Nape atoa angalizo hali ya Uchumi; awaponda CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape atoa angalizo hali ya Uchumi; awaponda CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Jun 14, 2012.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Na Nape Moses Nnauye

  Nilikuwa nikisikiliza Bunge na kusikia hotuba juu ya hali ya uchumi hapa nchini na nikajiuliza hivi hawa "watani" wetu wanaopita kuchangisha watu nchi nzima na kunadi kuwa hali yetu ya kiuchumi ni "mbaya sana" na wengine wakaandika makala kwenye magazeti kuwa serikali haina hata uwezo wa kuagiza mahitaji ya mwezi nje ya nchi na HAZINA imekauka..,nilijiuliza kuwa hayo wameyatoa wapi..? ni uvivu wa kufuatilia na kusoma ripoti za serikali juu ya hali ya uchumi au ni dhamira ya kukusudia kupotosha na kudanganya umma wa watanzania..,

  Nimekuwa nikisoma na kufuatilia ripoti na taarifa mbalimbali za uchumi za nchi mbalimbali duniani na kufarijika baada ya kugundua kuwa hali yetu ya kiuchumi inaelekea vizuri kuliko nchi nyingi hata zile zinazotajwa kuwa zilizoendelea za kule Ulaya na Asia.

  Mathalani kwa India, takwimu za uchumi zinaonyesha kuwa GDP imeendelea kushuka kwa 5% tangu mwaka 2010.,according to economic watch.,Ugiriki wamekuwa wakitapatapa kujinasua kwenye madeni makubwa waliyonayo,lakini pia wanayo hatari kubwa katika kupungukiwa nishati ya umeme ambayo ni msingi katika shughuli za uzalishaji nchini humo hata serikali kulazimika kutumia dola milioni 50 za dharura kutoka hazina yao kukabiliana na hatari hiyo. Na hii ni nchi yenye watu wasiozidi milioni 11.5.

  Pia, Benki ya dunia imeonesha wasiwasi wake juu ya hali ya ulaya kwa sasa na athari zitazopatikana katika uchumi wa dunia, hata kufikia Benki ya Dunia kushauri nchi za ulaya kuelekeza nguvu zaidi katika mipango na miradi yao ya muda mfupi na muda wa wastani na kuacha kufikiri na kupanga mipango ya kimaendeleo ya muda mrefu.

  Nadhani watanzania sasa tunapaswa kuelekeza masikio yetu na macho yetu Dodoma ili kupata uhalisia wa hali yetu kiuchumi na namna tunavyoendelea kuimarika kiuchumi.

  Nimefurahishwa na majibu ya waziri wa Nishati na Madini Mhe, Sospeter Muhongo pale aliposema kuwa sasa wanatekeleza mipango ambayo si tu itahakikisha Nishati ya umeme inapatikana Tanzania bali wana-projections kugeuza Tanzania kuwa ni wazalishaji-wauzaji wa Nishati hiyo, na hivyo wamelazimika kuanza kuchimba madini ya Uranium kabla ya Kenya.

  Tuendelee kusikiliza Bunge letu litakaloendelea tena saa kumi Jioni...
   
 2. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ahsante kwa kutufariji kaka, tuna macho, masikio, akili na utashi.
   
 3. m

  mabhuimerafulu Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mmmh! Kweli Nape ana roho ngumu. Ni mtu wa kuogopa kama ukoma. Hivi hata serikali hii ina watetezi? Kweli Nape jasiri!
   
 4. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Rubish Nape! Nothing new!!

  Zile zile ahadi za JK za maisha bora kwa kila mwananchi!!

  Wanataka wananchi waishi kwa matumaini ambayo hayapo, kama wagonjwa wa UKIMWI wanaotumaini kuwa iko siku dawa itapatikana ili wapone!! Siku zinakwenda wagonjwa wanazidi kuteketea.

  Na CCM inataka waTZ waendelee kuishi kwa matumaini huku wanakufa kwa njaa, magonjwa, kukosa elimu bora, n.k.

  Samahani kwa kutoa mfano wa UKIMWI hapo juu, LAKINI AFADHALI UKIMWI KULIKO CCM!!!!

  Kwa nini afadhali UKIMWI kuliko CCM?

  Kwa sababu:
  1. CCM inaangamiza watu wote (except very few) wkt UKIMWI unaangamiza watu wa namna fulani
  2. Uangamizaji wa UKIMWI unaweza kuepukika wkt uangamizaji wa CCM haukwepeki
  3. CCM inaangamiza wanyama wetu wkt UKIMWI haugusi wanyama
  4. CCM inaangamiza raslimali zetu (madini) wkt UKIMWI haufanyi hivyo
  5. E.t.c (tafadhali endelezeni)
   
 5. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  So what??

  Hivi pamoja na matatizo ya hizo nchi alizotaja bado tunaweza jilinganisha nao kiuchumi?? Au the boy is feed with media manipulation na uongo wa Wassira na Serikali ya Magamba??

