Nape atimiza umafia Mwanza

Nape atimiza umafia Mwanza

...huwezi kutatua matatizo kwa kutumia njia zilezile ulizozitumia wakati wa kuyapata hayo matatizo...njia tulizotumia kuyapata matatizo ya nchi hii ni ya kuwapigia kura ccm kwa miaka takribani 30 sasa...wanachi wa mwanza na sehemu nyingine yoyote ile Tanzania hapa wanakubaliana na mimi hivyo nape ajue kuwa ccm hatuna ushirika nayo kamwe sisi watanzania
 
...katika maadhimisho ya miaka 35 ya ccm huko mwanza Nape amesema wanachama 1847 wamejiunga na ccm baada ya kukimbia kwa baba yao wa kambo...Nape hajasema baba yao huyo wa kambo ni nani ila mipango yao ya kutengeneza kadi feki kibao za chadema na kugawa kwa hawa watu ili wadai kuzirudisha ilishajulikana...alichokifanya nape ni kutimiza umafia wa kuhadaa wananchi na kukihujumu chadema...kweli ccm ni chama pinzani mwanza leo nimejiridhisha..

alafu wamewatelekeza, magamba bwana!shame on u NAPE! WANADAI HAWANA NAULI YA KURUDI KWAO KISESA, MAGU,NASA, SENGEREMA!JAMANI WAPENI NAULI WARUDI KWAO MBONA HIVYO????
 
Tatizo la Watanzania hilo tu, Yaani kuona hilo vazi basi unahukumu, we una uhakika kwamba hiyo picha ndiyo mwenyewe? au kwa vazi hilo basi una mhukumu kuwa ni muislamu. ooh, Tanzania, watu wako wanaharakati uchwara, wepesi, hawana fikra. Watu kama nyie sijui mtaelimika lini. Acheni kukurupuka na tujaji mambo ya msingi kwa hoja. Poor Tanzania. Sasa wewe tukikupa hata ubalozi wa nyumba mbili si utatuangusha? Acheni siasa za kusoma mwanahalisi. lisingekuwepo ungefanya wapi siasa? Ndugu zangu, mabadiliko tunayatamani hata sasa yaje, lakini si kwa staili hizi za hoja "chapwa"

Mkuu, umekuja kwa jazba mno bila tafakuri walau kidogo kumuelewa Mzito Kabwela alimaanisha nini aliposema "Ndio maana ni vigumu kuitofautisha CCM, CUF na UISLAM" .
Huyo unayemtetea FF aliandika hivi "Kumbe walisilimishwa 1,800? na bado".
Kwa jazba zako hii sentensi ya FF unaielewaje? Kusilimishwa maana yake nini? Ukiishalijibu hilo ndipo utakapomuelewa Mzito Kabwela.
Kaazi kweli kweli !!!!!
 
Naona Nape anatutia aibu sisi vijana. Kusema kweli mimi nilitegemea kuwa kama kijana angekuwa chachu na kuleta mabadiliko ya fikra ndani ya CCM na hasa kwa nafasi aliyopewa. Naona atumia mbinu zilezile za kizamani tu. Ameshindwa kusoma alama za nyakati na ameshindwa kujuwa shauku ya vijana wa nchi hii nini. Nimejaribu kufuatilia namna anavyo fanya kazi zake za uenezi,na kila wakati taa inayowaka ni ya "mawazo mgando ". Kama anataka kufanikiwa atoke huko kwenye upuuzi wa kurudisha kadi na afanye siasa za kisayansi. Mfano amehangaika sana sa siasa za kujivua gamba, bila kuzifanyia utafiti wa kutosha na matokeo yake kile ailichotegemea sicho.

Sasa kuna mawili ama uwezo wake wa kiutendaji ni mdogo hata baada ya kujiandaa kiutafifti na kimkakati ama kwa kawaida uwezo ni mdogo na hivyo hayo anyosema na kutenda ndio level yake.
 
Back
Top Bottom