MgungaMiba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2011
- 999
- 816
Jana nzima na leo mjini Hai kulikuwa na matangazo katika magari ya vipaza sauti kuwa leo Jumaamosi kutakuwa na mkutano wa hadhara utakao hutubiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa CCM Bw Nape Nauye. Lakini bahati mbaya mpaka kufikia saa 10:30 hali ya mahudhurio ya watu katika uwanja wa Snow View ilikuwa hairidhishi kabisa (very pathetic) pamoja na jitihada za kuleta watu kutoka Rombo, Moshi mjini nk. Chakusikitisha zaidi ni kuwa Bw Nape hakutokea kabisa uwanjani hapo japo kuna tetesi kuwa alishafika Moshi mjini, lakini kutokana na mahudhurio hayo hafifu, alishauriwa asifike kabisa, wakati huohuo kuna taarifa kuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe alikuwapo mjini Hai kwa shughuli za kawaida jimboni mwake.