Nape amekosa uhalali kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea rushwa na matumizi mengine mabaya ya fedha ndani ya ccm. Anazidi kuanika uozo ndani ya chama chake kuwa hakiko makini kuwashughulikia mafisadi kuendelea kujenga mitandao ya urais ndani ya chama.
Cha kujiuliza, kama Nape aligundua kuwa kuna hako ka mchezo ka kupanga wajumbe wa cc na halmashauri kuu yeye kwa nafasi yake na wengine wachukia maovu ndani ya ccm walifanya nini kabla ya yeye kuyasema hayo kupitia makutano show?!
Kama alikaa kimya na hakuweza kusema kitu bora angeendelea kukaa kimya kuliko kuanika udhaifu na upumbavu wao. Mtoto wa baba wa taifa kang'olewa kwa milioni 300 za rushwa, chama kimefanya nini baada ya kugundua kuwa Makongoro kachezewa rafu?! Usanii mtupu.