  Leo hii experts in Economics say the 2012/13 budget could worsen the national debt yeye anaimba taarab za TOT!

  Hata anashindwa kufatilia ukweli kuwa pamoja na bajeti ya mwaka uloisha kuwa kubwa kuliko ya mwaka mwingine nyuma bado fedha hazikufika katika halmashauri zetu!

  Ujinga mwingine wa kushabikia mambo bila kufanya tafiti ni laana!

  Aje hapa atuambie kwanini pverty imekuwa ni rural phenomenal??

  Mijitu inayoshabikia ujinga inakera sana watu tunalipa kodi halafu kodi haieleweki inafanya nini mjinga mmoja ankejeli watu kama mtangazaji wa TBC Masome anyefurahia ABG kuongeza asilimia moja kwenye mrahaba na ansifu kama ni mafanikio makubwa...

  Nape ajifunze kusoma kama wenzake akiendelea na propaganda na kuota kitambi atajifedhehesha yeye na chama chake!
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Nape mbona kama umechanganyikiwa? Yan bila kuitaja cdm huwezi kuongea?

  Najua sasa hivi utaanza kuagiza na kufanya kazi za waziri wa nishati na madini.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nape, jitahidi uwe unaongea/unaandika mambo unayoyafahamu, vinginevyo utajikuta unaanika udhaifu wake hadharani.

  GDP ya Tanzania ni USD 23 billion
  GDP ya India aprox. USD 1.8 trillion

  India hawategeme wafadhili kuendesha nchi. Serikali ya CCM inategemea wafadhili sio tu kujenga barabara bali hata kulipa mishahara ya wafanyakazi! Kama hazina ilikuwa imenona unaweza kutumbia ni kwanini wizara zooooote hazikupata hela zilizopitishwa na bunge FY 2011/12 ? Kuna wizara zimepata only 30% ya budget iliyopitishwa!

  Mirado ya ujenzi wa barabara imekwamba, je hazina haijakauka?
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu:
  1. CCM inaangamiza watu wote (except very few) wkt UKIMWI unaangamiza watu wa namna fulani
  2. Uangamizaji wa UKIMWI unaweza kuepukika wkt uangamizaji wa CCM haukwepeki
  3. CCM inaangamiza wanyama wetu wkt UKIMWI haugusi wanyama
  4. CCM inaangamiza raslimali zetu (madini) wkt UKIMWI haufanyi hivyo
  5. CCM inaangamiza Tanganyika
  6. CCM inaangamiza elimu (Ukimwi chuo kikuu)
  7. CCM inaangamiza maadili (Professor wa rushwa)
  Edgelea
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  [h=1]The World's Most Expensive Places to Live 2012[/h]Europe's debt crisis, slowing growth in the U.S. and worries about a hard landing in China: Even if you've kept your job this past year, you've probably had plenty to worry about. But how about the rising cost of living?

  According to a new report from human resources firm Mercer Consulting, the cost of living in North American, Asian and African cities has been rising this past year, despite the global slowdown.

  The study looked at 214 cities worldwide and used New York City as the benchmark. Mercer's annual cost of living survey is used by multinational companies to determine compensation for their expatriate employees around the world. The rankings are based on the cost of more than 200 items in each location including housing, transportation, food, clothing and entertainment.

  The World's Most Expensive Places to Live 2012 - Yahoo! Finance

  Nape: Hata Tanzania gharama za maisha zinapanda badala ya kushuka. Hii sababu yako ni ya ovyo sana na hasa ukiangalia kuwa nchi karibu zote zilizotuzunguka, zinakwenda mbele kwa speed kubwa sana ukianzia Kenya, Rwanda, Congo, Mozambique, nk nk.

  Msitafute sababu za kuonyesha kwa nini hatuendi mbele wakati kila siku, tunasikia madudu mnayofanya. Nchi zote ambazo uchumi wake unategemea VIWANDA na Mabenki, ndiyo hao wanalia sasa hivi. Africa imekuwa ikitegemea sana madini na kilimo. Hali ya chakula kwa sasa duniani ni mbaya sana na kama tungelikuwa tukizalisha kwa wingi, chakula peke yake (Mazao na mifugo) ingelitosha kututoa kwenye umasikini.

  Nape na wenzio, Watanzania siyo mabwege tena (by Dr. H. Mwakyembe, PhD).
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mwehu huyo achaneni naye,2015 ataokota makopo.
   
 11. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Kwanini na rasilimali zote hizi bado tujilinganishe na greece na nchi zenye matatizo duaniani. Kwa nini tusijilinganishe na nchi kama Ujerumani au Brazil? Kama ni swa kujilinganisha na nchi zenye matatizo ya uchumu ..basi tusiishie hapo, tufanye hadi yale serikali zao na viongozi waliyofanya....KUJIUZURU ..kama serikali ya Greece, Italy chini ya Berlusconi etc....
   
