Nape atimiza umafia Mwanza

leo ccm imetia huruma mwanza,manake wahudhuriaji wa kukodiwa ndio waliujaza uwanja,na kulipwa mlo wa mchana...,duh kumbe njaa nayo ni mtaji
 
Magwanda inaonesha mlikuwa mnafatilia kwa makini sana besidei ya CCM Mwanza. Kweli nimeamini CCM ndio namba wani. Kila details za besidei leo tunaipata kutoka kwa magwanda, raha sana. Kumbe walisilimishwa 1,800? na bado.

Sasa tunashauri kitengo cha propaganda kifanye besdei kila wiki na si kila mwaka.

CCM juu, juu, juu zaidi

Toba!!! Maulana, Wamesilimishwa?? wamekuwa suni? Boko Haram? au Al Shaabab?
 
...katika maadhimisho ya miaka 35 ya ccm huko mwanza Nape amesema wanachama 1847 wamejiunga na ccm baada ya kukimbia kwa baba yao wa kambo...Nape hajasema baba yao huyo wa kambo ni nani ila mipango yao ya kutengeneza kadi feki kibao za chadema na kugawa kwa hawa watu ili wadai kuzirudisha ilishajulikana...alichokifanya nape ni kutimiza umafia wa kuhadaa wananchi na kukihujumu chadema...kweli ccm ni chama pinzani mwanza leo nimejiridhisha..


Kwa mtu aliye makini ambaye anaijua mwanza vizuri, CHADEMA haiitaji wanachama kushinda, inahitaji wananchi wa Mwanza.
 
CCM ni chama kina wanachama wengi na bado kinapendwa, hawawezi kuwa na udanganyifu wa ku print kadi za CHADEMA ili ionekane watu wamezirejesha na kujiunga na CCM.
 
ccm leo imefunika vibaya mwanza, ni ndremo na vifijo huku mtaani

Imefunika kwa kubeba watu kwa malori, mabasi na bodaboda kutoka viunga vya mji wa Mwanza na mikoa jirani na kutoa hongo ya shilingi elfu kumi kumi.

Hii aibu mtaishi nayo mpaka lini?
 
kumbe mnajindaa kulipiza kisasi na kumwaga damu mkishika dola.


Mazingira ya kisasi hayapo kabisa CHADEMA, ingekuwa hivyo nchi ingechafuka 2010 maana kwa muungwana kushinda kwa wingu la kura kuibia sio sahihi, pili Mwanza serikali ni ya CHADEMA lakini kwa uungwana walionao CHADEMA, ndo maana CCM wakaomba wafanyie birthday yao Mwanza, utalipizana kisasi na wehu wa fikira kwa namna gani? hawa ni wa kusamehe tu, hawajui walitendalo. Laiti wangejua nchi tajiri kutoka kwa mungu leo hii iwe yenye watu masikini haiwezekani, wangekaa kando waone japo wengine watafanya nini tofauti na wao, sasa ukikuta mtu anafikira mgando kama alivyowaonya Mkama, anadhani ni ujanja kung'ang'ania ufunguo/usukani hata kama Kufuli/barabara imemshinda, eti hoja yake ni bora tulale nje au tukose wote.
 
CCM ni chama kina wanachama wengi na bado kinapendwa, hawawezi kuwa na udanganyifu wa ku print kadi za CHADEMA ili ionekane watu wamezirejesha na kujiunga na CCM.

Unaweza ukasema lolote kwa nchi, lakini hakika nakwambia CCM mwanza, imebaki viongozi na watoto wao, wadoea pilau na watu wa namna hiyo. Mwanza ni mali ya CHADEMA sio kupitia wananchama wake, bali wananchi wa MWANZA. uliza dialo alipigwa vipi? Masha alipigwa vipi? ndo ujue wananchi wa Mwanza ndo wameipa CHADEMA umiliki wa MWANZA, WAKIWEMO WANACCM WAKUBWA.
 
Kwa hoja hii woooooote mmbebweka kuna chama kinakuja kitakachobeba utawala 2015 kama muujiza. achananeni na C C oooohh CCJ,CCM,CUF.CDM na wengine wengi wasotambulika hata kwa 5% ya watanzania lakini wanajidai wamo kwa kelele na ripoti za watafiti feki wa mezani na majibui ya D A I M!! Mmm vipi? Tafiti za kweli zisiszojali Posho na Mirage zimefanyika !!???! Mi ni Mpumbavu Kweli ila si MJINGA!

Sasa hiki nacho ni nini?mara oooh CCJ,CCM,CUF,CDM, mbona hueleweki ulitaka kumaanisha nini?
 
