Napataje bima ya mtoto wa siku tano

Napataje bima ya mtoto wa siku tano

Moneytwister

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
316
Reaction score
1,032
Salaam..

Ndugu zangu nahitaji msaada wenu, je nitapata vipi bima kwaajiri ya mtoto mchanga kwaajiri ya matibabu ambayo anapata muhimbili?

Na kwa wazoefu wa hili, iyo bima ina faida gani linapokuja swala la malipo?

Nishawahi kuuguza mtoto mchanga muhimbili miaka miwili iliyopita gharama zake zilikua kubwa sana nahitaji msaada kuhusu bima nifanye taratibu gani ili kupata na itanisaidia vipi kabla mambo hayajawa magumu tena?

[emoji1666]
 
Nenda kwenye ofisi zao, nasikia Ni tsh. 50,000
 
Nenda na tangazo la kuzaliwa mtoto huko NHIF na utawatajia jina unalotaka kumpa kisha utalipia hiyo 50,400/= hapo utakuwa umeshamkatia bima kabla hajapata cheti cha kuzaliwa.
 
Kwenye kampeni tuliambiwa matibabu ya watoto chini ya miaka mitano ni bure.
We acha tu me nimeuguza mtoto aliyetoka kuzaliwa kwa gharama kubwa pale muhimbili na bado alifariki waligoma kunipa maiti hadi nilipe deni lililobaki [emoji28] na huyu kazaliwa na kesi ile ile kwaiyo naendelea nilipoishia[emoji1]
 
Salaam..

Ndugu zangu nahitaji msaada wenu, je nitapata vipi bima kwaajiri ya mtoto mchanga kwaajiri ya matibabu ambayo anapata muhimbili ?

Kama tayari yupo kwenye matibabu, hii ni ngumu kuipata bima ya 50400 maana hii utaipata baada ya siku 90.
 
Pole kwa changamoto, nenda ofisi ya bima ya afya iliyo karibu nawe kwa msaada zaidi, Bima ya mtoto nasikia ni 50,000 kwa mwaka (japo sina hakika maana hapa katikati kulitokea changes)
Shukran mkuu
 
Jamaa kinipa maelezo apa kwa faida ya wengine ni kwamba kwasisi ambao sio watumishi bima inachukua siku 90 kuanza kupiga kazi iyo haina utaalamu wowote hata mkono wa rafu hauchezi apo [emoji38]
Ndiyo hivyo mzee halafu ukichelewa kufanya malipo ya kazi wanafungia hiyo kadi mpa ulipie na ukilipia ni baada ya siku 90 ndio inafunguliwa na kuuza kufanya kazi
 
Back
Top Bottom