Nape katua Arusha, kapokelewa kishujaa!

Nape katua Arusha, kapokelewa kishujaa!

Mzalendo K

Member
Joined
Jun 22, 2012
Posts
32
Reaction score
13
Nimeshangaa sana leo nilikuwa mkutano wa CDM kata ya Kimandolu ghafla nikaona kundi kubwa la vijana wanasukuma gari, kuangalia kwa karibu nikaona gari la Nape linasukumwa na vijana wanaimba "Lema byebye"! Nikaambiwa Chalii wa CCM ameingia mjini kuja kumzika Lema! Mkutano wa Chadema ukavurugika vijana wakahamia kushangaa msafara wa Nape.

Hali ya Chadema na Lema Arusha taabani kabisa!
 
Acha uongo.Amezomewa vibaya hapa Kimandolu mpaka anatia huruma.

Acha kupotosha Jukwaa.
 
Muda mrefu Wenzio wameshamwaga hapa jamvini yaliyomkuta Nape, we unatuletea stori za uongo
 
Nimeshangaa sana leo nilikuwa mkutano wa CDM kata ya Kimandolu ghafla nikaona kundi kubwa la vijana wanasukuma gari, kuangalia kwa karibu nikaona gari la Nape linasukumwa na vijana wanaimba "Lema byebye"! Nikaambiwa Chalii wa CCM ameingia mjini kuja kumzika Lema! Mkutano wa Chadema ukavurugika vijana wakahamia kushangaa msafara wa Nape.

Hali ya Chadema na Lema Arusha taabani kabisa!

ndiyo unaamka wakati jua karibu linazama.pole sana ndugu yangu...
 
Kila siku anatukana watu anaowaita Kanda ya Kaskazini.Leo kafuata nini huko?
 
Huwa hamkubali nyinyi. Jamani serikali tatu hapana ni kuongeza umasikini.
 
Acha uongo.Amezomewa vibaya hapa Kimandolu mpaka anatia huruma.

Acha kupotosha Jukwaa.

Mkuu!

Mbona unapoteza muda kujibizana na hao walio BINAFSISHA AKILI zao? Hebu tumia muda wako kututumikia wanyonge tunao subiri uhuru wa kweli.

Ni nani asiye juwa kwamba MAGAMBA wanazomewa kila mahali? Wazomewe Mtwara halafu Arusha washangiliwe??!!! Haitatokea!!!
 
Molemo,hata kama unayo sema ni kweli itakua ngumu sana watu kukuamini

Nimekuwepo kwenye huu mkutano tangia Nape anaingia hadi anaondoka. Hakuna kitu kama hicho kwani waliokuwa wamevaa sare za CCM wengi ni wanywaji wa pombe aina ya banana choka mbaya na wazee na dada poa ambao ramani imepotea na wanajaribu kuitafutia CCM kwa njia ya kuvaa sare ili wakubwa wawahurumie wapewe kama Vick kamata.

Gari halijasukumwa na CHADEMA ni Imara huku Kimandolu kuliko mwanzo na CCM wategemee maumivu kama kawaida. Siongei KISHABIKI KWANI UPEPO UKO VERY CLEAR
 
Nimeshangaa sana leo nilikuwa mkutano wa CDM kata ya Kimandolu ghafla nikaona kundi kubwa la vijana wanasukuma gari, kuangalia kwa karibu nikaona gari la Nape linasukumwa na vijana wanaimba "Lema byebye"! Nikaambiwa Chalii wa CCM ameingia mjini kuja kumzika Lema! Mkutano wa Chadema ukavurugika vijana wakahamia kushangaa msafara wa Nape.

Hali ya Chadema na Lema Arusha taabani kabisa!
Hebu omba radhi hapa jf! Nape yupi apokekewe kishujaa Arusha? Jk mwenyewe hapati mapokezi itakuwa huyu asiye mjua babake?
Nape kazomewa mwanzo mwisho. Kama Mlimshindea Lema mahakamani imekula kwenu. A town wana pata hasira wakisikia neno ccm. Jumapili siobali stay tune. Kusukumwa hata mkokoteni unasukumwa acha Nape
 
tatizo makamanda wa arusha mnaniudhi hamrekodi hata kwa simu hayo matukio..fanyeni hivyo basi
 
Ilitakiwa iwe hivi:
NAPE AZOMEWA KISHUJAA ARUSHA
 
Yani wewe mleta mada umekuja kupotosha hapa jamvini maana habari za Nape zilishafika hapa masaa na kuchambuliwa!!! Au umetuma kupotezea!!
 
Back
Top Bottom