FFU wamezunguka Ikulu. Kuna tishio la kuvamia Ikulu?

Status
Not open for further replies.

muhosni

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,108
152
Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine. Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.
 
wanaogopa peoples power. wenye nchi wakiamua hizo silaha sio kitu.
 
Unajua sehemu yenye joto kubwa tayari na vitu vinavyoweza kuwaka moto, hata ukisugua chuma tu, cheche zinaweza kuwasha moto.

Haya mambo ya sensa na nini kama maisha yangekuwa mazuri kidogo tu watu wasingeshiriki sana kuyapinga, lakini sasa hivi huhitaji hata kuwahubiria sana watu wajiunge na maandamano ya kuipinga serikali, kwa sababu serikali yenyewe inaonekana haijali wananchi na haitumii akili.

Hivi serikali ingekubali hilo swali la dini kwenye sensa hawa waliodai wangefanya nini baada ya kuhesabiwa na kuambiwa waislamu wako asilimia fulani?
 
Bongo maandamano pekee ambayo watu hawaogopi ni yanayogusa imani na siyo siasa. Kwahiyo usiote kabisa cdm kuwa inaweza ika organize maandamano kisha eti wakaelekea wizara yoyote,hawana ubavu huo.
 
JK uliambiwa nchi haitatawalika ukawa unachekacheka sasa goma liko uwanjani hilo
 
Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine. Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.

Maskini hawa polisi!! Wanafanya kazi kwa matukio sana.Intelijensia zao hazifanyi kazi? au wamezi pause? Wanakimbia huku na huku na kule kama pepo akikemewa.... They are not informed.Wanakimbilia panapofuka moshi....
 
TAIFA LETU TULIPENDALO SAAANA LA TANZANIA HIVI SASA LIKO NJIANI KUANGAMIA SHAURI YA KUKOSA UONGOZI SIKIVU, ADILIFU NA WENYE HEKIMA

"Taifaa la Tanzania linaumwa tena linaugua ugonjwa wa hatari sana tangu uchaguzi wa Oktoba 2010, kufanyike juhudi za haraka kulitibu taifaa," alisikika miezi michahe akitoa hii kauli yenye hekima tele yule Mhe Mbuye wa Arusha alie likizoni Godless Lema.

Hata hivyo, ni wangapi ndani ya nchi hii walau waliweza kumuazima sikio na kutafakari ki-undani zaidi hii kauli???????????

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na maswahiba wake wanaoendelea kufilisi nchi hii kupitia Dowans, EPA na rundo la fedha za ki-shetani kwenye Benki Uswisi, wataendeleaa kuishi kwa matumaini ya ulinzi wa FFU mpaka lini?????????

Ama kweli Tanzania taifa langu linaangamia kwa kukosa uongozi wenye hekima na uadilifu.

Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine.

Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.
 
JK uliambiwa nchi haitatawalika ukawa unachekacheka sasa goma liko uwanjani hilo
Sio Nchi tuu, hata Chama Cha Mapinduzi chenyewe hakitawaliki. Tuliambiwa Gamba - limeshindikana, Tukaambiwa Wajipime Wenyewe - Imeshindikana. Makundi yamepamba moto, sumu wanatiliana na bunduki kuonyeshana. mwaka wa kufa CCM miti yote huteleza
 
Mkuu acha utani. Usogelee "kitu kizito" ukipige picha? Nilipita fasta nikawa na wasiwasi labda kuna uasi umetokea ikulu nisijepigwa na "kitu kizito"

wow! unaleta jeuri? hujui ni marufuku kupiga picha hapa? haatukupeleki mahakamani...yani hatukutuhumu. Tunakuua kwa 'kitu kizito' kwa kuwa umefanya kosa.

ha...ha...ha...
mtatuua sote kisha mjitawale njie wenyewe...na kale kauroho chenu...!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom