Nape adai kunasa nyaraka za Marando

Nape is just full of hot air!
Sijui kama wakubwa wa ccm walijua hilo kabla ya kumpa kazi inayomzidi umri, akili na hata maarifa. bad news through and through!
 
hongera nape na hongera jk kwa kumteua nape.

amewashika pabaya chadema. anakula nao sahani moja.

ukiona hapa jf wanapiga kelele jua chadema imekamatwa pabaya.

hata daktari wa wakatoliki kapotea baada ya kuumbuliwa na nape na mshahara bila kodi.

nape udumu baba. chadema wanafiki wakubwa.

marando anapinga ufisadi kwa kumwakilisha fisadi jeetu.
 
hongera nape na hongera jk kwa kumteua nape.

amewashika pabaya chadema. anakula nao sahani moja.

ukiona hapa jf wanapiga kelele jua chadema imekamatwa pabaya.

hata daktari wa wakatoliki kapotea baada ya kuumbuliwa na nape na mshahara bila kodi.

nape udumu baba. chadema wanafiki wakubwa.

marando anapinga ufisadi kwa kumwakilisha fisadi jeetu.


In your dreams! Nape = copy & paste! aibu.
 
hongera nape na hongera jk kwa kumteua nape.

amewashika pabaya chadema. anakula nao sahani moja.

ukiona hapa jf wanapiga kelele jua chadema imekamatwa pabaya.

hata daktari wa wakatoliki kapotea baada ya kuumbuliwa na nape na mshahara bila kodi.

nape udumu baba. chadema wanafiki wakubwa.

marando anapinga ufisadi kwa kumwakilisha fisadi jeetu.

Hivi jamani haya malumbano ya kushikana pabaya sijui pazuri yanatusaidia nini? Ktk maendeleo yetu hebu acheni kushikanashikana tuleteeni maendeleo na mtimize yale mlioahidi sio kuzungusha shanga mkidai kushika watu
 
lakini tuwe realistic. Si kwamba Nape anayo alternative. atazungumza nini? anaowahutubia hali yao ni ngumu kwelikweli. vitu bei juu, kila kitu hovyo. na akijaribu kuwa realistic, ataishia kufoka juu ya ubadhirifu, uzembe, uozo unaofanywa katika serikali ya chama chake cha CCM, ambayo ndiyo kelele ya CHADEMA. ndivyo ilivyomtokea Pinda alipokwenda Kagera "kufuta nyayo" za CHADEMA. aliishia kukemea tu uozo ambao ndio CHADEMA walikuwa wanazungumzia. hivi kwa vyovyote vile, Nape hana ujanja: ama akemee uozo wa serikali ya CCM, ambayo ndiyo kazi wanayoifanya CHADEMA, au atafute namna ya kuiongelea CHADEMA moja kwa moja. hawezi kukwepa ama kuiongelea CHADEMA, au kurudia maneno ya CHADEMA.
 
Ooooh,so ataenda mahakamani au?na ridhwani nae aliyetoa siku 7?
Tanzania kuna visa.........
 
hongera nape na hongera jk kwa kumteua nape.

amewashika pabaya chadema. anakula nao sahani moja.

ukiona hapa jf wanapiga kelele jua chadema imekamatwa pabaya.

hata daktari wa wakatoliki kapotea baada ya kuumbuliwa na nape na mshahara bila kodi.

nape udumu baba. chadema wanafiki wakubwa.

marando anapinga ufisadi kwa kumwakilisha fisadi jeetu.

unalipwa tsh. ngapi?
 
lakini tuwe realistic. Si kwamba Nape anayo alternative. atazungumza nini? anaowahutubia hali yao ni ngumu kwelikweli. vitu bei juu, kila kitu hovyo. na akijaribu kuwa realistic, ataishia kufoka juu ya ubadhirifu, uzembe, uozo unaofanywa katika serikali ya chama chake cha CCM, ambayo ndiyo kelele ya CHADEMA. ndivyo ilivyomtokea Pinda alipokwenda Kagera "kufuta nyayo" za CHADEMA. aliishia kukemea tu uozo ambao ndio CHADEMA walikuwa wanazungumzia. hivi kwa vyovyote vile, Nape hana ujanja: ama akemee uozo wa serikali ya CCM, ambayo ndiyo kazi wanayoifanya CHADEMA, au atafute namna ya kuiongelea CHADEMA moja kwa moja. hawezi kukwepa ama kuiongelea CHADEMA, au kurudia maneno ya CHADEMA.


