Nape Atunukiwa Shahada Ya Pili Ya Utawala Mzumbe

Nipe tano

Senior Member
Jun 16, 2011
100
27
Nape Atunukiwa Shahada Ya Pili Ya Utawala Mzumbe
Submitted by Mjengwa on 16.12.11

Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipongezwa na mama yake, Kezia Alfred, baada ya kutunukiwa shahada ya pili ya uongozi katika mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, leo.
 
Mzumbe hii hii inayopigiwa kelele?

Ahongereke!
Kelele za vipi Mkuu? Tuhabarishe basi. Hata mimi nilikuwa nashangaa kwa mchakamchaka huu wa UDC, Katibu Mwenezi wa CCM, Kuvuana magamba n.k. alipata wapi muda wa kusoma, kufanya utafiti na kuwasilisha mada? Kelele za vipi? Tuhabarishe basi.
 
Kwani ni viongozi wa chama kilichoko madarakani tu ndo wanatakiwa kutunukiwa? Maana kila kukicha nasikia magamba tu ndo wametunukiwa
 
Kelele za vipi Mkuu? Tuhabarishe basi. Hata mimi nilikuwa nashangaa kwa mchakamchaka huu wa UDC, Katibu Mwenezi wa CCM, Kuvuana magamba n.k. alipata wapi muda wa kusoma, kufanya utafiti na kuwasilisha mada? Kelele za vipi? Tuhabarishe basi.
siku ina masaa 24,Hongera sana Nape
 
Huu ni ujumbe tosha kwa Mbunge Lema.
Yafaa aige wanavyofanya wanasiasa wenzake na yeye angalau aboreshe hako ka Form Two kake.
 
Huu ni ujumbe tosha kwa Mbunge Lema.
Yafaa aige wanavyofanya wanasiasa wenzake na yeye angalau aboreshe hako ka Form Two kake.

Acha kuupotosha umma, Mh.Lema (Mb) ana diploma ya ualimu kasomea butimba
 
Hongera Nape, mungu awe nawe. Elimu ni jambo la msingi sana.
 
kwa mzumbe siilikuwa wiki kama mbili hivi zilizopita ni mzumbe ipi hasa unaongelea..
 
Huu ni ujumbe tosha kwa Mbunge Lema.
Yafaa aige wanavyofanya wanasiasa wenzake na yeye angalau aboreshe hako ka Form Two kake.

Kikubwa kuchapa kazi na si uchakachuaji kwa kutumia videgree wanavyopewa magamba.
 
Hata kama angepata Shahada ya Uzamivu ya Mbinguni na akakabidhiwa na Jibril kwa niaba ya Mola la msingi ni OUTPUT yenye MANUFAA KWA TAIFA.

Kama atasimama pamoja na umma kwa maslahi ya taifa HONGERA ZAKE tena HONGERA SANA! Ila kama atakula na kuchovya tonge pamoja na mafisadi kwa hasara ya taifa letu basi shahada hizo ni upupu tena ni zaidi ya kelele za vuvuzela livumalo bila manufa yoyote.

Tunasubiri kuona atasimama upande gani tena kwa matendo thabiti na si kwa maneno matupu.
 
Huu ni ujumbe tosha kwa Mbunge Lema.
Yafaa aige wanavyofanya wanasiasa wenzake na yeye angalau aboreshe hako ka Form Two kake.

nani kakuambia kuwa elimu mpaka uwe na degree? Tofautisha elimu na kusoma. Kwa hiyo Nape kasoma lakini hana elimu.
 
nani kakuambia kuwa elimu mpaka uwe na degree? Tofautisha elimu na kusoma. Kwa hiyo Nape kasoma lakini hana elimu.

Sina uhakika na unalosema. Ila nijuavyo mimi kuna tofauti kati ya aliyesoma na asiyesoma. Kwa mfano, kama Lema angekuwa ameenda shule, asingekuwa anafanya baadhi ya mambo ya kitoto anayofanya sasa kama ya kujipeleka gerezani ili apate mtaji wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom