Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Fanya unachoweza ukisema ufuate ushauri,uta felii Mungu ni, wa ajabu sana anajua unashida lakini hata mia huokoti lakini ukiomba mabaya yanakupata Fasta
 
Sasa si ungeogea tu chumvi ya mawe?
Anyway umeyaanza yamalize na inaonekana una mganga mzuri.
Rudi tu kapigwe kinga maana hiyo vita uliyoanzisha si mchezo.
 
Mungu hafikiri km mwanadamu, ni mwingi wa rehema. Narudi kumalizia therapy ya kalmanzila, uzuri doctor hachanji wala hahitaji kafara hata ya njiwa hizo ndo connection hatari kwenye ulimwengu wa roho. Mambo yakiniendea vizuri narudi kwa God kikamilifu huku nikifurahia mafanikio niliyoyapata kwenye shirki. Hapo vipi kiongozi
Huu mchanganyo wa giza na nuru haufai....bora kuwa Moto au baridi na sio vuguvugu.
 
aisee utakufa muda si mrefu au utakuwa chizi. kimbilia kwa Yesu haraka aponye maisha yako. utakuja kunishukuru.tafuta kanisa la watu waliookoka, ukatubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha na uokoke ujiunge ktk safari ya wokovu, ukipuuzia shauri yako.
 
Nilijenga msingi mzuri wa imani yangu kwa Mungu, kuwa ndio anayeweza kunitoa kwenye hili dimbwi la kukosa kipato licha ya kugraduate since 2014 hizi digrii yeboyebo. Japokuwa Mungu alinisaidia kupata kazi za mikataba ya muda mfupi lakini mishahara ni ile ikizidi sana ni laki nne, sehemu nyingi niliambulia laki mbili, mpk laki moja kwa mwezi.

Kutokana na majukumu ya kusomesha mtoto na mama yake, kwangu inakuwa ni ngumu kusogea kimaisha. Hivyo muda mwingi ninakuwa kwenye stress ya kipato kidogo na madeni mengi.

Nilijitahidi kuwa muaminifu kwenye fungu la kumi na sadaka, maombi na kujitoa kwa kiwango kizuri kumtumikia Mungu. Nilitegemea nikifanya hayo angalau nut zitaanza kulegea kwenye uchumi, lakini ndio mambo yakazidi kuwa magumu sana.

Madeni yakaongezeka kwa sababu natakiwa nilipe ada ya mtoto na mama yake(nilimpa mimba dent kuepuka mvua 30 ikabidi nibebe jukumu la kusomesha private school. kwa sasa anamalizia six on May)

Mapema February kuna jamaa akanishauri anipeleke mahali nikaangalie kwa nini nakula msoto hivi licha ya bidii ninayowekeza kutafuta noti. Bibi wa kupiga bao akaniambia shida yangu ni ishu za mila za kwetu na NYOTA yangu imechezewa. Hivyo, nikamilishe mambo ya mila then nitafute fundi wa kusafisha nyota.

Nikapata ushuhuda mahali kuwa kuna fundi mzuri wa hayo mambo, kwa buku mbili tu ana darubini za kuona rohoni mwako. Siku ya kwanza nikaenda nikakuta nyomi, nikafanikiwa kumuona nkaeleza shida akaniambia nina nyota ya kutoa tu, ila ya kupokea, kutunza na nyingine nmesahau zimefungwa. Nikapewa dawa ya kuogea baada ya kurudi nyumbani

Usiku wa siku nliyotoka kwake, nikaota kuna mtu ananifukuza na ananitupia mishale mingi. Nilipambana kuikwepa kwa nguvu zangu ikashindikana lakini nikakumbuka kukemea kwa jina la Yesu mrusha mishale akapotea.

Nikarudi kwa doctor siku ya pili kwenda kufanyiwa huduma kuu yenyewe ya kusafishwa nyota. usiku wake tena baada ya kutoka huko nikaota tena kuna nyoka black ananishambulia kwa kunirushia mate ya sumu, nilipambana kwa nguvu zangu lkn alitaka kunizidi nguvu, nkakumbuka kukemea kwa damu ya Yesu ndio akapotea.

Nilimpigia kalmanzila kumueleza kuhusu hizo ndoto, akaniambia nirudi akanipe kinga...mpaka muda sijarudi tena huko

Matokeo baada ya huduma yake, ni kuwa nimepata kazi japo ni ya muda mfupi lakini ina maslahi mazuri na kuna HR wa shirika moja zuri aminiahidi soon kuna neema inatoka kwenye shirika lao nitakuwa front line kwa sababu ni qualifications zote na experience wanayoihitaji.

Naweza kusema angalau naona mabadiliko kwenye suala la kibali tofauti na mwanzoni


Sasa wanajamvii nauliza, nirudi kwa kalmanzila nikamalizie dozi au nikatubu nimrudie Mungu.
Huyo bibi ni wa ukweli sana,uganga wa ndoto ni mzuri,una maadui wanakushambulia mzee,hata Mimi najipanga ntafute 400,000 nikajiswafi,mandugu wanafiki sana,ndugu ndugu ndio wabaya wetu,kula nao,Cheka nao lakini wanakumaliza kimya kimya
 
Huyo bibi ni wa ukweli sana,uganga wa ndoto ni mzuri,una maadui wanakushambulia mzee,hata Mimi najipanga ntafute 400,000 nikajiswafi,mandugu wanafiki sana,ndugu ndugu ndio wabaya wetu,kula nao,Cheka nao lakini wanakumaliza kimya kimya
vya upande wa giza kuvipata ni haraka lkn vina garama huko mbeleni
 
Back
Top Bottom