Nape: CHADEMA iwajibike matukio ya mauaji

Nape: CHADEMA iwajibike matukio ya mauaji

Haya Wadau, nadhani wengi wetu tumeiona hii news. Mie hoja yangu ni moja tu, hivi Kina Nelson Mandela, Govan Mbeki, Solomon Mahlangu na wapiganaji wengineo wa uhuru wa ANC wangewajibika kwa mauaji yaliyofanywa na Askari dhalimu wa SERIKALI ya kibaguzi ya makaburu leo hii tusingekuwa tunawataja kina Mandela kama mashujaa wa afrika. Hivyo kijana nape asifikirie kuwa viongozi wa CDM watawajibika kwa mauaji ya makusudi yanayofanywa na Policcm kwenye mikutano halali ya CDM. Tukifuatilia mikutano yote ya CDM ambayo haikuingiliwa na madhalimu hakuna hata aliyeguswa hata na punje ya mchanga(Mfano ni Lindi, Mtwara, Dar es salaam na kwingineko kwingi tu). Hivyo kama ni kuwajibika, Nape angewajibika yeye pamoja na Wizara yake ya mambo ya ndani.
 
huyu anachojua ni kujipaka mkorogo-carolite tuu!NAPE hao watu wameuliwa na polisi au chadema?polisi ipo chini ya ccm au?
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwajibika kutokana na kuwepo kwa matukio ya watu kupoteza maisha yanayosababishwa na maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wafuasi wake. Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
“Chadema wana kila sababu ya kuwajibika, kwa sababu matukio haya ya mauaji yamekuwa yakitokea kwenye operesheni za mikutano yao na matukio ya aina hii kutokea katika kazi za chama cha siasa ni aibu, hivyo viongozi wa kisiasa wanaokutwa na matukio hayo ni lazima wawajibike kwa umma, lakini matukio haya yamekuwa yakitokea bila wao kuwajibika,” alisema Nape na kuongeza:
“Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.”
Alisema CCM inaungana na wanaCCM na wananchi wote kulaani mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu.
“Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine,” alisema Nape.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema CCM imetoa mwito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa
kuchunguza kwa umakini na weledi mauaji ya Mwangosi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.
“Pamoja na mwito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba
uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo,” alisema Nape na kuongeza:
“Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na Chadema nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombovya ulinzi na usalama.”
Aliyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni la kuuawa kwa kada wa CCM mkoani Singida, kuuawa kwa Ali Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Mwangosi, kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine yalitokea wakati viongozi wa Chadema wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.
Nape alisema matukio hayo si mazuri kutokea kwenye shughuli za chama cha siasa kwa madai ni aibu kwa
wanachama wake na wananchi kwa ujumla na hivyo kupoteza sifa ya kuitwa chama chema cha siasa.(Source: Habari Leo 6th september 2012)

Hivi Nape hawezi pitisha siku bila kuwashwa na CHADEMA?
 
C................ Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mimi kila nikipanda daladala lazima nikute Konda na abiia wakikwaruza..na mara jingine hadi kutoana damu....anaishauri vipi?Niache panda basi?Au nami na husika na haya mambo ya mabasi?
 
Muimbaa taarabu maarufu. Hana jipya huyu zaidi ya kuropoka anavyoviwaza na uti wa mgongo badala ya ubongo.
 
Hivi huyu Nape na magamba wenzeka wanaishi dunia gani ambao hawakuona kilichowatokea akina Gaddafi na Mubarak? Waache waendelee kumtupia Mungu mawe wasijue hakawii kubadilisha kibao na wakaumbuka na kuteketea. Yaani mmewageuza watanzania vipofu na mataahira wasiojua kuwa wauaji ni nyinyi? Nape unatia kinyaa hata kama unalipwa kwa kujidhalilisha. Nasikia una Masters sijui ni ya nini kama huwezi kutumia hata common sense?
 
