Nape asema Edward Siyo msafi

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.

Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.

Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.
 
Napeeeeeeeeeeeeeeeeee haya ngoja tuone huu mkanganyiko wenu wa kujikanyaga
 
.......... Nape... Nape..... Nape ! kama anakiri kwamba EL sio msafi.. pengine anao ushahidi wa kuthibitisha hayo..........
 
Kwa pointi ya nape kuwa siyo lazima kuwe na ushahidi badi watu wakihisi na kuongea inadhihirisha uchafu wake bac anakiri chama chao kimejaa mafisadi wengi wakiwemo kina chenge,lowasa et al bt hawachukuliwi hatua.wao kama chama wanafahamu hivyo lakini hakuna uchukuaji wa maamuz magumu kwan ni kanuni zao kulea mafisadi na wezi.watasema yote mpaka tufike 2015.
 
Hili nalo, badala ya kuongelea yaliyotokea wiki hii linazungumzia mambo ya urais 2015 anajuaje usalama wa nchi hadi tufikie uchaguzi huo? Tunsubiri tamko la chama chetu juu ya vurugu zinazoendekea nchini.
 
Itakuwa JK kamdanganya Nape kuwa chaguo lake ni MEMBE na kuwa atahakikisha vyombo vya usalama vinatoa taarifa ya kumchafua Edward Lowassa wakati wa mchujo wa CC ili kwa kigezo hcho Eddo aondolewe na kumpitisha kibaraka Membe.

Lakini jambo ambalo Nape na JK wanasahau ni kuhusu ripoti hiyo hiyo mnamo mwaka 2005 ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TISS ndugu Apson alileta taarifa ya usafi wa kimaadili na JK kuwekwa nafasi ya sita kutokana na tabia zake ambazo usalama uliziona, hata hivyo wajumbe wa CC walizingatia vigezo vingine vya siasa na ushindani na kumpitisha JK apambane na mwandosya na salim na hatimaye akashinda.

Nape awe makini sana anatumika kama galasa kwa JK na Membe, NEC inayochaguliwa na CCM hawana uwezo wa kumpitisha mnafiki MEMBE, nape bado ni kijana asipoangalia hatua zake atajikwaa mapema sana na kwake na Riz 1 , 2015 itakuwa ni giza kubwa sana kwao.
 
Magamba wote wachafu ndio maana Lowassa anachanja mbuga kuelekea 2015...Hakuna hata mmoja wa kumnyooshea kidole na kumwambia, "Kwa ufisadi ulioufanya nchi hii kamwe haustahili kupewa ridhaa na Watanzania ili kuwaongoza, hivyo kaa pembeni."

Mkapa mchafu, Mwinyi mchafu, Kikwete mchafu, SAS naye walishamchafua DHAIFU na kundi lake la mtandao, kwa UDHAIFU huo mkubwa uliopo ndani ya magamba Lowassa anajua watasema pembeni tu lakini hadharani wanaogopa kumkemea maana nao pia ni watenda dhambi hivyo ameanza kutoa rushwa mapema sana ili kujisafishia njia ya kwenda Ikulu 2015. Sijui mpaka tunafika October 2015 atakuwa ametumia mabilioni mangapi katika kutoa rushwa ili kununua ULAIS...Siyo siri nchi yetu imeoza!!!
 
Hivi bado nape yupo? Ni muda kitambo kidogo alikuwa asikiki kabisa.
 
Nepi Samahani Nape kama sio safi amepitaje katika mchujo wenu kugombea nafasi za juu katika chama chenu?USANII MTUPU >MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Nape amekosa uhalali kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea rushwa na matumizi mengine mabaya ya fedha ndani ya ccm. Anazidi kuanika uozo ndani ya chama chake kuwa hakiko makini kuwashughulikia mafisadi kuendelea kujenga mitandao ya urais ndani ya chama.

Cha kujiuliza, kama Nape aligundua kuwa kuna hako ka mchezo ka kupanga wajumbe wa cc na halmashauri kuu yeye kwa nafasi yake na wengine wachukia maovu ndani ya ccm walifanya nini kabla ya yeye kuyasema hayo kupitia makutano show?!

Kama alikaa kimya na hakuweza kusema kitu bora angeendelea kukaa kimya kuliko kuanika udhaifu na upumbavu wao. Mtoto wa baba wa taifa kang'olewa kwa milioni 300 za rushwa, chama kimefanya nini baada ya kugundua kuwa Makongoro kachezewa rafu?! Usanii mtupu.
 
Nape ni sawa na mbwa kibogoyo. Hang'ati. Amejaa unafiki mtupu. Hana uwezo wa kupambana na rais mtarajiwa wa Tanzania, Hon Edward Lowassa. 2015 ataumbuka sana huyo Nape.
 
Mtoto mnamfundisha kuongea akishajua anaanza kuropoka siri za ndani.Kama EL sio msafi na yupo kwenye cc ya chama inamaana wote huko ni wachafu ndio maana wamemkumbatia.
 

Similar Discussions

17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom