Nape aimba: Uamsho bye bye!

Nape aimba: Uamsho bye bye!

Asilimia kubwa ya wanamagamba wana vipaji vya kuzaliwa vya miziki yenye asili ya Taarabu na Mipasho..... Sijui kwa nini hawaendelezi vipaji vyao wanarukia kwenye siasa?

Hata baba yake Nape, Moses Nnauye alikuwa mwanamuziki anayepiga accordion.
 
[h=5]What a leader! What a speech! Rais Mstaafu wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM (Zanzibar), Mhe. Amani Karume, amewapa darasa zuri la uongozi na demokrasia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama chake na wananchi kwa ujumla hasa kuhusiana na mwelekeo wa siasa Zanzibar. Alisema hali ya kisiasa Zanzibar ni ya kuridhisha na yenye amani na utulivu ambapo fujo na ghasia za hapa na pale zinatokana na wanaharakati na siyo wanasiasa. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikubaliwa kupitia vikao vya CCM lakini iliamuliwa kwa kupitishwa na Wazanzibari ambao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ndiyo waamuzi wa mwisho wa mustakbali wa kisiasa wa Zanzibar. Viongozi wa CCM Zanzibar wasipowatendea wema wananchi watawakumbuka wakati wa uchaguzi ukifika. Ubaguzi, ubabe na kuchochea mfarakano si katika malengo ya ASP. Kila mtu aachiwe kuwa huru kutoa maoni anayoyataka kuhusiana na Mjadala wa Katiba Mpya na watu wasiitwe majina mabaya kwa sababu tu maoni wanayotoa hayaungwi mkono na baadhi ya watu. Tumewataka watu watoe maoni yao, basi tuheshimu mawazo yao. Wanaotaka Muungano uendelee ni haki yao, wanaotaka Serikali mbili kama zilivyo, wanaotaka Serikali mbili za Mkataba, wote waheshimiwe. Tume ya Katiba ndiyo iliyopewa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi, iachiwe ifanye kazi yake. Hatimaye maoni ya walio wengi yaheshimiwe. Uongozi ni kazi nzito, na mimi nina asili ya ubaharia kupitia kwa baba yangu. Leo nakiegesha chombo salama bandarini na nina-sign off. Ni jukumu la wenzangu sasa kukipeleka chombo salama. Muhimu tujifunze kuvumiliana. Hapa kwenye Mkutano Mkuu huu, Mwenyekiti kaalika viongozi wa vyama vya upinzani na wametwambia maneno ya maana ya kutushauri. Ingekuwa Zanzibar kumefanyika yale tungeitana kila majina mabaya. Tujifunze kuvumiliana.

[/h]
 
What a leader! What a speech! Rais Mstaafu wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM (Zanzibar), Mhe. Amani Karume, amewapa darasa zuri la uongozi na demokrasia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama chake na wananchi kwa ujumla hasa kuhusiana na mwelekeo wa siasa Zanzibar. Alisema hali ya kisiasa Zanzibar ni ya kuridhisha na yenye amani na utulivu ambapo fujo na ghasia za hapa na pale zinatokana na wanaharakati na siyo wanasiasa. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikubaliwa kupitia vikao vya CCM lakini iliamuliwa kwa kupitishwa na Wazanzibari ambao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ndiyo waamuzi wa mwisho wa mustakbali wa kisiasa wa Zanzibar. Viongozi wa CCM Zanzibar wasipowatendea wema wananchi watawakumbuka wakati wa uchaguzi ukifika. Ubaguzi, ubabe na kuchochea mfarakano si katika malengo ya ASP. Kila mtu aachiwe kuwa huru kutoa maoni anayoyataka kuhusiana na Mjadala wa Katiba Mpya na watu wasiitwe majina mabaya kwa sababu tu maoni wanayotoa hayaungwi mkono na baadhi ya watu. Tumewataka watu watoe maoni yao, basi tuheshimu mawazo yao. Wanaotaka Muungano uendelee ni haki yao, wanaotaka Serikali mbili kama zilivyo, wanaotaka Serikali mbili za Mkataba, wote waheshimiwe. Tume ya Katiba ndiyo iliyopewa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi, iachiwe ifanye kazi yake. Hatimaye maoni ya walio wengi yaheshimiwe. Uongozi ni kazi nzito, na mimi nina asili ya ubaharia kupitia kwa baba yangu. Leo nakiegesha chombo salama bandarini na nina-sign off. Ni jukumu la wenzangu sasa kukipeleka chombo salama. Muhimu tujifunze kuvumiliana. Hapa kwenye Mkutano Mkuu huu, Mwenyekiti kaalika viongozi wa vyama vya upinzani na wametwambia maneno ya maana ya kutushauri. Ingekuwa Zanzibar kumefanyika yale tungeitana kila majina mabaya. Tujifunze kuvumiliana.
Hotuba ya Mhe Karume ni ishara ya mtu aliyekata tamaa.
He's dipping into obscurity.

