki 15 zilizotangazwa awali TANEPS aina ya TVS kwa jumla ya shillingi milioni tisini na tisa (Tsh 99,000,000/=) sawa na Tsh milioni tatu na laki tatu kwa pikipiki moja (Tsh 3,300,000) . Mkurugenzi alilazimisha kampuni kupewa kazi na kuuza pikipiki hizo. Tarehe 04-11-2022 mkuu wa mkoa wa Mpanda Mh Mwanamvua Mrindoko alialikwa kuzindua pikipiki hizo.

MpandaUzinduzi.jpg


Bei Sokoni

Gharama ya pikipiki moja aina ya TVS kwa bei ya soko ni Tsh 2,550,000/= badala ya Tsh 3,300,000/=. Hivyo kwa kila pikipiki moja bei imeongezwa Tsh 750,000/=

Kwa pikipiki 30 zilizonunuliwa imeongezwa jumla ya Tsh 22,500,000/=.

Ugawaji wa Pikipiki hizo.


Ugawaji wa pikipiki ulifanyika siku ya tarehe 10-11-2022 kwa watumishi na chakushangaza pikipiki 6 zikakosa watu ikabidi Mkurugenzi aanze kutafuta mtumishi yoyote apewe. Hii inaonyesha zilinunuliwa bila kujua uhitaji halisi wa taasisi na mkubwa huyo kutumia njia hiyo kujipatia kipato.

 • Pikipiki zilinunuliwa bila kuomba kibali kutoka TEMESA.
 • Pikipiki hazikufanyiwa ukaguzi na TEMESA baada ya kununuliwa.

AJIRA ZENYE UTATA

Kwa muda wa miezi miwili tangu aingie ofisini, bila kufwata utaratibu wowote wa ajira, bila bodi ya Mamlaka ya maji Mpanda kujua chochote na bila kikao chochote cha bodi, Mkurugenzi kaajili watumishi wanaokadiliwa kuwa zaidi ya thelathini na tano (35) bila usaili na kuwapa mikataba, huku akitisha kwenye vikao rasmi vya utendaji mtumishi yeyote kuhoji lolote (Ushahidi wa sauti upo).

Chanzo chetu kimefanikiwa kupata taarifa za baadhi ya waajiliwa hao na akaunti namba za mishahara yao bank ya CRDB.

JINA
KIASI
BANK ACCOUNT
ZULFA RAMADHAN SHAABAN
340,488​
0152627654900​
FATUMA MALOTI MVUNGI
340,488​
0152376491100​
AISHA ALLY GINGI
454,200​
0152690912000​
ISDOR LAZARO MWINUKA
784,500​
0152404189000​
WAITON ELIAS PONELA
616,500​
0152696862600​


Jambo linaloshangaza zaidi ni uajiri wa watumishi ambao nafasi zao zilikuwa na watendaji. Mfano wahasibu, wasimamizi wa ufundi, surveyors etc. Mamlaka haikuwa na upungufu wa wafanyakazi katika maeneo hayo. Kwa sasa ofisi moja ya uhasibu imerundikwa na wahasibu watatu (Wawili zaidi wakiwa wameajiriwa na Mkurugenzi bila usaili wala uhitaji)

Bajeti ya Mamlaka (2022/2023)

Katika bajeti ya Mamlaka mwaka 2022/23 mamlaka haikupanga kutoa ajira mpya, cha kushangaza Mkurugenzi kaamua kuajiri na kulipa mishahara watumishi hao bila utaratibu wowote.

Maswali ya Msingi ya Kujiuliza

 • Kibali cha ajira kiliombwa?
 • Tangazo la ajira lilitoka?
 • Usaili umefanyika? Kama ndiyo, lini na wapi? Na nani aliusimamia?
 • Nani anaempa nguvu nje ya sheria Mkurugenzi huyu?
 • Nani anamkingia kifua Mkurugenzi huyu?
UHAMISHO WA GHAFLA WA AFISA MANUNUZI
 • Baada ya afisa manunuzi (Bi Grace Christopher Sinkamba) kukataa kutoa ushirikiano kwenye baadhi ya manunuzi ambayo Mkurugenzi huyo ametaka yafanyike bila kufwata utaratibu, afisa manunuzi huyo alihamishwa na kupelekwa Mamlaka ya maji Sumbawanga bila kufuatwa utaratibu wowote. (Mamlaka ya maji Sumbawanga tayari ina afisa manunuzi wake).
 • Bi Elizabeth Pius Ndowo, aliletwa mara moja kuchukua nafasi ya Bi Grace Sinkamba aliyeondolewa, Bi Elizabeth akalazimishwa na Mkurugenzi huyo kutoa kazi kwa kampuni Fulani (Jina kapuni) bila kufwata utaratibu, baada ya mabishano makali na afisa manunuzi huyo kumtaka Mkurugenzi huyo kuandika maandishi ili aweze fanya matakwa yake na Mkurugenzi kugoma kuandika, afisa manunuzi huyo aliamua kuacha kazi mara moja (Siku alizodumu kazini hazikufika 10).
 • Baada tu ya Bi Elizabeth Pius Ndowo kuondoka ofisini, Mkurugenzi alileta afisa manunuzi mwingine anayeitwa Bwana Abdulmalik Nassibu na kumpa kuongoza idara ya manunuzi mara moja. Bwana Abdulmalik ameonekana kukubaliana na Mkurugenzi huyo katika manunuzi yenye utata yaliyoshindwa kufanyika hapo awali.
The Public Procurement Regulatory Authority (PPRA)
 • Ndani ya siku saba, Mkurugenzi kabadilisha maafisa manunuzi aliowaleta na kuwajulisha PPRA kuwafungulia akaunti kwa ajili ya kuendelea na shugulia za manunuzi.
Abdulmalik.JPG


