Nape awapasha wana taaluma Mlimani City | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape awapasha wana taaluma Mlimani City

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zamwamwa, Dec 4, 2011.

 1. z

  zamwamwa Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dogo vuvuzela wa CCM Nape Nnauye leo mchana kawatolea uvivu wanataaluma wa (Tanzania Profesionals Network) kwenye summit yao iliyofanyika Mlimani City wakati yeye na Mnyika wakitoa mada ya Uzalendo na Utaifa.

  Nape amedai wataalamu ndio hu-draft mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, akatoa mifano ya Dowans jinsi wanasheria walivyishauri serikali.....

  Akatoa mifano ya wataalamu walivyoshiriki utoroshaji wa wa wanyama hai kwa ndege!
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Dah hii Kali atutajie wakina nani hao tule nao sahani moja haiwezekani tukawa tunapiga kelele kumbe kuna watu wanoishauri serikali upumbavu. Najua watajitetea kuwa tuliwashauri hivi serikali wakabisha. Lakin twende nyuma twende mbele wanasheria ndo wanaoifanya nchi yetu iwe masikini.
   
 3. Polonium210

  Polonium210 Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Wana siasa hao hao wanaendelea kuwalea na Kuwalinda Wanataaluma hao
   
 4. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kwamba huyu dogo ni vuvuzela wakati mwingine anasema ukweli.

  Mimi nilishasema siku nyingi kwamba kama kuna kundi la wabongo ambalo linapaswa kulaaniwa na kuhukumiwa 'kupigwa mawe' hadi life ni the so called wasomi. Wasomi ndio wameshika nafasi za utawala na za kufanya maamuzi yanayohusu jamii - wasomi ndio marais, mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wanasheria, wakurugenzi, wakuu wa vitengo, wahasibu, wengine wengi wana ma-title (ya ukweli na feki) ya uDkt, uProf, uEng. uAcct, nk.

  Hawa hawa ndio ndio wameshiriki - kwa makusudi au kwa kutojua (ambalo nalo ni kosa kwa msomi) - kuimarisha utamaduni/mfumo wa kifisadi.

  Ninakuunga mkono dogo vuvuzela wa magamba - only that you are making such a great point from the wrong side of the political landscape.:lol:
   
 5. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Tasnia ya sheria inatia aibu sana...nadhani hawa ndio wanaongoza kwa kuharibu hii nchi...wengi wao ni walafi na wapenda pesa zaidi hawana Uzalendo hata chembe...wachache sana wanafirkiria hii nchi...kwa kweli most of these people are Mercenaries...ni aibu sana..
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bado yupo huyu kijana!
  Anasahau kuwa wanasiasa ndio wameharibu nchi hii, kwa kutoa mamuzi ambayo wataalamu wameyakataa
   
 7. z

  zamwamwa Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dogo wa CCM Nape Nnauye leo mchana kawatolea uvivu wanataaluma wa (Tanzania Profesionals Network) kwenye summit yao iliyofanyika Mlimani City wakati yeye na Mnyika wakitoa mada ya Uzalendo na Utaifa.

  Nape amedai wataalamu ndio hu draft mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, akatoa mifano ya Dowans jinsi wanasheria walivyishauri serikali..... Akatoa mifano ya wataalamu walivyoshiriki utoroshaji wa wa wanyama hai kwa ndege!
   
 8. B

  BMT JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooood nape
   
 9. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hana mpya huyo, ye kashaona kugezea kushonesha suti kama ya Mnyika ndio ujanja basi aishie hapo hapo. Yeye alivyo draft mchakato wa kujivua gamba alionaje? amefanikiwa?
   
 10. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,780
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Huyo dogo kwenye red ni kichwa kwelikweli. Si jioni hii alikuwa pia kwenye mjadala mwingine wa "Muungano na Tanzania Tunayoitaka" uliorushwa live na Star TV? Amejibu hoja kwa ustadi wa kutisha. Sijui CHADEMA inatoa wapi hawa watu?
   
 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Mnyika na wewe uliwezaje kukaa meza moja na huyu BOGUS Nape Meza moja. Uwe unaangalia watu wa kwenda nao kufanya summitt. Nape siyo Kiwango chako kabisa Mnyika. Juzi juzi tu umetoka kuaibika kutia saini na Emmanuel Nchimbi na leo tena upo Nape!
   
 12. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Hivi hata Richmond napo wanahusika? Hivi Wanasiasa sio ndio walijipa majukumu ya kujifanya ni Accounting officer, Tender board na PMU badala ya TANESCO kama PE, Mkurugenzi wa TANESCO kama AO na tender board,PMU za TANESCO. Kwenye Richmond TANESCO waliporwa majukumu yao kwa mujibu wa PPRA act,wanasiasa wakajipa majukumu.
  Wanasiasa ndio wanoharibu nchi hii, wenyewe wanajifaanya wanajua kila kitu. Sio ndio hawa Wanasiasa wanaopitisha sheria za ajabu kule mjengoni, sheria kama ununuzi wa vifaa vilivyotumika, wanasiasa kuwa sehemu ya mahakama nk.
   
 13. S

  Selungo JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAKUU!

  Nape asituletee giza hapa. Kwani hao anaosema wataalam si wameteuliwa na serikali ya akina NAPE? Sasa atakuwa amewapasha wataalam au ameipasha serikali ya chama chao cha ma-used? Si ni juzi tu kule mjengoni Dodoma kwa uwingi wao waliamua kusimamia sheria ya kununua MITUMBA? Nao walikuwa wataalam au wanachama wa CHAMA CHA MA-USED (CCM)? Apeleke kujichubua kwake na mikorogo yake huko Lumumba.
   
 14. z

  zamwamwa Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani nani kaiga za mwenzake Sokwe? Nikumbukavyo mie Nape kaanza mda mrefu na suti hizi hata kabla hajawa Dc, nadhani ungesema Mnyika kaiga... We angalia hata viatu vyaooo
   
 15. z

  zamwamwa Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasiwasi wangu wengine mkijibiwa tutakula ban... Hivi ulishaacha ule mkorogo wa mikononi? na ile cheni ya kiunoni je?

   
 16. S

  Selungo JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAKUU!

  Hivi kumbe NAPE ni DC? Duh! Hiyo wilaya i,eula wa chuya wakuu!!! Yaani DC, halafu siku zote yupo kiguu na njia kuzurura TZ kusikuwa na bado aitwe mkuu wa wilaya? Ama kweli Chama Cha Ma-used ni zaidi ya ukijuavyo.
   
 17. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnyika kiwango chako si cha watu kama nape;nchimbi na huyu uliyekuwa naye jioni hii sijui nani huyu katibu sorry khatibu. Uwe unawakwepa hawana iq ya kuargue na wewe. Real katika lile bunge unachukua nafasi ya wabunge 200 wa magamba kwenye hoja zenye logic .
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Nothing but 100%, Great Thinking ndio maana tunasema CCM haina njia ila kuwekeza kwa Viongozi wenye umri mdogo kama huyu maana ndio the future ya Chama!, Bravo Mheshimiwa Nape, umesikika mpaka JF kumkoma Nyani uwanja wa Damu, I mean Mpaka Waziri Mwandosya amekubali kuwa JF mpango mzima, saafi sana washitueni na wengine huko kwenye power kwamba elimu ya bure ya taifa ipo hapa! JF Kumkoma Nyanis!


  William @..NYC,USA: Le BAHARIA!

   
 19. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Nape sio DC, alikuwa DC huko nyuma kabla ya kuwa katibu Mwenezi wa CCM.
   
 20. U

  UNIQUE Senior Member

  #20
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa tu ukitaka usomi wako ukubalike na ccm andika wanavyotaka. Angalia maprofesa wa ccm kama magembe utafikiri mataahira
   
Loading...