Sijui haya mkuu yataisha lini
Sioni haja ya kuongelea issue ya Marando na Nape wala nani sijui
Yako mambo ya muhimu ya kuongelea
maisha bora kwa mtanzania wa Sumbawanga yatafika lini, bei ya bidhaa itashuka lini, mafuta juu, umeme wa mgao, barabara mbovu za kusafirisha mazao yao, ubadhirifu wa mamilioni kila sekta mpaka halmashauri za wilaya, badala haya yaongelewe tunaelezwa kuna barua ya Nape na Marando then hiyo barua kwa mwanasumbawanga inamfikisha wapi na inamsaidia nini
Tufike mahali haya malumbano ya vyama yaishe tuelezwe sera na mipango ya kupunguza umaskini wetu wa tanzania
 
nape asidanganye watu kama marando anajua huo ni uongo alitoa siyo kitu laisi kuandika barua kupinga hilo wakati anajua barua inaweza pelekwa ccm kuonyesha kwamba huo ni uongo na akaonekana ayuko makini hizo ni propaganda za nape na ccm yake
 
kama kweli walio hudhuria ni "maelfu" afu akashangiliwa na "mamia"
basi wananchi wanajua pumba ni zipi na mchele ni upi!!!!!!

Mheshimiwa: umedadafua vizuri, hii ndiyo faida ya kusoma na kujua hesabu, kama kweli waliodhuria ni MAELFU na walioshangilia mada ya Nape ni MAMIA kweli CCM kazi wanayo: ni bora atulie tu kwenye nafasi aliyopewa ya ukuu wa Wilaya vinginevyo anajitafutia ugonjwa wa moyo.
 
hongera nape na hongera jk kwa kumteua nape.

amewashika pabaya chadema. anakula nao sahani moja.

ukiona hapa jf wanapiga kelele jua chadema imekamatwa pabaya.

hata daktari wa wakatoliki kapotea baada ya kuumbuliwa na nape na mshahara bila kodi.

nape udumu baba. chadema wanafiki wakubwa.

marando anapinga ufisadi kwa kumwakilisha fisadi jeetu.

Aliyeshikwa pabaya ni chama cha magamba hawatekelezi ilani yao badala yake wanatekeleza ya cdm,marekebisho ya katiba haikuwepo kwenye ilani yao na safari hii wataenda ahera kwa sababu janja yao ya kuchakachua haitawezekana,tutalala takrir square.Nawashangaa ccm eti leo kwenye gazeti la udaku la jambo leo wanasema maandamano yao mpanda yanazidi ya cdm,kumbe cdm ndo SI unit mmeliona hlo endeleeni kulipa promo chama linalowatawala.
 
Nape adai kunasa nyaraka za Marando Saturday, 04 June 2011 09:49 :peace:
Mwandishi Wetu, Mpanda
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amedai kuwa amenasa barua za mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, akikana kuwaambia Watanzania kuwa yeye (Nnauye) alifaidika na fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

Nape aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika mjini Mpanda, mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake.

"Kimsingi namheshimu sana Marando, lakini kitendo cha kuchanganya uwakili na siasa karibuni kitamgharimu, hasa siasa za majitaka za Chadema," alisema Nape huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika katika mkutano huo.

Alisema kufuatia hatua yake ya kupata ushahidi wa nyaraka, anamtaka Marando kuchagua ama kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kwa sababu kufanya vyote kwa pamoja kutamgharimu.

Nape alisema madai ya Marando dhidi yake, aliyatoa hivi karibu baada ya yeye kumtaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa, aache unafiki kwa kueleza sababu za kulipwa na chama chake Sh 7.5 milioni kila mwezi tena bila kuzilipia kodi.

Alisema rai yake wa Dk Slaa, ilitokana na ukweli kwamba aliwahi kupinga wabunge kulipwa mshahara usiofikia kiasi hicho kwa kwa maelezo kuwa ni mkubwa.

Alisema badala ya raia hiyo kujibu na Dk Slaa, Chadema ilimtumia Marando ambaye alitoa tuhuma kwamba Nape ni miongoni mwa waliofaidika na fedha za EPA wa msingi huo ni mmoja wa mafisadi.

Kwa mujibu wa Nape, katika madai yake Marando alidai kuwa yeye (Nape) alipewa fedha hizo za wizi na mfanyabiashara mmoja wa jijini Dar es Salaam.

"Nilishituka sana kusikia mtu ninayemheshimu akitoa tuhuma hizo mzito, nikajua ndio matatizo ya kuchanganya siasa na uwakili, siasa zenyewe za Chadema. Lakini cha ajabu baada ya siku chache Marando amemwandikia mfanyabiashara huo, akikanusha taarifa ile na kuisukumia Chadema,"alisema Nape.

"Nadhani ni muhimu Marando akachagua kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kabla aibu kubwa haijamkuta," alisistiza.

Akionyesha kujiamini kuwa ana nyakaraka za uthibitisho, Nape alisema anazo barua za mawasiliano kati ya mfanyabiashara huyo na Marando, zinazoonyesha wakili huyo alikataa katakata kuhusika na kauli iliyonukuliwa kwenye vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa Nape barua hizo ni pamoja na ya Mei 16 mwaka huu iliyoandikwa na mfanyabiashara huyo kwenda kwa Marando ikimtaka aeleze sababu za kumhusisha naye katika tuhuma za fedha za EPA.
"Wananchi yapo mengi kama hili ambayo viongozi wa Chadema wanawadanganyeni kupitia kwenye mikutano au vyombo vya habari, lakini kwa kutojua baadhi yenu huwa mnawaami . Kitendo hiki kinamfanya Marando na chama chake wasiaminike kwa umma," alidai.

Nape alisema, bila aibu Marando anamkana Antoni Komu na chama kuwa hakuunga mkono tuhuma hizo dhidi yake.


Source: Mwananchi
Nitarudia mara kwa mara hivi sisi ni wavivu wa kusoma au vipi?
Hapo kwenye red chini ndio nyaraka ya Marando anayojivunia Nepi Nawewe? Adokeze hizo nyaraka kama alivyodokeza ya huyo Tajiri, kwani hata yeye anaweza kumuandikia Marando maneno ya kipuuzi tu, kwahiyo atadai ni nyaraka za Marando.
CCM amkeni tuelezeni ktk miezi nane hii tu ni ilani, sera, ahadi gani mmeshawatekelezea Watanzania?
 
Cdm,cdm ... Kila siku cdm. Nape kama hauko serious sasa unapotea mwenyewe. Ivi ukiitangaza ivo cdm ujui kuwa watu watasahau ccm yani kila utakapoenda watu watapenda kusikia unaiongeleaje cdm. Yan hujataja cdm watu wanaisi labda umesahau,mwisho wa siku kila mtu anawinda taarifa za cdm na hapo ndo watu wataisaau ccm. Ujue ccm imeshikwa akili,ukitaka ccm waimbe cdm,basi ni kutaja kashfa zao,hapo ndo usahau kila kitu na kuanza kuwaimba cdm. Kwa ili cdm wamefanikiwa kuwawekea maneno mdomoni ccm.
 
Miaka yote hii hamsini ya uhuru hujaona pumba na nchele tu? Labda tukupe mia!

