Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM-Taifa,
Nape Nnauye amechoka. Amechoka kimwili,kiakili,kimaneno na kimatendo. Kila uchao na kila apitapo,Nape anasema yale yale na kwa namna ile ile. Sasa Nape ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana huko Dodoma. Nape ana ngekewa ya kupewa jukwaa na kuhutubia. Viongozi wa kitaifa waamuamini na kumpa nafasi.
Nape amechoka.Uchovu wake sasa u wazi kabisa. Anarudiarudia yale yale palepale na kwingineko.Yeye ni CHADEMA tuuuuuuuu...basi.Hana hoja za haja za kuwaambia wananchi na kuiuza vyema Ilani yetu ya CCM ya 2010-2015. Kuonesha Ilani ilivyotekelezwa kwa vitendo na vitengo kumemshinda Nape. Nape anang'ang'ania ugaidi,utapeli wa CHADEMA na mgogoro wa CHADEMA.
Nape habadili santuri. Hana jipya.Hapaswi kuendelea kupewa jukwaa na kuendelea kuwaboa na kuwakera wananchi. Apumzishwe. Kurudiarudia maneno na matendo ni uchovu wa dhahiri kwa
Nape Nnauye. Nafasi adhimu anayopewa Nape apewe mwingne chamani. Kama vijana tunao wengi tu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam