Kushangaa Mwekezaji Mlimani City kuwekeza sh 150,000 hujui biashara zinazoanzishwa bila mtaji pesa?

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Wanaoshangaa Mwekezaji Mlimani City kuwekeza sh 150,000 hawajui kuwepo biashara zinazoanzishwa bila mtaji pesa?

Na:Mathias Byabato

"Hapo zamani katika kampuni moja ya huduma za Meli kulikuwa na mzee moja aliyekuwa fundi katika meli bila kusomea kazi hiyo katika vyuo vinavyotoa elimu hiyo.Mzee huyo alifanya kazi kwa miaka 50 akitumia tu uzoefu na uongozi wa Meli haukuona umuhimu wa kuajiri ‘wasomi’ kutoka vyuoni.Lakini kadri mabadiliko ya kielimu yalivyokuwa yakiendelea,uongozi ulilazimika kuajiri wataalamu watano waliobobea katika ufundi wa meli hivyo mzee yule alistaafishwa kwa maslai ya umma.Mzee alieekea kijiji kwao na kuanza maisha mapya.

Baada ya miaka minne tangu mzee huyo aache kazi meli ilipata itilafu katika injini yake na mafundi walijaribu kila mbinu kurekebisha lakini walishindwa,walitafuta mafundi wa kila aina lakini hawakufanikiwa na hatimaye uongozi wa meli uliamua kununua meli mpya lakini kabla ya kutekeleza azma hiyo mmoja wa wakurugenzi alikumbuka yule mzee na kuomba aitwe labda anaweza kurekebisha tatizo.

Yule mzee alipofuatwa aligoma na kudai kwa kazi hiyo wanayodai imewashinda wataalam waliopitia kila aina ya mafunzo yeye ataweza vipi?.Lakini akasema kwanza atafika atazame.Alipofika alikagua meli kwa dakika 30 kisha kulieleza jopo zima lililokuwa linafuatilia anachofanya mzee yule kwamba gharama ya kurekebisha tatizo ni milioni 20 kwa wakati huo.

Uongozi ulisema kama ataweza kulitatua watamlipa hizo fedha ambapo aliomba wasaini mkataba na walikubali kufanya hivyo huku wakitaka kujua kazi itachukua muda gani na vibarua watalipwa na nani.

Mzee aliwaeleza kuwa hiyo kazi wamuachie yeye.

Mzee alioomba nyundo ndogo na kumuaru kaptein apande usukani na afuate maelekezo yake.Mzee aligonga mahali katika injini mara tatu na kumuomba kapteini awashe na injini ikawaka.Wote waliokuwa pale wakashangilia huku mzee akibebwa juu juu kama mfalme.

Lakini Mmoja wa mafundi wakuu wa meli alimtaka mzee huyo atoe mchanganuo namna kazi aliyofanya ya kugonga sehemu kwa nyundo ndogo mara mbili na injini kuwaka inavyoweza kuthaminishwa na gharama ya milioni 20,alitakiwa atoe mchanganuo kwa maandishi.

Mzee aliandika hivi.

1:Kugonga sh 1,000

2:Kujua pa kugonga 19,999,000

Wote waliangua kicheko na kukubalina naye,alilipwa fedha yake yote na kuondoka zake."

Nimeanza na kisa hiki nikitaka kueleza kwa ufupi kwa nini nakubalina na hoja ya 150,000 inavyoweza kutumika kuanzisha biashara ya mabilioni ya fedha hivyo kuondoa mshangao uliotokana na yaliyoibuliwa na Kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwenye ukaguzi mradi wa Mlimani city ilibobaibaini

Mwekezaji aliyepewa dhamana ya kuwekeza huku akiwa na na mtaji (FEDHA) wa dola 75 tu sawa na shilingi za kitanzania laki moja na nusu.

Sitajadili sana suala hilo maana liko katika vyombo vya serikali na Bunge likichakatwa lakini nataka kudadavua namna ilivyo rahisi matumizi ya mtaji wa 150,000 kuchukua eneo lote la Mlimani city fedha ambayo mdau mmoja amedai kuwa haitoshi hata kununua Tecno wereva.

Je inawezekana?. Kwa maoni yangu suala hilo linawezekana sana tena fedha hiyo ni nyingi sana katika suala la mtaji fedha kiasi gani unahitaji kuanzisha biashara au fursa Fulani.

Ebu rejea chapisho la mtaalamu wa biashara Dr Bassanga(2011)

MTAJI NINI?, Mtaji ni kitu au rasilimali ambayo mtu anaweza kuitumia ili kuanzisha biashara,rasilimali hii ndio ambayo itamfanya mtu yeyote aweze kuanzisha biashara na kuifanya biashara yake ikuwe, hautaweza kuanzisha biashara kama hautakuwa na mtaji.

Kuna aina mbalimbali za mitaji na unaweza kutumia zote au mojawapo ya hizo kuanzisha biashara au fursa yotote.nitaongelea chache ikiemo wazo,jitihada,pesa.

Tuanze na wazo: Nataka tutazame namna wazo linvyoweza kutumika kuanzisha biashara kubwa bila kuwa na mtaji fedha au fedha ikatumika kama ya mwekezaji wa Mlimani City kuanzisha mradi wa mabilioni ya fedha.

Hapa nitatumia mifano ya madalali,wapiga debe,wapambe wa viongozi nk.



ITAENDELEA…………………………
 
mmekuwa watetez wa mabepari, naomba usizunguke sana, eleza namna gani laki na nusu ukawa mtaji wa kuwekeza mliman city. ukihusisha thaman ya eneo na asset mbalimbali zilizokuwepo. bila kusahau mikataba waliyosain. kama hujui hayo, kaa kimya usilete ujuaji na mifano yako ya madalali.
 
Wanatufedhehesha wanaoshangaa; wakaulize NBC mwekezaji alileta mtaji kiasi gani. Hata Nyerere aliuliza...
Ni kosa hilo hilo limejirudia katika uwekezaji wa Mlimani City. Walipewa kila kitu bure kuanzia benki yenyewe na majumba ya benki pamoja na madeni ambao benki ilikuwa ikiwadai Wateja wake. Majengo si asset kwa mabenki, hivyo yakauzwa na wao wakapanga. Madeni yakakusanywa kwa kasi ya ajabu. Fedha iliyopatikana ndo iliyotumika kununua benki yetu pendwa ya National Bank of Commerce. Wakabakiwa na faida kubwa tu kiasi cha kwamba ilikuwa wameuziwa hiyo benki bure.
Tumestukia mchezo mchafu uliofanyika kwenye kampuni yetu ya simu. Mambo yalikuwa hayo hayo. Tumejimaliza sisi wenyewe hakuna sababu ya kutafuta mchawi nje ya nchi.
 
mmekuwa watetez wa mabepari, naomba usizunguke sana, eleza namna gani laki na nusu ukawa mtaji wa kuwekeza mliman city. ukihusisha thaman ya eneo na asset mbalimbali zilizokuwepo. bila kusahau mikataba waliyosain. kama hujui hayo, kaa kimya usilete ujuaji na mifano yako ya madalali.

Likini nyinyi na ccm yenu imesaidia mabepari kutuibia na kutufanya sisi tuwe masikini
 
Likini nyinyi na ccm yenu imesaidia mabepari kutuibia na kutufanya sisi tuwe masikini

Mambo mengine ni ya ajabu. Hapo mtetea mabepari sijui ni aliyefanya kwa vitendo kuwapa bure au anayezungumza
 
mmekuwa watetez wa mabepari, naomba usizunguke sana, eleza namna gani laki na nusu ukawa mtaji wa kuwekeza mliman city. ukihusisha thaman ya eneo na asset mbalimbali zilizokuwepo. bila kusahau mikataba waliyosain. kama hujui hayo, kaa kimya usilete ujuaji na mifano yako ya madalali.

Soma tena na tena utaelewa mantiki. tunachosema na maoni yako ni vitu 2 tofauti
 
Back
Top Bottom