Usikonde mkuu!
Bwana mdogo Nape kawavalia njuga na anacheza ngoma mnayoifahamu vyema.
Unajua debe tupu haliachi kutika na amelionyesha vema debe hilo.
Tatizo kubwa kuna wanasiasa uchwara wanajilinganisha wao wenyewe na uadilifu wa Mwalimu, uadilifu ambao hawana, huku wakiimba majukwaani sera zisizo na mshiko.
Ni vizuri kuumbua uozo, lakini ule wa kwako mwenyewe unauficha chini ya kitanda au maelezo mareeefu yasiyo na maana!
Kuwapa mimba wake za watu is not exactly exemplary, not in the least kama hamjaoana.
Bulungutu la chama wasela wanalogawana, na jinsi wanavyogawana linanishawishi kuwa ufisadi ni kila mahala.
Yote haya wakati kabla ya uhuru Mwalimu alikuwa akinyonga baiskeli toka Pugu hadi Kariakoo akigombea uhuru wa Mtanganyika
Nape anawaumbua wafanyabiashara hawa ndani ya chama cha upinzani!
WIZI MTUPU!
 
PATA HABARI KAMILI:

Katibu wa NEC, CCM Itikadi na Uenezi Taifa Nape Nnauye amedai kunasa barua za Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na wakili maarufu nchini Mabere Marando akikana kuwaambia Watanzania kuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Mnauye alifaidika na fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA).


Amesema kutokana na kuupata ushahidi wa nyaraka hizo, anamtaka Marando kuchagua kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kwa kuwa kuendelea na vyote kutamgharimu.

Nape aliyasema hayo jana kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini hapa mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa nji huo na vitongoji vyake.

" Kimsingi namheshimu sana Marando lakini kitendo cha kuchanganya uwakili na siasa karibuni kitamgarimu, hasa siasa za majitaka za CHADEMA", alisema Nape huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano huo.

Nape alisema, hivi karibu alipomtaka Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilibrod Slaa aache unafiki kwa kueleza kwanini analipwa na chama cheke sh. milioni 7.5 kwa mwezi tena bila kuzilipia kodi, wakati aliwahi kupinga wabunge kulipwa mshahara usiofikia kiasi hicho kuwa ni kubwa, badala ya kujibu yeye, CHADEMA ilimtumia Marando kutoa shutuma kuwa Nape naye ni miongoni mwa waliofaidika na fedha za EPA, hivyo ni fisadi.

Katika madai hayo Marando alidai Nape alipewa fedha hizo za wizi na mfanyabiashara Jayantkumar Patel ambaye kwa mujibu wa maelezo aliyokaririwa Marando na baadhi ya vyombo vya habari alidai Patel alimtaja Nape kwenye tume ya Rais ya iliyokuwa inashughulikia swala la EPA.

"Nilishituka kusikia yale maneno yakisemwa na mtu ninayemheshimu, nikajua ndio matatizo ya kuchanganya siasa na uwakili, siasa zenyewe za CHADEMA. Lakini cha ajabu baada ya siku chache Marando amemwandikia Jeetu Patel akikanusha taarifa ile na kuisukumia CHADEMA" Alisema Nape na kuongeza: "Nadhani ni muhimu Marando akachagua sasa kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kabla aibu kubwa haijamkuta".

Akionyesha kujiamini kuwa na nyakaraka za uthibitisho, Nape alisema anazo barua za mawasiliano kati ya Jeetu Patel na Marando zinazoonyesha Marando akikataa katakata kuhusika na kauli iliyonukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba Nape alinufaika na fedha za EPA.

Kwa mujibu wa Nape barua ya Jeetu Patel ya Mei 16, 2011 kwenda kwa Marando ikimtaka aeleze kwanini alimhusisha Nape na fedha za EPA huku akijua si kweli, huku barua nyingine ikiwa ya Marando ya tarehe hiyo hiyo, kwenda kwa Jeetu Patel akajitetea kwamba aliwashauri CHADEMA wasimshutumu Nape kwa EPA bila mafanikio, naye akaamua kuuaminisha uma jambo asiloliamini.