Elizabeth.JPG


UTATA ZABUNI YA UNUNUZI WA MABOMBA NA VIUNGO VYAKE
 • Zabuni namba AE/114/2022/2023/G/4-1, AE/114/2022/2023/G/5, AE/114/2022/2023/G/6-1 na AE/114/2022/2023/G/6-2 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili (Tsh 2,000,000,000/=) zimetolewa kwa shinikizo kubwa la Mkurugenzi.
Ilivyokuwa
 • Mkurugenzi alimfwata afisa manunuzi akimtaka aweke tangazo la kutafuta mzabuni katika mtandao (TANEPS) lakini akampa majina ya kampuni anayotaka yeye wapewe. Huku akisisitiza zabuni hizo ziwe restricted kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.
 • Baada ya mabishano makubwa na afisa manunuzi (Bi Grace Sinkamba) juu ya utaratibu wa manunuzi kufuatwa, Bi Grace alijulishwa siku inayofuatwa kwamba amehamishwa ofisini na atakuja afisa manunuzi mwingine.
 • Baada ya siku mbili Bi Elizabeth Pius Ndowo aliletwa kama afisa manunuzi mpya, na kukabidhiwa jukumu la kutoa zabuni kwa kampuni ambayo Mkurugenzi (Eng Hussein Salum Nyemba) aliitaka, Bi Elizabeth alilalamika juu ya utaratibu pamoja na bodi nzima ya manunuzi. Kwa sababu Mkurugenzi alikuwa akishinikiza sana, na usumbufu wa mara kwa mara, Bi Elizabeth alimshauri Mkurugenzi atoe sababu zinazofanya mchakato wa manunuzi usifwatwe inavyotakiwa. Baada ya Mkurugenzi kutoa sababu hizo kwa mdomo. Afisa manunuzi huyo aliziweka kwenye maandishi na kuhitaji Mkurugenzi huyo aweke sahihi ili aweze kutoa hati ya ushindi kwa kampuni hiyo.

Mkurugenzi agoma kusaini

 • Baada ya afisa manunuzi huyo kumpelekea Mkurugenzi huyo barua yenye sababu alizozitoa, Mkurugenzi alikataa kusaini huku akimshutumu hana Mamlaka ya kumsainisha mwajiri wake. Baada ya tukio hili, afisa manunuzi huyo aliondoka bila kuaga na ikawa mwanzo wa kuleta afisa manunuzi mwingine Bwana Abdulmalik Nassibu.
 • Siku mbili baadae Bwana Abdulmalik Nassibu aliajiliwa kama afisa manunuzi mpya na kukabidhiwa mfupa uliowashinda maafisa manunuzi waliotangulia.
 • Kampuni hizo zipo kwenye mchakato wa mwisho wa kupewa kazi hizo.

TAKUKURU

 • Vyanzo vyetu vya habari vya uhakika vinatujulisha Eng Nyemba kabla ya kupelekwa Mamlaka ya maji Mpanda, alikuwa Mamlaka ya maji Igunga.
Sababu zilizomtoa Igunga
 • Baada ya kugundulika kuwa na matumizi mabovu ya ofisi pamoja na kujihusisha na rushwa, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) – Igunga iliweza kumtia hatiani na kumfungulia kesi (Inasemekana kesi inaendelea). Hili lilifanya arudishwe wizarani. Baada ya kukaa wizarani kwa takribani miezi kadhaa, akateuliwa na wizara kwenda Mamlaka ya maji Mpanda.
 • Vyanzo vyetu vilivyo wizarani, vinatujulisha kuna wakubwa (Kapuni) wanaomkingia kifua mkubwa huyu.
Maswali ya kujiuliza?
 • Imekuwaje mtumishi mwenye kesi mahakamani na TAKUKURU kupewa cheo zaidi?
 • Je, wizara haina chombo chenye uwezo wa kuchuja wakurugenzi wake wanaoteuliwa?
 • Je, aliyempa cheo hicho alikuwa hajui malalamiko dhidi ya mkubwa huyu?
 • Kuendelea kumpa nafasi mkubwa huyu sio kuhatarisha ustawi wa jamii anayoenda kuongoza?

