Nape: Lowassa kapoteza sifa ya kugombea

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
sakata la Nape na lowasa limeendelea baada ya Nape jana kumwambia kwa kutangaza nia kabla ya wakati wake amepoteza sifa ya kuteuliwa kupitia chama cha mapibduzi.
maoni yangu: Nabe acha kushindana na Lowasa au umesahau ulivyobanwa kule dodoma ukitakiwa kupeleka ushahidi wa ufisadi wa lowasa vinginevyo umuombe msamaha, ukakomea kumpigia magoti, umesahau ulishatangaza siku 90 vinginevyo ungemg'o mpaka leo Siku 90 imegeuka miaka 90..

source: Mwananchi/RFA


====================
Ufafanuzi wa Nape
====================
 
Nape ni kiongozi wa CCM lakini mwenzake ana kundi kubwa na chama ni watu.Sasa siijui atashindana na huyo jamaa kivipi.Pili Lowassa hakutamka wazi kuwa anataka kugombea ila aliongea kwa mafumbo.

Nape kazi ya kutumika itakuumbua!
 
Nape alisema wote wanaotangaza nia wamepoteza sifa ya kuteuliwa.
Kwa juu nawaona lowasa january makamba sitta sumaye na membe hawa wanatumia lugha ya matendo kutangaza nia.
 

Mkuu mbona sikuelewi?! uko upande wa nani?! ushajikatia tamaa au unakula kotekote?
Je ushauri wako ni ili ccm iendelee kutawala au unajipendekeza kwa lowasa?
 
Acha kupotosha watu weka chote nilichosema. Nilichosema ni kuwa yeyote anayekiuka taratibu za chama katika mchakato ANAJIONDELEA SIFA za kuwa mgombea wa chama hichi!(Labda Chama kiamue kutofuata taratibu zake chenyewe, na kikiziacha hakina namna ya kuendelea kuaminiwa)!

Sasa si swala la Lowassa ni swala la KILA ANAYEKIUKA TARATIBU!kama naye anakiuka anaingia kwenye mkumbo huo, sio kwasababu ni Lowassa ila kwasababu ni mwana CCM na taratibu za CCM haziruhusu! Sio swala la Nape ni swala la taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa kabla hata Nape hajazaliwa!

Haiwezekani watu wagawe rushwa hovyo tukae kimya tu kisa anayegawa flani!!!! Hivi kuna uwezekano wa kuingia na kiti moto msikitini ukapigiwa makofi?!! Unaweza kupigiwa makofi na kupewa uongozi wa kanisa wakati humwamini Yesu Kristo?!! Watanzania tusiogope kusema ukweli maana ndio utakaoiponya nchi yetu.

Kama mnamgombea ana sifa atachaguliwa tu huna haja ya kuongezea sifa zake kwa rushwa! Haya si yangu ya CCM, na ni kwa madiwani, wabunge na hata urais!

HERI YA MWAKA MPYA 2014!
 
Nilini lowasa aliwahi kuwa nasifa za kuwa mgombea...
 
Nadhani Lowassa alisema anaanza na Mungu na kwa Jina la Yesu Kristo atatimiza ndoto yake. Imani hiyo ni juu ya yote na ni juu ya mawazo na mipango na taratibu tunazozijua. Mhimu sasa Mungu mwenyewe aweke mtenda kazi wake.
 
Nape Nnauye na wewe unaamin kwamba ukweli ndio utaiponya nchi???!!
 
Last edited by a moderator:
Nape yuko ccm kimaslahi tu, lakini kimtazamo yuko upinzani kabisa! Lowassa akiukwaa urais nape ahame nchi.

siyo kwamba ni kambi tofauti tu ndiyo maana anatofautina na lowasa na vijana wake kama nchemba, january....wakati kambi yake ni Sitta, mwakyembe...
 
Nape punguza mdomo usijifanye mungu mtu,mimi naunga mkono lowasa kuwa mgombea kwasababu uweza anawo sababu anayo mwisho anamaamuzi magumu nchi itanyooka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…