Nape: Dr. Slaa anaiua CHADEMA

sasa natambua kwanini chama cha mapinduzi kimekupa hiyo nafasi kijana mwenzetu!! kumbe nafasi hiyo inatumikiwa na watu wenye majungu fitina na wasiokuwa na weledi wa kuelezea mambo! naomba nikupe tahadhari kuwa kumtoa baba mwenye nyumba nje ya nyumba yake siyo jambo la siku moja unaanza kumsogeza kwanza sebuleni kisha barazani na baadae unamtoa nje ya geti kabisa!!! kupata kata 5 siyo jambo dogo tena bwana Nape, tazama nguvu ya chama cha mapinduzi imebaki vijijini ila mjini ni kushne huko tunapoenda cdm wakifanikiwa kuingia vijijini ujiandae kuwa mpinzani. sifungamani na upande wowote!!!!!!
 
Obama baba (Nape) rusha ndege ya ccm hiyo: m4c ambayo ingeleta matumaini ni kuunganisha upinzani pekee lakini hiyo ya kupitapita kutukana na kupasua mabomu haitamuongezea mlalahoi shibe wala kumletea tumaini
 
DR. SLAA AMECHANGANYIKIWA: Nape
Adai amekubuhu kwa utapeli wa kisiasa
Amtuhumu kuiua Chadema
Asema si M4C tena bali ni M4D



Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.

Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni *kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo *zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.


Nape Moses Nnauye

Sasa kama anaiua yeye si ndio amshukuru anamsaidia kutimiza malengo yake makubwa sasa ndio anasikitika makubwa.
 
PEOPLE POWER........................................... Roooho zao zinawauma wakisikia, hasa nape
 
We mjomba hebu taja jina lako kamili kwa nini unapenda kuficha ukweli? Wajiita Nape ili kuwapumbaza watu nawe uwe wa kusini wakati sisi tulikupa jina zuri tu la NAPEGWA maana yake NIMEPEWA. Sasa nakuomba utumie jina lako kamili ss wajomba tunakasirika na hiyo tabia yako.
 
Back
Top Bottom