Nape: Dr. Slaa anaiua CHADEMA

Nape: Dr. Slaa anaiua CHADEMA

hivi kwenye mtihani ukipata asilimia 20 wakati mwaka jana ulikuwa na asilimia 8 utasema umeshinda ati kwa vile maksi zako za mwaka huu ni mara mbili na nusu ya za mwaka uliopita?

Mwaka jana ulikuwa hujua kusoma na kuandika, leo unajua bado unapata asilimia 20 tu. Uwezo wa Chadema ni zaidi ya asilimia 20. Chadema kimeshindwa vibaya chaguzi hii.
 
Adui akikusifia ujue unapotea,siku zote mpinzani wako hawezi kukupa moyo,kazi yake ni kukuvunja moyo regardless of what you have done!
 
Ukweli usemwe! CCM imepunguza idadi kwa 11% na CHADEMA imeongeza 60% ... Kwanini wengine wabishi humu? CCM propagandist NAPE lazima aseme uongo, hiyo ni kawaida kwa CCM. Tuwape baibai tu. Tunaendelea kuwabandua mdogomdogo mpa weshe.

Baibai haiji kwa kuongeza kata 3 wakati wenzenu wameweza kutetea kata zao 27. Wapi na wapi? Nape ana haki zote za kutamba. Kama viongozi wa Chadema wameridhika na matokeo haya kweli inasikitisha na kutia sana uchungu.
 
DR. SLAA AMECHANGANYIKIWA: Nape
Adai amekubuhu kwa utapeli wa kisiasa
Amtuhumu kuiua Chadema
Asema si M4C tena bali ni M4D

Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.

Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni *kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo *zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.
 
Sleep walkers cum day dreamers!! angalia msijikwae mtaumia!! Change is irreversible no matter what doom sayers and professional Vuvuzelas say and do, period.
 
Nianze kwa kusema Nape amepewa nafasi kubwa katika chama cha CCM lakini hatambui hilo anaipeleka CCM shimoni, ukiwa na upeo mdogo kama wa Nape hustahili kupewa nafasi nyeti kama hiyo,

Nape alitakiwa kujua ushindi waliopata CCM katika chaguzi ndogo za madiwani ni kama kupoteza CHADEMA wamerejesha viti viwili na kuchukua zaidi vilivyokuwa vya CCM , hiyo haitoshi jumla ya kura walizopata CHADEMA katika chaguzi hizo ni nyingi sana tofauti na yeye anavyofikiria. ukiwa na kiongozi kama huyo kwenye chama ni janga
 
Nianze kwa kusema Nape amepewa nafasi kubwa katika chama cha CCM lakini hatambui hilo anaipeleka CCM shimoni, ukiwa na upeo mdogo kama wa Nape hustahili kupewa nafasi nyeti kama hiyo,

Nape alitakiwa kujua ushindi waliopata CCM katika chaguzi ndogo za madiwani ni kama kupoteza CHADEMA wamerejesha viti viwili na kuchukua zaidi vilivyokuwa vya CCM , hiyo haitoshi jumla ya kura walizopata CHADEMA katika chaguzi hizo ni nyingi sana tofauti na yeye anavyofikiria. ukiwa na kiongozi kama huyo kwenye chama ni janga
Mkuu nakuomba KWA HERUFI KUBWA mwache Nape wetu, usimsumbue kabisa na wala usimpigie simu kumweleza haya, utamwaribia program zake zote.....Mwache kwani Nape ni njia ya ukombozi wa fikra kwa watanzania wote na tuzidi kumwombea...yeye ni ngazi ya pili toka juu tunakoelekea. Acha tuvuke hapo salama kumfikia mwenyekiti. Na hii nadhani itakuwa ni 2015...Tumwombeeni kwani naona ameanza kujitambua kutokana na dose kali ya M4C. Gamba lake limeanza kulainika sasa tusimfanye kuwa mgumu tena.
 
Kupoteza kata tatu siyo mchezo inabidi tutafakari wana ccm wenzangu,wenzetu wametetea kaza zao
nakutunyang"anya zetu inabidi tutafakari.hata mbuyu ulianza kama mchicha.
:fencing:
 
hata mimi nafikiri watu amestuka ndio maana kusini hakuna chadema
CHADEMA inabidi ijipange upya kama iliwekwa na kanisa basi ilikane kanisa maana wengine humu humu wameanza
kukiita chadema chama takatifu.CHADEMA ikitaka kuongoza nchi hana budi padre slaa kutogombea kwa hali ilivyo sasa kati
ya waislam na wakristo alaf wamchague padre ni ndoto kwa hiyo slaa aachie ngazi amepoteza mvuto
 
NKADABWI;Uliposema kuwa Dr Slaa apumzishwe ni propaganda tu na hata ww unajua hivyo na propaganda HAZIWEZWI ACHWA ZIPITE bila kujibiwa!CCM wamepoteza viti 5 vya udiwani lkn HUJASEMA KAMA sasa Nape anapaswa ajiuzuru LKN CHADEMA na kuongeza viti 4 zaidi unasema viongozi wake wa kitaifa wapumzishwe>>>>>>>WHY?Walio ongeza viti vya udiwani ndiyo viongozi wake wanapaswa kupumzishwa na wala sio wale waliopoteza viti?

