Nape: CHADEMA wajiandae kuingia msituni

Nape: CHADEMA wajiandae kuingia msituni

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,172
Reaction score
162,619
Akiongea leo mkoani Dodoma katika mkutano wa hadhara,katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,bwana Nape Nnauye , amekielezea kikundi cha Red Brigade kama kikundi cha kigaidi kinachoweza kuvunja amani ya nchi na kuwataka wananchi kuwa macho na vikundi vya aina hiyo.

CHANZO:ITV

My take;
Hivi kati ya Red Brigade na watuhumiwa wa Escrow,nani anahatarisha amani ya nchi hii?!

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amerusha kombora kwa Chama cha Demokrasia na Maendekeo (CHADEMA) akidai makundi ya vijana wa ulinzi vya chama hicho (Red Brigade) yameandaliwa kwa ajili ya kuingia msituni kwa shughuli za ugaidi. Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Mpwapwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, inayoendelea mkoani Dodoma.

"CHADEMA wanaandaa vijana kupitia Red Brigade ili kuingia msituni na kuchukua madaraka ya nchi kwa mabavu. Wanafanya hivyo kwa sabababu wanajua hawawezi kuchaguliwa kwa njia ya kura wakati wa uchaguzi mkuu," alisema Nape na kuongeza: "Hawa wanaopiga kelele huko mitaani eti Red Brigade wanaandaliwa kwa ajili ya kulinda kura, naomba niwaulize hizo kura wanazotaka kulinda nani atawapigia? Hata hizo kura za kuiba zitatoka wapi," alisema.

Nape alidai kwamba tayari CCM wamepata taarifa nyeti za mpango ovu unaoandaliwa na CHADEMA kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwamba kuna mpango wa kuwatumia vijana wa Red Brigade.

"Taarifa tulinazo ni kwamba Red Brigade ni vikosi vinavyoandaliwa kwa ajili ya vitendo vya ugaidi na shughuli nyingine za ovyo. Taarifa ni kwamba hili ni kundi la kigaidi, wataanzishaje kundi la usalama wakati tunavyo vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi yetu?" alihoji Nape.

Nape alikituhumu pia chama hicho kwa kujihusisha na vitendo vya kuvunja amani katika matukio mbalimbali nchini ikiwamo yale yaliyotokea kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga na maeneo mengine kama Morogoro na kusababisha kuuawa kwa kijana muuza magazeti.
 
Nimesikia ITV
Ila wale wao sio tatizo?
Anaongea imladi aongee
 
Na green guard ya ccm wann wale kama co hao wanaotuteka na kuua wakat wa uchaguz wasilete uwehu wa red briged kuwa ni kukundi cha kigaid je nahao mafisad
 
mbona jina halionekani hapa

attachment.php
 
WanaJF na Watanzania Wote,Salaam.

Naandika kujibu hofu,wivu,mashaka na upotoshaji pia wa makusudi unaofanywa baada ya Picha na habari kusambaa zinazoonyesha namna Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alivyoapisha Vikundi Vya Ulinzi na Usalama "Brigedia Nyekundu(Red Brigade)"vya CHADEMA katika kanda na mikoa mbalimbali
attachment.php


Vikundi hivi ambavyo vimepewa mafunzo ya hali ya juu sana kuliko wakati mwingine wowote na vyenye uwezo mkubwa na mbinu za kisasa kabisa vinatambulika kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ibara ya 7.6.4.(h) inayotangaza na kutambua uundwaji wa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chama ambayo Brigedia Nyekundu inatekeleza majukumu yake yaliyoanishwa ya Kulinda Mali,Viongozi na Maslahi ya Chama popote nchini.Pia katika Fasiri ya " B" ya kanuni za uendeshaji wa Chama

Katiba ya Zamani kabla ya toleo la Mwaka jana na Marekebisho yake ilisomeka katika ibara ya 7.7.5

Katiba hii imekaguliwa na kuthibitishwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kuwa ni katiba halali na ambayo ibara zake zote hazijakiuka sheria wala katiba ya nchi na katiba hii ipo kwa msajili miaka yote

Msajili amethibitisha kuwa matakwa ya katiba ya nchi ibara ya 20.2(C) yamezingatiwa kwamba hakuna chama cha siasa bila kuathiri kifungu cha 1 na 4 kitakachotumia nguvu kama sera yake ya kufikia dhima yake katika lengo la kuchukua madaraka.



Hofu,Wivu na kelele zinatokana na wapinzani wetu kuona kwamba Mwaka huu hawataweza kuufanya uharamia wao waliokuwa wakiufanya miaka yote hasa wizi wa kura,kutisha wanachama na wafuasi wetu na hata wananchi wakati wa kujiandikisha na kupiga kura

Zilishaibuliwa Propaganda humu na Naibu katibu mkuu wa CCM Mhe.Mwigulu na kupotosha kwamba Red Brigade ni Sawa na "Brigate Rosse" ya Italia ambacho ni kikundi cha kiuhalifu.Alifanya kazi yake kwa nafasi yake nasi tulifanya kazi yetu tukampa changamoto atuletee katiba ya "Brigate Rosse" hadi leo hatujui alikotokomea au pengine labda anaisaka

Pia wananchi waliopotoshwa na kuanza kutulaumu na kuonyesha mashaka wana haki ya kufanya hivyo kwa kuwa hawajaambiwa kuwa kikundi hiki kinatambulika kisheria.Kwa kuwa sasa watafahamu kuwa kikundi hiki kinatambulika kikatiba na kisheria hawatakua wanatutendea haki ikiwa wataendelea kutulaumu au kukubali kupotoshwa

Sasa na Mimi Natoa Changamoto kwa Chama tawala CCM kilichounda serikali inayopaswa kusimamia Utawala bora wa Sheria nchini kitueleze Vikosi vyake vya "GREEN GUARD" vinatambulika kwa mujibu wa katiba ipi maana sijaona kipengele chochote kwenye katiba ya CCM kinachokitambua kikundi hicho na hivyo ofisi ya Msajili haikitambui ,hakitambuliki kisheria.Ninayo katiba yao hapa,Sikioni.