"Wananchi yapo mengi kama hili ambayo viongozi wa CHADEMA huwadanyeni kupitia kwenye mikutano au vyombo vya habari, lakini kwa kutojua baadhi yenu huwa mnawaami . Kitendo hiki kinamfanya Marando na chama chake wasiaminike kwa umma.

Nape alisema, bila aibu Marando anamkana Antoni Komu na Chama chake cha CHADEMA kuwa hakuunga mkono shutuma hizo dhidi ya Nape huku akijua wazi kuwa CHADEMA ilibidi wamtumie Marando kuwaeleza watanzania jambo ambalo hata yeye haliamini na kwamba kwa kufanya hivyo kwakuwa Marando ni wakili wa baadhi ya watuhumiwa wa kesi za EPA Watanzania wataamini kwa haraka.

" Je wananchi tuendelee kumwamini Marando na chama chake?" Nape alihoji umati wa wananchi kwenye mkutano huo wakajibu "hawaaminiki hao".

Nape alisema kutokana na kukana alichosema, sasa asimame na kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadangaya kuhusu tuhuma hizo. "Sasa namshauri kwanza atoke kuwaomba radhi watanzania kwa kuwadanganya katika hili na mengine mengi aliyotumiwa na CHADEMA kusema bila kuyaamini kama alivyofanya kwa hilo.

Nape alisema Marando aspoomba radhi Watanzania ataitoa hadharani barua husika ili Watanzania waisome waone unafiki wa Chadema na viongozi wake.

Kuhusu madai ya Chadema kwamba nchi haitatawalika, Nape alisema wanaodai nchi haitawaliki hawana mapenzi wala uchungu na nchi hii, ndo maana kwao hata nchi ikichafuka si tatizo ili mradi wanapata wanachotaka.

Aliwatahadharisha Watanzania kutohangaika na baba wa kambo wakati baba mzazi yupo. Akimaanisha vyama vya upizani ni baba wa kambo na CCM ndio baba mzazi.

Alisema mabadiliko makubwa yanayoendelea ndani ya CCM ndio matarajio ya watanzania kwa kuwa CCM inafahamu kuwa wasipoyapata watayatafuta nje na hapo CCM itakuwa imepoteza haki ya kuongoza nchi, hivyo ni muhimu wana CCM wakawapatia watanzania mabadiliko wanayoyataka.

Katika hatua nyIngine baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, wamedai kwamba haijawahi kutokea mkutano wowote uliofanyika katika miaka ya karibuni mjini Mpanda kupata watu wengi kiasi cha waliohudhuria jana mkutano wa Nape.

"Chadema pia waliwahi kuja hapa juzi juzi, lakini kwa kweli umati huu wa aleo umevunja rekodi, wale hawakupata watu kama hawa" alisema mkazi mmoja wa mji huo, Samel Msakazi.

Naye Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu akizungumza kwenye mkutano huo aliwataka watanzania kutokubali kugawanywa na wanasiasa uchwara wanaotaka kuwatumia kwa malengo yao binafsi,bali waendelee kuienzi amani nchini ambayo imejengwa kwa muda mrefu.

Wajumbe hao wa sekretarite mpya ya CCM watamalizia ziara yao ya siku nne mkoani Rukwa jana asubuhi. (Imeandikwa na Bashiri Nkoromo kutoka Mpanda)
 
Hivi huyu NEPI
Kama hayuko serious vile.
Halafu dogo anajifanya kichwa ngumu
Juzi watu 500 walirudisha kadi za CDM
Alipoingia humu watu walimchambua
Mpaka akakiri kuwa amebugi step
Jana hakuna aliyerudisha kadi za CDM?
Au ndo jana alikuja na gia ya kusema amepata nyaraka za Marando kwenda kwa Jeetu Patel
Dogo akili yake ni finyu sana hajui sanaa na hajui kudanganya watu.
NAOMBA KUJUA JANA WANGAPI WALIRUDISHA KADI ZA CHADEMA?
Najua NAPE umo humu tunaomba umwage hizo nyaraka ulizozikamata hapa sio unatuletea propaganda za kipuuzi.
 
Back
Top Bottom