Nape awapasha wana taaluma Mlimani City

Nape awapasha wana taaluma Mlimani City

- Nothing but 100%, Great Thinking ndio maana tunasema CCM haina njia ila kuwekeza kwa Viongozi wenye umri mdogo kama huyu maana ndio the future ya Chama!, Bravo Mheshimiwa Nape, umesikika mpaka JF kumkoma Nyani uwanja wa Damu, I mean Mpaka Waziri Mwandosya amekubali kuwa JF mpango mzima, saafi sana washitueni na wengine huko kwenye power kwamba elimu ya bure ya taifa ipo hapa! JF Kumkoma Nyanis!

William @..NYC,USA: Le BAHARIA!

[/QUO

Vuvuzela Nape ndio mtu makini? Sio kuwa na vijana wala, vibabu au vikongwe itakyoisaida CCM ila kuwa na utaifa na kulinda maslahi ya taifa. CCM haiwezi hiyo hata wangeletewa malaika watamwita shetani kisha kuendelea na matendo yao maovu kama kawa.
Wasomi si tatizo hata kidogo. Tatizo ni wanasiasa. Wanasiasa ndio wamepewa dhaman ya uongzozi wa nchi. Wao ndio watakao chagua wasomi wepi wawatumie. Wanajua aina ya wasomi wanaowatumia wakitaka kuibia nchi. Wanajua wasomi wanaotema udenda ukiwanang'iniza noti usoni. Wanawakwepa wasomi wazalendo wanaoweza kukataa upuuzi wao. Tatizo ni wanasiasa. Tatizo ni ccm na kuwa na vuvuzela kama Nape hakuwezi kulisaidia. Nape kashindwa kujivua ghamba anataka kuwalaumu wasomi. Hakuna aliye mbora ccm, awe kijana, awe mzee, awe yuko nje ya nchi au ndani ya tz, awe mtoto wa mkulima au mtoto wa tingatinga, awe bajaji au baiskeli wote wabovu. Tatizo ni wao wanasiasa tena wanasiasa wa CCM.
 
- Mkuu Political parties are made kushinda uchaguzi kwanza, na mengine baadaye until Tanzania we understand that, CCM itaendelea kushinda tu uchaguzi, Nape ni kiongozi wa CCM sio Serikali he stands for interest ya Chama kwanza!

William @...NYC,USA: lE mUTUZ!

Bilashaka hao wasomi wanasheria anaowazungumzia Nape ni kina Andrew Change na Jaji Werema. Bila kumsahau waziri wa mambo ya sheria na utawala bora ambaye najisikia vibaya hata kumtaja tu. Warden........
 
Si wasomi wanaharibu mikataba, tatizo ni wanasiasa wanaingilia.
 
Nape kafulia, hana jipya, asubiri adhabu ya kutokuwa na nidhamnu kwa "wenye CCM" yao!
 
Bilashaka hao wasomi wanasheria anaowazungumzia Nape ni kina Andrew Change na Jaji Werema. Bila kumsahau waziri wa mambo ya sheria na utawala bora ambaye najisikia vibaya hata kumtaja tu. Warden........
Mbona mamaako aliyekukataa alikuwepo pia nawe hujamtaja au coz babaako alikutupa jalalani???? Ndo maana akili iko hivyoooo
 
Tasnia ya sheria inatia aibu sana...nadhani hawa ndio wanaongoza kwa kuharibu hii nchi...wengi wao ni walafi na wapenda pesa zaidi hawana Uzalendo hata chembe...wachache sana wanafirkiria hii nchi...kwa kweli most of these people are Mercenaries...ni aibu sana..

Hivi Lowassa, Karamagi na Rostam ni wa taaluma gani vile?
 
Huyo dogo kwenye red=Mnyika ni kichwa kwelikweli. Si jioni hii alikuwa pia kwenye mjadala mwingine wa "Muungano na Tanzania Tunayoitaka" uliorushwa live na Star TV? Amejibu hoja kwa ustadi wa kutisha. Sijui CHADEMA inatoa wapi hawa watu?

Mie kaniboa baada ya kutoka kunywa kahawa IKULU
 
Watakuwa wana phd ya ufisadi.NI WANAFUNZI AMBAO WALIKUWA WANALIMUDU VIZURI SAANA SOMO LA UFISADI NA WALIFAULU VIZURI MNO.Ndiyo maana hata kuwatia hatiani ni vigumu zaidi ya kuwasafisha tu.
 
pamoja na kwamba huyu dogo ni vuvuzela wakati mwingine anasema ukweli.

Mimi nilishasema siku nyingi kwamba kama kuna kundi la wabongo ambalo linapaswa kulaaniwa na kuhukumiwa 'kupigwa mawe' hadi life ni the so called wasomi. Wasomi ndio wameshika nafasi za utawala na za kufanya maamuzi yanayohusu jamii - wasomi ndio marais, mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wanasheria, wakurugenzi, wakuu wa vitengo, wahasibu, wengine wengi wana ma-title (ya ukweli na feki) ya udkt, uprof, ueng. Uacct, nk.

Hawa hawa ndio ndio wameshiriki - kwa makusudi au kwa kutojua (ambalo nalo ni kosa kwa msomi) - kuimarisha utamaduni/mfumo wa kifisadi.

Ninakuunga mkono dogo vuvuzela wa magamba - only that you are making such a great point from the wrong side of the political landscape.:lol:
naunga mkono hoja hii
 
Mbona mamaako aliyekukataa alikuwepo pia nawe hujamtaja au coz babaako alikutupa jalalani???? Ndo maana akili iko hivyoooo
Haya basi ni warden Selina Kombani, sema lingine ujifurahishe.
 