Kikosi chao Kina hadhi na sifa zote za kuitwa kikosi cha kihuni,cha kihalifu na kinachotekeleza majukumu yake kwa mrengo wa itikadi za kigaidi maana vikundi vyote vya kigaidi kama Interahamwe,Boko Haramu, Banyamulenge n.k vilianza hivi.Havitambuliki popote kisheria

Jeshi la Polisi nchini limekaa kimya. Hivi tunalipeleka wapi taifa hili?

Kama ambavyo "Brigate Rosse" ilivyojiendesha kihuni ndivyo "Green Guard" wanavyojiendesha na tukio la karibuni ni kumteka Mhe.Rose Kamili Mbunge wa Chadema kule Kalenga kwenye uchaguzi mdogo

Utekaji nyara umeshamiri nchini huku kikundi hiki kisichotambulika kisheria kikiachwa tu

Mauaji ya Albino yameshamiri na inawezekana unyama huu unafanywa na vikosi vya kukodishwa .Ni nani anadhibiti(Regulate) utendaji wa Kikosi hiki cha Green Guard?

Jeshi la Polisi kama halitaki kufanya kazi yake au linapoendelea kufanya kazi kwa upendeleo tutajilinda na pia tutawalinda wananchi wanyonge wanaonyimwa haki zao za kiraia kwa sababu chama tawala na jeshi la polisi kuruhusu uharamia huu

Kwa kuwa CHADEMA tunalenga kuunda Serikali yenye nidhamu,Kikundi chetu cha Ulinzi kipo kisheria na tumeonyesha dhamira ya dhati kabisa katika kufuata sheria tunapojilinda na pia tumelipa kipaumbele suala la usalama wa chama chetu kama tunavyolipa kipaumbele suala la usalama wa nchi yetu kwa serikali ijayo.

Wafuasi wetu wamekua wakiuawa na hata viongozi wetu na wengine kujeruhiwa na hata kukoswa koswa hata mahali ambapo Polisi wanajifanya kuweka ulinzi kumbe ni geresha

Hatima ya usalama wetu ipo mikononi Mwetu.Tutajilinda,tuna haki ya kisheria na kikatiba.Tupo Imara kuliko wakati Mwingine wowote

Wasalaam !

Aluta Continua,Victory Ascerta

Ben Saanane
 
Ina maana usalama wa Taifa haujatambua hilo?

Ngoja JK aunde tume kama ile ya kuchunguza mauwaji ya albino
 
Akiongea leo mkoani Dodoma katika mkutano wa hadhara,katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,bwana Nape Nnauye , amekielezea kikundi cha Red Brigade kama kikundi cha kigaidi kinachoweza kuvunja amani ya nchi na kuwataka wananchi kuwa macho na vikundi vya aina hiyo.

CHANZO:ITV

My take;
Hivi kati ya Red Brigade na watuhumiwa wa Escrow,nani anahatarisha amani ya nchi hii?!
Na "Green Gurd" ni nani?
 
Maneno ya nepi ni hewa chafu inayotokea mlango wa nyuma kutokana na kujaza, pilipili,tomato sosi,ulanzi wali maharage kwenye ziara, Biere, Mahindi ya kuchoma kwenye lile tumbo kubwa utafikiri Kibanda cha kufugia Minyoo...!!!

BACK TANGANYIKA
 
Siasa za Tanzania ni usanii usanii tu...
 
saanane
Ukweli anaujua ila huyu mtu ni sawa na mfa maji haachi kutapatapa.

Naamini hata hii post aliisoma ila basi tu anajifanya haelewi
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahah.... Mkuu Ben Saanane naona umeamua kuwakumbusha....!!!!

Hivi kwanini hawataki kuleta kifungu cha Katiba yao kinachotambua uwepo wa Greengurd??

MwanaDiwani ufafanuzi please kaka.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
MEANDU
Nimezoom ili nione jina la Nape bado sijaliona.Yamkini alikuwa anatumia jina lingine katika familia
 
Last edited by a moderator:
Nape kadiri siku zinavyosonga anazidi kuharibika, ni afadhali ya jana kuliko alivyo leo, sijui kesho atakuwaje!
 
Mtumbo wake mkubwa Kama mtungi unampofusha fikra kima huyo wale waliokua wanapiga gwaride maji maji songea ni kina nani? greenguard ni kina nani? Akafie mbele na njaa yake.

ImageUploadedByJamiiForums1425582868.321748.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1425582898.802514.jpg
Hawa sijui ni kina nani. Hivi huko ccm hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima wakuweza kumwambia Nape aache kuropoka ropoka hovyo? Au wote wana akili sawa naye?
 
Back
Top Bottom