Kosa kubwa alilofanya ni kutoyasema haya wakati yuko madarakani.
Mbaya zaidi ni kuingia ubia na Uamsho katika siasa ambazo zimeishia kuchoma makanisa na kuchimba barabara huko zanzibar.
Na ndio maana anaonekana mtu wa ajabu sana kusema aliyosema wakati hana madaraka, hana ushawishi na amepoteza hata umaarufu wake kwa kujiingiza uhusiano na watu wasio itakia mema Tanzania.
 
Halafu kama ni huyu Karume kuwa mwana Uamsho kwanini serikali isimchulie hatua kama Aboud Jumbe alivyofanyiwa alipotaka kusaini mapendekezo ya mwanasheria mkuu Zanzibar ili kuvunja muungano enzi akiwa Rais wa Zanziar ambapo hadi leo yupo hapo Kigamboni kama raia fulani sawa na mimi na wewe. Achukuliwe hatua na huyo Karume.
 
Hata baba yake Nape, Moses Nnauye alikuwa mwanamuziki anayepiga accordion.

Nikiwa JKT Mafinga kwa mujibu wa sheria Brigedia Moses Nnauye alikuja na kijana wake mdogo sana wakati huo ambaye ndiye Nape (Nnape) Nnauye, hakika yule mzee aliimba nyimbo mbalimbali za zamani wakati Nape akipiga kinanda.
Nyimbo walizotuimbia ni "Waniuaua kipenzi waniuaua, Malaika nakupenda malaika, Tausi ndege wangu, nk"
 
Kile kilikuwa kijembe cha uhakika kwa viongozi fulani ndani ya CCM , toka Zanzibar waliokipigia chapuo hicho kikundi cha Uamsho.
Sasa kiongozi wao kaondoka nadarakani ndani ya chama- ndiyo bye bye yenyewe!

Hivi huyu nape hakuona kitu ingine zaidi ya uamsho? je ufisadi vipi? si kila siku wanaimba kukomesha mafisadi? au kinyume chake! huyu ana ajenda ingine sio bure!
 
uamsho itabaki pale pale ila haitakuwa taasisi rasmi
 
Kwa mujibu wa habari za chini chini inadaiwa Rais mstaafu wa Zanzibar Abeid Amani Karume analiunga mkono kundi la uamsho hivyo nape kuimba 'Uamsho bye bye' ni kumkejeli Karume kwakuwa nafasi yake ya umakamu wa CCM Z'bar sasa imechukuliwa na Shein
 
Akiuchangamsha umati wa wana CCM hapo Kizota, nimemsikia Nape akiimba kwa hamasa kubwa, huku akishangiliwa na umati wa mkutano huo:
Uamsho bye bye!
Uamsho bye bye!

Ningependa kukubaliana naye kwa dhati, ila kuna aliyekusudiwa?

nae huyu mtoto wa kuzaliwa kwenye madansa wakati huo...anajidai..kwa wasiomjua....

uamsho ni tayari imeshaamsha watu na yale yapo ndani ya wazanzibar wengi...wenye uchungu na nchi yao..huwezi kuifuta tena...hata nape akiamua kuwapa sumu kina farid na wenzake....walicho kihubiri kuhusu muungano na ubaya wake kwa zenji kila mtu ameelewa...watoto na vijana waliokua hawajui sasa wanajua..tayari wamefanya kazi nzuri ila mapambano yanaendelea....kazi ya kudai uhuru na haki ni ngumu na ndefu.....na pia ni chungu...kina lumumba walipoteza maisha yao kwa kudai uhuru kamili wa Congo...walikuwepo kina nape pia amabo ndio hao kina mabutu....lakini tunasema aluta tunaendela
 
Back
Top Bottom