Nape Nape Nape Mnauye!!!! Rudi shule ukasome. I doubt kama ulifaulu na kujua kutumia elimu uliyoipata barabara!!! Hebu tupeni wasifu wake kielimu huyu jamaa!!!! Bora hata January Makamba pamoja na kufutiwa matokeo ya sekondari lakini anajitahidi kusahaulisha umma maana majuzi kazindua board ya Bumbuli Development ....!!!! sasa wewe Nape mpayukaji what is your legacy?
 
Kama hao policcm wanajiamini kwa wanachokifanya kwanini wasiwauwe viongozi wanuawa raia wasio na hatia.
 
Kwa kauli hii ya Nape naanza kuamini kauli za kuwa haya mauaji kwenye mikutano ya chadema yanapangwa na CCM, ili tu watupe lawama kwa chadema. Lakini wamechelewa sana mpango wao umestukiwa.
 
Hivi huyu Nape na magamba wenzeka wanaishi dunia gani ambao hawakuona kilichowatokea akina Gaddafi na Mubarak? Waache waendelee kumtupia Mungu mawe wasijue hakawii kubadilisha kibao na wakaumbuka na kuteketea. Yaani mmewageuza watanzania vipofu na mataahira wasiojua kuwa wauaji ni nyinyi? Nape unatia kinyaa hata kama unalipwa kwa kujidhalilisha. Nasikia una Masters sijui ni ya nini kama huwezi kutumia hata common sense?

masters ya kuimba taarabu kaipatia Mombasa.
 
Kama mimi ninge kuwa Kikwete ningekuwa nimeisha timulia mbali Hiki kituko, hii ni aibu kubwa kwa kwa chama cha magamba, Nape naongea toka moyoni mwangu, nasikia uchungu sana kila ukifungua mdomo wako kuongea, unatia aibu wewe lazima unatatizo wala hii siongei kwa ushabiki. sasa hamka, toa matongotongo ya njano kwenye macho yako. matamshi yako na umri haviendani, hachana kabisa na nafasi iliyo nayo ndani ya chama chako kilicho jichokea, kweli unatia aibu mpka familia yako kama unayo, nape nakuombea usiku na mchana, Mungu akupe maono uone ugolo unaokutoka kwenye ubongo wako, lakini kwa kuwa Mungu si athuman kuna siku atakusaidia "Amen."
 
Huyu bwana mdogo ni mpumbavu na hajui asemacho. Ila nguvu ya umma itamfundisha muda si mrefu.

Tatizo la watu wa CDM ni uhodari wa kutusi wengine wanapokuja na hoja wasizozipenda. Shame on u
 
HV Nape ni nani vile? hv si yule aliyesema wanajivua gamba au mwingine? kama ndiye mwambie kwanza atupe taarifa ya utekelezaji wa kujivua gamba, sawa?
 
Siyo watu wa chadema. Ila kama unamkubali huyu jamaa kweli na wewe jifikirie.
 
mimi nikimsikia mwanamke anamtajataja sana bwana wake huwa ninajua mume anamfikisha penyewe.
 
Wakuu huyu chonde tumsaamehe tu bure huyu kijana w Mzee Nauye, kamwe hajui atendalo.

Isitoshe, siku zote mtu ukishakua na mwili mkuuuubwa kuliko uwezo wa mifupa mwilini kuweza kubeba, hapo hapo hata akili nayo hufyonzwa kichwani n mtu kubaki mtupu kabisa bila hata injini ya kutegemeka kutoa suluhisho za kutumainika.

Afadhali siku za nyuma ambapo mshauri wake mkuu alikua ni Le Mutuz le Baharia (ambaye naye siku hizi haonekaniki tena akiungua jua nasi huku mitaani tena) walau alikua akifungua mdomo angalau alikua anaweza akakukuna akili kwa maneno mawili matatu kabla hajaanza kukushangaza tena kwa rundo la mi-kauli ya ajabu ajabu tu.
 
Hivi Nape ni lazima uonge kila wakati?unaweza kula Big G life ikasonga mbele....coz unavyozidi kuongea ndiyo kujichoresha madhaifu yenu pamoja na hao mnaowapa Maagizo.
 
Back
Top Bottom