Huwezi kusababisa matatizo harafu ukavunga kujua namna ya kuyatatua bila msaada kutoka kwa mkosoaji wako, matatizo ya TZ chanzo ni CCM na Serikali zake, Sasa leo eti wamachinga waorodheshe shida zao Kikwete atasaidia??? Kama Rais ina maana hajui matatizo ya wamachinga hadi aorodheshewe??? ni usanii mmachinga kaliwa kwa mara ya nyingine tena.

Jiulize kwa namna hiyo nchi inautawala kweli? vyombo za kiintelejensia viko wapi rais anaomba wamachinga waorodheshe shida zao, ina maana hajui wamachinga wapo TZ, kama anajua hajui shida zao? au ndo anataka awape pesa milioni kadhaa harafu ale kona, zikiisha atunge usanii mwingine. WAMACHINGA WANATAKA SEHEMU ZA KUFANYIA KAZI, WANATAKA WASUMBULIWE WAKIWA WANATEMBEZA BIASHARA ZAO MAANA HUO HASA NDO UMACHINGA, WANATAKA WASAIDIWE ELIMU YA UJASIRIAMALI sasa rais hajui; akili yake anadhani wanataka pesa tu, kwa hiyo anataka aambiwe sh. ngapi hivi zitawanyamazisha hawa wachovu wa TZ
 
ukitaka kumjua adui kummaliza na kumchinja zaidi kaa karibu naye.so magwanda tulikua bega kwa bega ilituweze kuwachinja.we c unaona majembe yote yanavaa nin?kichwa kimoja sawa na wtu mia.mgwada juuu.
 
Nape mjanja sana anatumia style zile zile za makamba!!ubwabwa sana na leta malori toka vijijini wape 10,000 kila mtu cheza ngoma kama vile furahisha meza kuu,......ikija uchaguzi wale wote huwaoni!!

Teh teh. Nshawahi kushuhudia malori kadhaa yakiwa na wanachama wa chama cha Nape miaka kadhaa iliyopita mkoani Tanga. Baada ya sherehe kuisha wanachama wakaanza kulalamika kwamba wameachwa solemba bila hata ya 'maji ya kunywa'
 
Wangewapa na suruali na viatu hata yebo yebo basi maana vile viatu walivyoaa sungusungu vinaidhalilisha CCM
 
...katika maadhimisho ya miaka 35 ya ccm huko mwanza Nape amesema wanachama 1847 wamejiunga na ccm baada ya kukimbia kwa baba yao wa kambo...

Hizo ndizo mbinu za medani katika siasa, nani anataka kupoteza kibarua chake kwa kuzembea cha chama chake kudodora? Unaweza kuta wote waliochukua kadi sio wapya, bali walikuwa na kadi tangu mwaka 2005, sasa zimekusanywa na kupewa upya. Walichofaidi ni kushikwa mkono na Mkuu wa nchi.
 
Hata kama wameletwa na ndege kwani kuna ajabu gani, tatizo lenu nyie CDM mnafikiri kila kitu ni kampeni, hizo zilikuwa sherehe za CCM sio kampeni. Kama wanacdm walitokeza kurudisha kadi basi hiyo ilikuwa zawadi kwa CCM.

CCM walisha shinda na 2015 watashinda kiulaini, hii sherehe ilikuwa ni kuenzi chama. Haya mambo ya kuosha sura tunawaachia kina Slaa na sugu.
 
VIPI WALIPIKA WALI KWENYE KAMPENI..............................??????maana sijaelewa hapa.
 
Magwanda inaonesha mlikuwa mnafatilia kwa makini sana besidei ya CCM Mwanza. Kweli nimeamini CCM ndio namba wani. Kila details za besidei leo tunaipata kutoka kwa magwanda, raha sana. Kumbe walisilimishwa 1,800? na bado.

Sasa tunashauri kitengo cha propaganda kifanye besdei kila wiki na si kila mwaka
CCM juu, juu, juu zaidi

Mamdogo wangu FF mbona unazidi kunikatisha tamaa kila nikijaribu kukuona wewe kama ni objective person unayesimamia unalolijua. Wote tuliowengi humu tulianzia CCM.......lakini unapolazimisha watu waamini kuwa kitendo cha watu kujiunga na CCM ni kusilimishwa ni kukiweka chama chako kwenye wakati mgumu. Utaona ni simple lakini kuna mwana ccm na ni mkristo mzuri sasa akiju kuwa kitendo cha yeye kuwa magamba tayari kasilimishwa......kidogo ina utata. Mie nina imani wewe ni adult. Kweli udini ndo umekushika kiasi hiki ma mdogo?
 
Back
Top Bottom