NO SENSE!

kazi ipo nchi hii
:A S 11: :A S 11:
 
Kati ya Kata 26 zilizokuwa chini ya CCM, wamepata kata ngapi? Nape acha hesabu za ngumbaru. Pamoja na tume mbovu ya uchaguzi na kutumia green guard na jeshi la polisi na tiss bado kata zimepungua toka 26 mwaka 2010 mpaka 22 mwaka 2012! Na mume wenu Mamvi ndio anapiga jaramba hivyo mwaka huu waropokaji chu.pi zitawabana! Mliomwita Gamba sijui mtakimbia nchi!

:bange::attention::second:Mropokaji wa magamba wewe endelelea hivyo hivyo na uropokaji,mara vua gwanda vaa magamba,mara vua gamba vaa uzalendo,almradi unaongea ongea kama mwenda wazimu, na utabaki hivyo hivyo mpaka 2015 ambap hutaamini utakachokishuhudia, hivi nakuuliza 29-7=22 Jibu lake ni sawa sawa na (kichwa chako+EPA+Richmond)-(Meremeta+Kagoda+Takrima)=SISIEMU, Inaelekea Bwana mdogo Nepi hujui hesabu sawa sawa..:boink: :violin::flock:
 
Nianze kwa kusema Nape amepewa nafasi kubwa katika chama cha CCM lakini hatambui hilo anaipeleka CCM shimoni, ukiwa na upeo mdogo kama wa Nape hustahili kupewa nafasi nyeti kama hiyo,

Nape alitakiwa kujua ushindi waliopata CCM katika chaguzi ndogo za madiwani ni kama kupoteza CHADEMA wamerejesha viti viwili na kuchukua zaidi vilivyokuwa vya CCM , hiyo haitoshi jumla ya kura walizopata CHADEMA katika chaguzi hizo ni nyingi sana tofauti na yeye anavyofikiria. ukiwa na kiongozi kama huyo kwenye chama ni janga

kuweni kama mwanakijiji ameappreciate kwamba chadema bado inabidi warudi kujiuliza kwanini wameshindwa kuliko kujipoza na kujipa matumaini ya uwongo.
Kama kupata majimbo 3 kati ya 29 mnajisifia kuwa mmeadvance mjue 2015 YOU ARE IN FOR SUPRISE.MARK MY WORDS.
 
Hivi wewe nape unaakili kweli kweli?????????
  1. Cdm imewanyang'anya ccm kata 3 na cuf imewanyang'anya ccm kata 1...........hapa nani ana hasara????????wewe ni katibu mwenezi unayepoteza kila siku, umepoteza Arumeru mashariki, umepoteza Igunga, umepoteza Sumbawanga na sasa umepoteza kata 4. Je unafaa kuendelea kuwa mwenezi?????????? Tena umepoteza majimbo na kata muhimu. Hivi unjua mgombea wako wa kata ya mtibwa ndiyo aliyepitwa kwa kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote yule kwa kata zote 29? je umejaribu kuangalia tofauti ya kura kati ya shishiem na cdm????????? je umeangalia mmeonga magodoro, pesa na ununuzi wa vitambulisho kwa sh ngapi????
  2. Mdomo ulimponza makamba sasa na wewe chezea cdm...............itaendelea kukulaulua.
 
docta slaa bado anatufaa sana, nape unajing'ata sababu unajua docta slaa anawachoma kinoma! pigeni kelele na tume yenu ya uchaguzi, tunawasubiri 2015 tukiwa na tume huru.. Mungu ibariki Tanzania.
 
Bandubandu humaliza gogo!
Nimeanza na usemi huo kwa maan kwamba yawezekana ccm ikawa ni gogo na mbanduaji ni cdm! Nape hajui hilo!

Hazijutii bali anashangilia huyo mzima kwl?

Sasa subiri 2015 kama hizo kata zitakuwa za ninyi m tena

pipooooooooooooooooooz!
 
Back
Top Bottom