Nape adai kunasa nyaraka za Marando | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape adai kunasa nyaraka za Marando

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 4, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Nape adai kunasa nyaraka za Marando Saturday, 04 June 2011 09:49 :peace:
  Mwandishi Wetu, Mpanda
  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amedai kuwa amenasa barua za mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, akikana kuwaambia Watanzania kuwa yeye (Nnauye) alifaidika na fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

  Nape aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika mjini Mpanda, mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake.

  "Kimsingi namheshimu sana Marando, lakini kitendo cha kuchanganya uwakili na siasa karibuni kitamgharimu, hasa siasa za majitaka za Chadema," alisema Nape huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika katika mkutano huo.

  Alisema kufuatia hatua yake ya kupata ushahidi wa nyaraka, anamtaka Marando kuchagua ama kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kwa sababu kufanya vyote kwa pamoja kutamgharimu.

  Nape alisema madai ya Marando dhidi yake, aliyatoa hivi karibu baada ya yeye kumtaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa, aache unafiki kwa kueleza sababu za kulipwa na chama chake Sh 7.5 milioni kila mwezi tena bila kuzilipia kodi.

  Alisema rai yake wa Dk Slaa, ilitokana na ukweli kwamba aliwahi kupinga wabunge kulipwa mshahara usiofikia kiasi hicho kwa kwa maelezo kuwa ni mkubwa.

  Alisema badala ya raia hiyo kujibu na Dk Slaa, Chadema ilimtumia Marando ambaye alitoa tuhuma kwamba Nape ni miongoni mwa waliofaidika na fedha za EPA wa msingi huo ni mmoja wa mafisadi.

  Kwa mujibu wa Nape, katika madai yake Marando alidai kuwa yeye (Nape) alipewa fedha hizo za wizi na mfanyabiashara mmoja wa jijini Dar es Salaam.

  "Nilishituka sana kusikia mtu ninayemheshimu akitoa tuhuma hizo mzito, nikajua ndio matatizo ya kuchanganya siasa na uwakili, siasa zenyewe za Chadema. Lakini cha ajabu baada ya siku chache Marando amemwandikia mfanyabiashara huo, akikanusha taarifa ile na kuisukumia Chadema,"alisema Nape.

  "Nadhani ni muhimu Marando akachagua kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kabla aibu kubwa haijamkuta," alisistiza.

  Akionyesha kujiamini kuwa ana nyakaraka za uthibitisho, Nape alisema anazo barua za mawasiliano kati ya mfanyabiashara huyo na Marando, zinazoonyesha wakili huyo alikataa katakata kuhusika na kauli iliyonukuliwa kwenye vyombo vya habari.

  Kwa mujibu wa Nape barua hizo ni pamoja na ya Mei 16 mwaka huu iliyoandikwa na mfanyabiashara huyo kwenda kwa Marando ikimtaka aeleze sababu za kumhusisha naye katika tuhuma za fedha za EPA.
  "Wananchi yapo mengi kama hili ambayo viongozi wa Chadema wanawadanganyeni kupitia kwenye mikutano au vyombo vya habari, lakini kwa kutojua baadhi yenu huwa mnawaami . Kitendo hiki kinamfanya Marando na chama chake wasiaminike kwa umma," alidai.

  Nape alisema, bila aibu Marando anamkana Antoni Komu na chama kuwa hakuunga mkono tuhuma hizo dhidi yake.


  Source: Mwananchi
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Chonde chonde Nape, hao akina Marando na Slaa huwawezi! Concentrate na issue za chama chetu! Tunataka kusukia kwako mwananchi ananeemeka vip kutokana na CCM kuwa madarakani na siyo kila siku kuongelea CDM majukwaani
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Go Nape Go!
  Nape anafanya vepa kwa kula sahani moja na hawa watu.
  Si muda mrefu tutaanza kuona tofauti ya pumba na mchele.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hivi haya yote yana faida gani kwetu commoners? aani ziara zote ni kujibizana tuuuu, tuwatofautisheje na taarabu? Nape na wenzio nendeni kwenye mustakabali wa nchi hii achana na hayo utazidi kujifunua tu!
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Miaka yote hii hamsini ya uhuru hujaona pumba na nchele tu? Labda tukupe mia!
   