Dogo vuvuzela wa CCM Nape Nnauye leo mchana kawatolea uvivu wanataaluma wa (Tanzania Profesionals Network) kwenye summit yao iliyofanyika Mlimani City wakati yeye na Mnyika wakitoa mada ya Uzalendo na Utaifa.

Nape amedai wataalamu ndio hu-draft mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, akatoa mifano ya Dowans jinsi wanasheria walivyishauri serikali.....

Akatoa mifano ya wataalamu walivyoshiriki utoroshaji wa wa wanyama hai kwa ndege!

Huyu vuvuzela amesahau mkataba wa richmond/dowans ulikataliwa na wataalam wa tanesco na wanasiasa ndio wakalazimisha kuusaini, angalia mikataba ya madini ni wanasiasa ndio wameifikisha hapo kutokana na tamaa zao, ukienda nchi kama botswana suala la madini liko chini ya kitengo cha kusimamia madini ambacho kina geologists, mining engineers hakuna mbunge wala mwanasiasa hata mmoja. Hapa kwetu tukitaka kuangalia mikataba utakuta wanasiasa na wanasheria ambao hawajui kitu chochote kuhusu madini ila wanaangalia nini cha kusema ili wapate sifa.
Namaliza kwa kusema wanasiasa ndio wameharibu nchi hii kwa kuwapokonya wataalam mamlaka yao na kujiingiza kwenye ufisadi
 
Tatizo la mfumo wa utawala wetu chini ya Katiba ya sasa - ni vigumu kutenganisha mwanasiasa na mtaalamu katika utendaji wa serikali. Profesa au Daktari aliebobea katika masula ya madini au uwanja wo wote ule akiishateuliwa na Mhe Rais wa chama cha Magamba, kwa mfano, kuwa Waziri, Katibu Mkuu, Mkurugenzi, Mkuu wa Idara, Mwanasheria Mkuu au Jaji, Gavana wa Benki Kuu, hata kuwa memba wa Bodi, basi anavua utaalamu wake na kuvaa gamba. Hapo ndipo tumekwamia. Unaposikia watu wanaoitakia nchi hii mema wakipigania kupata katiba ya wananchi badala ya katiba ya magamba usisite kuwaunga mkono.
 
Hivi yeye taaluma yake ni muandishi wa habari eeeh!!!! taaluma yake haihusiki katika madhambi ya mikataba mibovu?hakumbiki mafisadi waliyowanunua waandishi kufanya coverage ya mitambo ya Richmoduli na kutuaminisha Tz itaondokana nao shida ya umeme ambayo mpaka leo inatutesa
 
Hali ilivyo ni kwamba Msomi yeyote akiingia ccm hawezi kuujali tena usomi wake. Hebu fikiria wasomi kama Msekwa, Prof. Magembe, Mzee tingatinga (Malecela) n.k. wanavyoongea pumba!! Huko chama cha magamba kuna kitu kisichoeleweka ambacho wasomi wanalishwa na wanabaki wakifanya yaliyo nje ya usomi wao!!! Sijui kuna nini? Ndani ya ccm kuna wasomi wa kila aina - walioacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa - lakini ccm inaenda shangalabagala!!! Hata hivyo tuwaunge mkono wasomi vijana kama akina Mnyika, Kafulia, Januari Makamba n.k. wanaweza kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
 
Nape amedai wataalamu ndio hu-draft mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, akatoa mifano ya Dowans jinsi wanasheria walivyishauri serikali.....
Kama wataalamu wenyewe ndio kama yule niliyemuona kwenye mdahala wa star Tv jana 4/12/2011, tujue tumekwisha. Nilimuona huyo wa TLS akiacha maksudi kufafanua maneno ya msingi katika kifungu cha 102 cha katiba, ili atudanganye. Mnyika alivyomrudisha kwenye mstari hakuweza tena kuwa na makeke!
 
Aliyosema ni kweli kuwa siku hizi wasomi tunaowategemea kujenga nchi yetu ndiyo hao wanaibomoa. Hata hivyo hakuna excuse ya mwanasiasa (nikiamini kuwa nao ni wasomi) kusaini mikataba mibovu eti kwa sababu imekuwa drafted na wasomi. ETHICS za kazi pamoja na vyama vyao ya siasa ziko wapi?? Huyo JK aliyekataza Richmond isivunjwe naye si ni msomi/mwanasiasa? Au usomi wake ni wa kuchapia kiasi cha kutotambua kuwa kulikuwa na udanganyifu.
 
Dogo vuvuzela wa CCM Nape Nnauye leo mchana kawatolea uvivu wanataaluma wa (Tanzania Profesionals Network) kwenye summit yao iliyofanyika Mlimani City wakati yeye na Mnyika wakitoa mada ya Uzalendo na Utaifa.

Nape amedai wataalamu ndio hu-draft mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, akatoa mifano ya Dowans jinsi wanasheria walivyishauri serikali.....

Akatoa mifano ya wataalamu walivyoshiriki utoroshaji wa wa wanyama hai kwa ndege!

Hakuna Jipya hilo linafahamika na Wao kama chama tawala mbona hawajawachukulia hatua hao waliotufikisha hapa? au ndo cheap politics?Imekuwa desturi siku hizi wanasisasa wakipewa nafasi kuongea wanaongea mambo ambayo yanawafurahisha watu lakini swali la msingi walikuwa wapi kuyasema hayo?na wanamechukua hatua gani juu ya hayo wanayo yasema?
 
Back
Top Bottom