Mtwara: Mzazi arejeshewa kichanga alichodaiwa kukitupa porini baada ya kujifungua, hali ya sintofahamu yaibuka

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kichanga cha siku moja kilichookotwa na Afisa Mtendaji, Haridi Karo wa Kata ya Pachani, Mtaa wa Mtandi - Masasi Mkoani Mtwara kimeibua mvutano kati ya Ofisi ya Ustawi wa Jamii Masasi na Polisi wilayani humo.

Mvutano huo umeibuka baada ya Afisa Ustawi wa Wilaya, Leila akishikiriana na Mkuu wa Kituo cha Polisi Masasi kuamua kukikabidhi kichanga hicho kwa mzazi anayedaiwa kukitupa pasipo kuchunguzwa afya yake ya akili.

Akizungumza na Gazeti la Raia Mwema hili kwa njia ya simu, Karo amesema tukio lilitokea jirani na ilipo ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Mtandi; “Kuna dada alijifungulia porini akamuacha kwenye kichaka akaondoa, tulipokwenda eneo la tukio hatukumjua mama wa mtoto ni nani.

“Tukaomba majirani watupe kanga tukaenda kutafuta kiwembe kipya tukamkata kitovu, tukachimba shimo tukafukia uchafu wote pale, tukambeba tukampeleka kituo cha afya kwa ajili ya huduma ya kwanza, tukampatia huduma ya kwanza kichanga kilikuwa kimechubuka chubuka na michanga.

Karo aliongeza kusema: “Baada ya kupata huduma ya kwanza tukakipeleka kichanga kile kituo cha polisi. Baada ya kukamilisha tarativu tukaitangaza taarifa kwa kupigiana simu ili kuweza kuineza habari ya kichanga kutupwa kwa uharaka.

“Tukiendelea na mawasiliano kuna vijana wakatupigia simu kututaka twende waliko wao wakituelekeza kwamba kuna mama mmoja.

"Wanamuona eneo la mchikichini Pachani, tukaenda usiku tukamkata tule mama tukamuhoji akakubali kwamba alikuwa mjamzito, na alifanya hivyo wakati tayari ana mtoto mwingine anayekadiriwa kuwa na umri 12.

“Tukamchukua tukampeleka Polisi, mimi nikafungua jalada la kesi pale kutupa mtoto, mlalamikaji nikawa ni mimi mwenyewe, baadaye akatafutwa Ustawi wa Jamii akafika wakamchukua mama na mtoto wakampeleka kwa Hospitali ya Wilaya kwa Maindo, wakakaa pale wakipatiwa huduma kwa takribani siku tano mpaka waliporuhusiwa kutoka hospitalini Desemba 14, 2022. Mama na mtoto wakarudi Pacha ni akaendelea kuishi eneo lile. Baadaye majirani wakaniambia mbona yule mama aliyetupa kichanga karudi?

“Nikampigia simu Leila mbona mtuhumiwa wangu yupo uraiani? Leila akanijibu kwamba alikuwa anataka anitafute lakini Mkuu wa Kituo cha Polisi amefunga lile jalada la kesi. Anafungaje jalada la kesi wakati mimi ndiye mlalamikaji? Kwa nini asiite mimi?

“Leila akanijibu kwamba OCD ameona zile ni changamoto tu za maisha kwa hiyo ameona yeye amsaidie, nikamwambia hata wanaoiba mihogo ni changamoto za maisha, tafsiri yake ni nini! Tafsiri yake ni kwamba wanaona kinachoendelea kwa aliyetupa kichanga porini wataona kwamba ni tukio la kawaida , kesho atatupa mtu mwingine kwa sababu tu kuna mama alitupa mtoto na ameruhusiwa yupo uraiani.

"Kwa mujibu wa Karo, Desemba 17, 2022 alimuona OCD kwenye gari yake akiwa na Afisa Ustawi, Leila wanapita barabarani wakielekea kwa yule wakaenda wakarudi.

“Desemba 18, 2022 nilikuwa na kikao na Mkurugenzi wa Halmashauri yetu, nikamuona Leila nikamuuliza mbona mlipita jana akasema walipeleka mahitaji kwa yule mama, chandarua, pampas wakampelekea mzazi.

“Nikamuuliza kwa hiyo mtaenedelea kumuhudumia mpaka lini, lakini je huyu mama mmempima akili? Maana tayari mmemuachia na mmemkabidhi mtoto. Akimtupa tena hamkawii kuja ofisini kutoa taarifa za mama kutupa mtoto.

"Leila aliahidi kumueleza hilo suala OCD na aliahidi kunikutanisha naye. Nikawasiliana na mtu mmoja ambaye alipewa jalada langu mimi, unajua Polisi wana utaratibu wa kumpa mpelelezi jalada, simu ikaita haikupokelewa. Desemba 20, 2022 majirani wameniambia usiku wamemuona yule mama akihama na vyombo vyake amevipakia kwenye guta amehama mtaa. Amehamia wapi mimi sijui sasa. Polisi wameshafunga jalada langu mimi siwezi kufuatilia tena."

Alipoulizwa kuhusu maendeleo ya afya ya mtoto, Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya hiyo, Leila Kasuguru alisema suala hilo aulizwe mtendaji kata.

“Ningeomba umpigie mtendaji akueleze vizuri kwa sababu yeye ndiye mwenye eneo lake,” alisema Leila.

Akizungumza na Raia Mwema, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Wankyo Nyigesa alihoji aliyekabidhi kichanga hicho kwa mama huyo ikiwa ni ustawi wa jamii au Polisi: “Nani aliyekabidhi kichanga hicho kwa mhusika, ni Polisi au Ustawi wa Jamii? Ngoja niwasiliane na Polisi Masasi nitarejea kwako,” alisema.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili kwa njia ya simu Mkuu wa Polisi Mtwara, Wankyo alisema "Kichanga kilikabidhiwa kwa Ustawi wa jamii, wasiliana nao".


Chanzo: Mary Victor (Raia Mwema)
 
Kama ametulizwa na kusaidiwa kimaisha na ana akili timamu basi aachwe atunze mwanae atakuja kuwa Mkuu wa polisi Mtwara
 
Back
Top Bottom