 6. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Nape mpeleke marando mahakamani
   
 7. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Crap crap
   
 8. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hahahahahaha ha ha ha,,,umenifurahisha
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Naona anatafuta mwisho wake uwe mbaya huyu Napelape
   
 10. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Haa ha ha..si-hasa za Marando ni noooma, naona anauma huku na kupuliza kule mwisho wa siku anapata kotekote, kaazi kwelikweli!!

  CCM imefanya vizuri sana kumpata Nape, so far ameifanya kazi yake vizuri sana.
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  We pay him for that,ataitangaza chadema kila anapo enda,hata pale ambapo haijasikika
  atakua kipaza sauti chetu,..
  in return,wananchi watataka kujua "hawa chadema ni kina nani,kwa nini ccm ina wahofia"
  then....
  Dr. akipita huko,waka fananisha na pumba za Nepe neyuye watajua nani wa kufuata,
  nani wa kutosa
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kama kweli walio hudhuria ni "maelfu" afu akashangiliwa na "mamia"
  basi wananchi wanajua pumba ni zipi na mchele ni upi!!!!!!
   
 13. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,328
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Is this a real meaning of politics?kma ndiyo hiv tz tuna safar ndefu sana.Wenzetu wanawaza jins ya kuendelea ss tunalumbana na nadhan media nazo zingewachunia hawa wana si hasa
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,282
  Trophy Points: 280
  ATAKUWA ANATIKISA MBUYU! Au kupiga nyuki busu
   
 15. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hivi bado tuko kwenye kampeni? ccm watekeleze ahadi walizowadanya wadanganyika,cdm ni kazi yao kuifanya ccm isitawale=nchi isitawalike kama ccm hawako double standard basi msemo wa dr slaa nchi haitatawalika umetimia ccm ni chama cha upinzani kwa sababu cdm wanaanzisha hoja wao ndo wanapinga.MPINZANI NI NANI SASA
   
 16. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Tutaendelea kufanywa wajinga kwa hii michezo ya watu wa hovyo kama hawa CCM,
  Nchi ipo mikononi mwao kwa miaka 50 sasa......
  Amejisemea Mzee Jenerali Ulimwengu, wao bado wanacheza "Nachi" (wakati maandishi 12 yapo ukutani)
  Pitieni rai hii ya Jenerali na muache ushabiki wenu hapa nchi inazama hii
   
 17. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tunaomba kwenye hiyo mikutano tuambiwe sera za CCM na jinsi zinavyotekelezwa kumkomboa mtanzania wa kawaida maskini wa hapo Mpanda na kwingineko Tanzania. Kwani siasa ya Tanzania ni CCM na CHADEMA tu jamani. Mbona kuna CUF,TLP,UDP,PPT,CCJ nk. CCM kwa sasa wa-concentrate kwenye kutekeleza na kuwaonyesha wananchi kwamba wanatekeleza sera za chama,na wapi wamefika mpaka sasa.Mfano mzuri ni TATIZO LA UMEME WA UHAKIKA. Bila hivyo itafika 2015 hakuna lililofanyika,na hao CHADEMA ndio watapata muda wa kuwabana vizuri.
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Hii mkuu imetulia sana.
   
 19. Meking

  Meking JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama kuna sehemu hamjasikika mpaka sasa, sijui kama mtafika mkuu. Na sijui hali ilikuwaje huko miezi sita iliyopita, kipindi mlipodai kuibiwa kura.
  Halafu mnafanya vizuri kumlipa Nape, just hope he is getting your job very well done...
   
 20. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwenye Tv tumeonyeshwa huko huko Rukwa Sumbawanga kuna walimu wa Sekondari wameandamana kwenda kwa Mkurugenzi wakitaka kuondoka kwenye vituo vyao vya kazi kutokana nakutolipwa Mishahara ya Miezi mitatu yaani tangia wameajiriwa hawajaingizwa kwenye Pay roll...!Jifikirie Mazingira ya Sumbawanga ambapo watu wengi wakipangiwa kufanya kazi huko wanagoma kwenda bado hawa waliojitoa muhanga nao hakuna anayewajali Je ni Mtumishi gani leo akipangiwa Sumbawanga atakubali kwenda Kuripoti?Nape ├Ângelea mambo ya Msingi na uache kupiga Blabla shule hazina Walimu waliopo hawaangaliwi Chama chako kinachukua hatua gani,Ishu yako na Marando inawasaidia nini Wanasumbawanga ambao watoto wao hawafundishwi mwisho wa siku wanatoka na Div-0.
   
Loading...