Nape: Magufuli aliposema Mwanza wasibomolewe kwa sababu ya kura alikuwa anatania

Haya mnaopenda kumshangilia mshangilieni na leo.. eeeeeh

Au kwa kuwa kasema yeye haji upande wenu!?
Ha ha haaaa.. ila alishayasema haya kabla ma mlijadili humu huku mkilia na machozi yakiwatoka na kujipiga vibao vya usoni pia.
88aafa10ccbc435e429255b8a7f08ad7.jpg
 
Hapa Nape anamaanisha kwamba Polepole ameshidwa kazi aliyomrithi maana hii kauli alitakiwa kuitoa mapema.
 
Huyu mtu kila siku anatania?
Daaah tumechoka kufanywa mapoyoyo
Juzi kasema haongez mshahara
Oohhh mara mlimnukuu vibaya
Juz kaenda kagera kasema watu wanaofanya shughul ktk maeneo yasiyo rasmi wasisumbuliwe bado watasema alikua anatania
Kuna siku kasema zaeni tu watoto wengi nitawasomesha kakatokea kale ka mama ka afya eti alikuwa anawatania
Dadeeeq ccm hamkuchaguliwa kutuletea utani dadeeq tuheshimiane
 
Mbungewa mtama Nape Nnauye akiwa anahojiwa na DW amesema kitendo cha rais Magufuli kusema watu wa Mwanza wasibomolewe kwa kuwa walimpa kura ilikuwa ni utani sababu rais ni mtu anayependa kutania

Amesema pia ameshangazwa na bomoabomoa iliyofanywa kwa wananchi ambao serikali ilikuwa imewarhusu kujenga na kusema jambo hilo halifai

Ameseendelea kusema pia hana mpango wa kuhama CCM lakini hawezi kuapa kama hatahama chama hicho


Nape Nnauye.
Yaani huyu jamaa ni kinyonga
Juzi kasema anambinu zake za kumuua panya.
Sasa sijui huyo panya anauliwa na hizi nyimbo zake..
 
Haijarishi alikuwa serious au anatania, tuseme wazi tu Rais alikosea katika hilo, na anapaswa kukosolewa katika hilo kwa 100%.

Halafu toka lini Rais akawa anatania katika kutoa amri? Rais alisema Ubomoaji ule usitishwe mara moja, na akatoa amri kwenda kwa watendaji wake wote kwa kuwataja kuanzia mawaziri kadhaa kuhakikisha hilo linatekelezwa haraka na kwa uhakika.

To be honest, kama kuna matamshi ya rais aliyowahi kuyatoa akiwa very serious basi hilo la Mwanza ni mojawapo. Kama kuna watu hawaamini hilo, basi watendaji husika waendelee na ule ubomoaji pale Mwanza halafu ndio watamjua Magufuli huwa hanaga utani na kauli zake.
 
Back
Top Bottom