MALALAMIKO YA HUDUMA YA MAJI – MPANDA

 • Mji wa Mpanda umekuwa na malalamiko makubwa ya huduma duni ya maji. Hii pia ni pamoja na swali alilouliza Bungeni Dodoma Mbunge wa Mpanda (Mh Sebastian Kapufi) kwa wizara tarehe 11-11-2022.
 • Nani wizarani yupo nyuma ya mkubwa huyu?
 • Je, TAKUKURU Mpanda haijui haya na mengineyo?
 • Je, TAKUKURU inashindwa kuzuia haya au inasubiri uharibifu na wizi ufanyike?
 • Je, Mh Rais (MAMA SAMIA SULUHU HASSAN) anajua watendaji wake wanavyopanga mashambulizi ya pesa za miradi ya maji?
 • Hizi Tender za thamani ya takribani bilioni mbili kwa ajili ya kutatua shida ya maji – Mpanda ambazo mshindi katangazwa kwa ujanja ujanja, mradi utakuwa na value for money?
Abdulmalik.JPG
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
16,831
34,929
Tatizo la nchi yetu viongozi ni untouchable..Bashiru kaongea kidogo tu kashikwa shati kila kona ..mtoa mada umeandika kwa uzalendo mkubwa ila hili halitafanyiwa kazi nashauri ungeenda na takukuru
 

Anonytz

New Member
Nov 12, 2022
3
2
PART 2
Kwanza kabisa tunashukuru kwa serikali na vyombo vyake kulipa uzito unaoshtahili suala la Mamlaka ya Maji-Mpanda.

Chanzo chetu cha siri sana kutoka wizarani kimetujulisha juu ya
 • Mpango wa kutisha watumishi
 • Mpango wa kuficha ukweli
MPANGO WA KUTISHA WATUMISHI
Kuna mambo mengi hatujaya-report kwa umma (Ushahidi wa sauti, video, nyaraka n.k), tunasikitishwa na mkakati uliowekwa kutisha watumishi. Tunaelewa team yote iliyojipanga kufanya jambo hilo. Tunawaonya, watulie na waache serikali ifanye uchunguzi wake, kuendelea na mikakati hiyo kutatulazimisha kuandika na kuyaachia ambayo ni ya ndani na yataondoa heshima yao na wakubwa wetu wizarani.

MPANGO WA KUFICHA UKWELI
Chanzo chetu kilicho kwenye korido za wizara kinaelezea mkakati uliowekwa kwa ajili ya kuficha ukweli wa jambo hili haswa suala la Tender za mabomba ya maji na viungo vyake. Hii ni kwa sababu kuna WAKUBWA waliokuwa wanashirikiana na Mkurugenzi (Eng Nyemba) kuhofia kutajwa na kuhojiwa na TAKUKURU.

Mkakati huo ukiendelea, tutaleta ushahidi public wa MAJINA YAO, CHECK NAMBA ZAO, NAMBA ZAO ZA SIMU na UNUFAIKAJI WAO IN DETAILS. Tunawashauri tu, waache serikali na TAKUKURU ifanye kazi yake njema.

Acheni kuhangaika kujua sisi ni akina nani, haitawasaidia, jibuni hoja na acheni vyombo vifanye kazi yake. Sisi tunakunywa chai pamoja ila hatutawaacha mtafune pesa za miradi tukiwaangalia.

Tunaipenda sana hii nchi, tunawaonya mnaopanga hiyo mikakati mtulie, muache vyombo vya serikali vifanye kazi yake, hatutawaacha mpige pesa za miradi ya maji wakati serikali inajitahidi kuwaletea wananchi wake huduma karibu.

Mikakati hiyo hapo juu ikiendelea, mtatulazimisha kutoa toleo lingine.
 

Anonytz

New Member
Nov 12, 2022
3
2
Tunampongeza sana Mh Waziri Mkuu kwa hatua alizochukua juu ya hili, tunaamini haki itatendeka maana tuliyoandika hapa ni machache sana, kuna watumishi wengi wameumizwa wao na familia zao sababu tu ya Mkurugenzi kutaka kupiga pesa na watu wake walio wizarani (Waliona wawatoe hao kwenye nafasi zao, mpaka sasa wengine wamefungua malalamiko wizarani na hawashughulikiwi sababu kesi ya Nyani anapelekewa Ngedere- na bahati mbaya nafasi zao alizijaza kienyeji bila utaratibu kama alivyofanya Mpanda na kuwaambia haki watapata mbinguni). Tunafuatilia majina ya watumishi hao kutoka Igunga na Mpanda na tutayaweka hadharani ili waweze kupewa haki yao.

Pili tuna taarifa nyingi sana tumezitunza, tuna ushahidi usio na shaka wa Eng Nyemba na wakubwa wa wizara - Tunajaribu kuacha vyombo vifanye kazi yake, ila vikionekana kumlinda mtu mwenye kesi 16 jumlisha na hizo watapata Mpanda, tutalazimika kumwaga ushahidi wote hapa.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, tunashukuru wote mliochukua hii taarifa na kuisambaza maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Groups za WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii.
Wazalendo wa kweli wa nchi yetu!
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,272
4,662
Mwisho lakini sio kwa umuhimu, tunashukuru wote mliochukua hii taarifa na kuisambaza maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Groups za WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii.
Sawa, ila inaonesha MNACHONGA SANA
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom