Nape aimba: Uamsho bye bye!

Nape aimba: Uamsho bye bye!

Kile kilikuwa kijembe cha uhakika kwa viongozi fulani ndani ya CCM , toka Zanzibar waliokipigia chapuo hicho kikundi cha Uamsho.
Sasa kiongozi wao kaondoka nadarakani ndani ya chama- ndiyo bye bye yenyewe!
Alaa kumbeee! ndio maana uamsho walikuwa na confidence ile!! walijua Karume anawalinda na kusukuma mapambano kutokea ndani ya chama.UAMSHO WASHINDWE NA WALEGEE.
 
Nilikuwa nafuatilia matokeo ya uchaguzi ccm. Baada ya kutangazwa mwenyekiti na makamo mwenyekiti, Nape akaaanza kuimba" uamsho bye bye".
Hii ina maana gani? Kuwa uamsho ni sehemu ya ccm na leo wameshindwa? Nisaidieni wakuu.

Sio KUNDI kutoka Z'Bar ni NGO iliyoanzishwa ZANZIBAR kwa Wa-Zanzibari kuwahamasisha KISIASA; KIITIKADI kutosahau UHURU walionao Wakati wa UTAWALA wa SULTANI
 
Uamsho uko chini ya cuf, huo ndo ukweli mchungu kumeza!
Tena Mlezi na mratibu wa shughuli zao visiwani na bara Maalim Seif na CUF yao - Makamu wa Rais! Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako. Hivi hii nchi ina Usalama wa Taifa kweli?
 
kama ulisikiliza hotuba ya Amani Abeid Karume ungejua nani analengwa, mzee karume ni muamsho na alimjibu Nape kuwa anaakili ya samaki.
 
Daudi mchambuzi unaakili natafuta post yako nikugongee like siioni
 
Nilikuwa nafuatilia matokeo ya uchaguzi ccm. Baada ya kutangazwa mwenyekiti na makamo mwenyekiti, Nape akaaanza kuimba" uamsho bye bye".
Hii ina maana gani? Kuwa uamsho ni sehemu ya ccm na leo wameshindwa? Nisaidieni wakuu.

. .......hilo ndio jibu......kwamba uamsho ni ccm na ccm ni uamsho........ .
 
. .......hilo ndio jibu......kwamba uamsho ni ccm na ccm ni uamsho........ .

Usitake kujishebedua mkuu, nani asiyejua kuwa walioifadhili uamsho ni watu kama mama Karume aliyekiri kuwapokea na kuonge nao.
Kama mama Karume aliwapokea na kuonge nao mwanawe Amani je?

Hiyo bye bye ni kwa ajili yao.
Ni wazi hawapo pamoja nasi watanzania.
 
Alikusudia kumsema Karume,
na karume alimjibu kupitia hotuba yake ila wachache wenye akili ndo waligundua hili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Sio wote tulioangalia hio speech so eleza
 
Acheni kumung'unya maneno Nape alimaanisha uamsho kama wale wote wanaoamini katika kudai hakizao kwa maandamano na fujo
 
Hii ni kuchochea hasira za watu, ni sawa na kumchoma mtu msumari kwenye kidonda,
sijajua ni lini watu watakuwa na akili, nchi inazizima kwa vurugu za kidini,
Nape kama kiongozi wa ngazi ya juu anaimba nyimbo ambazo zilitakiwa ziimbwe na wale
watoto wadogo wakicheza mdako, hivi kweli kwa hali hii tutafika.
 
Back
Top Bottom