 12. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nina wasiwasi na elimu yake, lazima vyeti vyake vitakuwa vina maksi za kudesa na huruma za malecturer.

  katika maisha haya vijana wasomi wakitanzania wanavyoishi bila kujua kesho itakuwaje mtu anaweza kufunguka kipuuzi namna hii!!!!!!!! Thanks God he is not my leader
   
 13. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Prof Muhongo ni mwalimu wangu pale Mlimani tangia zamani wattu/wanafunzi walikuwa wanamjua ni mtu wa state hivyo kupiga siasa sio ajabu kwani anaendeleza utamaduni wa ccm wa kutoa ahadi juu ya ahadi....

  Mathalani kuchimba madini ya uranium sio leseni ya kumiliki kinu cha kuzalishia umeme...Kuchimba ni suala jingine na kuzalisha umeme kwa nuklia ni issue nyingine kabisa. Nape ngoja nikufundishe kidogo, ili kupata eneo la kujengea mitambo ya nyuklia inachukuwa miaka 10 hadi 15. Eneo linatakiwa kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa kipindi hicho ilikujua "Geotechnical stability of an area", Tectonic activity in an area etc...majibu ni miaka hiyo.

  Je tutakuwa tunatumia nini katika kipindi hicho??? Alichosema Prof Muhongo ni sahihi kitaalamu lakini kwa matiki ya kisiasa tu....TZ hatutaweza kuzalisha umeme wa nyuklia hata baada ya miaka 30 ijayo. Irani walianza kujengewa mitambo mwaka 1974 je wanazalisha?????
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Bado mnaletaga porojo za hilo vuvuzela tu? Angoje Budget mbadala ya upinzani huenda akajifunza kitu
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama Nape anayasema haya seriously, ni mtu anayestahili kupewa pole
   
 16. N

  Njaare JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni nini viashirio vya kukua kwa uchumi ambavyo mimi mwananchi wa kawaida naweza kuviona na kukiri kuwa uchumi umekua? Nape anataka tuamini kuwa tunaishi maisha mazuri kwa kuambiwa kuwa unaishi maisha mazuri. Uchumi mzuri wakati shule hazina walimu, wakulima wa korosho hawalipwi, hospitali hazina dawa.

  Anataka kutulazimisha tuamini kuwa mgomo wa madaktari ni viashiria vya uchumi mzuri!!!!! Hahahaaaa!!! Hizi sii zama za kudanganywa tena kuwa fikra za viongozi ni sahihi!!!!! Ha ha hahhhhaaaaaaaaa
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama Greece au any European Countries wangekuwa na rasilimali zilizopo Tanzania wasingekuwa na shida hata kidogo. Nape anashindwa kujua excatly nini kinachoongelewa kwenye mambo ya uchumi. Tuna bidhaa ambazo wakati wa mtikisiko ndipo huwa na thamani zaidi - Gold. Na angekuwa mdadisi angegudua kuwa Australia wako vizuri licha ya mtikisiko wa uchumi duniani kwa sababu moja kubwa - madini. Sisi tuna deposit kubwa sana, sasa kwa nini tunaogolea kwenye dimbwi la ufukara?
   
 18. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kipimo halisi cha hali ya uchumi popote ni hali za wananchi wenyewe kumudu bei za mahaitaji muhimu. Hivi sasa hapa nchini hakuna kabisa mzunguko wa pesa hata wauza maandazi wanahisi ukosefu wa fedha uliopo unaosababishwa na kukosekana kwa uzalishaji hapa nchini. na haya yote ni matokeo ya sera na mipango mibovu na iliyopitwa na wakati ya Serikali ya CCM na ufisadi uliokithiri wa viongozi wa CCM na watendaji wa serikali yake.

  Haishangazi Nape kudai kuwa hali ya uchumi ni nzuri sana kwa sababu wakati wote yuko katika VX akivuta posho hata kwa kikao cha kutoka ofisi moja kwenda ingine hapo makao makuu ya CCM.

  Ukweli ni kuwa Tanzania na watanzania hajawahi kuwa katika hali ngumu kiuchumi kama kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/12 ambapo wewe Nape Nnauye ndio ulikuwa msimamizi mkuu wa Serikali ya CCM. Wengi wamedai kuwa ugumu wa kipindi hiki unazidi hata ugumu ulioikabli Tanzania wakati na baada ya vita vya Kagera 1979/80
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nape kamegewa hako katonge na mwigulu nchemba aka mchumi!!!!! kaongopewa naye anatuongopea,
   
 20. U

  Uparo Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Nape uwe unafikirisha kichwa chako vizuri na kuchekecha mambo huwezi kusema uchumi wetu ni stable ukilinganisha na india kwa tofauti ya pato letu kuwa kubwa, ni sawa tunapato kubwa ila umejiuliza au kufananisha uwiano wa mfumuko wa bei katika nchi zote mbili?

  Pia ni uongo mtupu kusema uchumi unakuwa wakati kuna inflation kubwa nchini.kajipange upya na uchunguze vizuri uhalisia wa uchumi wa nchi na pia uwe unafanya uchambuzi halisia wa uchumi wa nchi yako na kufananisha na uwiano wa maendeleo uliopo
   
Loading...