Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
...Mh! Pole shemeji. unajua mi nimeoa wilaya ya Nzega kijiji cha Nkiniziwa kwa kweli hali ni mbaya sana ukilinganisha na ilivyotakiwa kuwa. Unajua wakati posa inapelekwa kule kijijini karibia Cresta yangu ibaki huko huko maana lile shimo la kutoka Nzega mpaka ufike kijijini na mvua imepiga sio mchezo lakini ndiyo hivyo dada yako ameninogea hakuna maelezo. nafikiri huu ni ujumbe mzuri kwa wakwe zangu Mzee 6 na Ka****ya wao ndio jua linazama historia itawahukumu kwa kutoinua mkoa wao. Yule anayetembea na kipaja cha kuku kiunoni achana nae wala usitegemee kuna atakachofanya Tabora. Tatizo siku hizi bwana shemeji majimbo yameingiliwa sana kwa hiyo hata hao walioamua kumchagua mnyamwezi mwenzao Igunga ni ufinyu wa kutofikiri tu lakini walitakiwa kufanya mabadiriko kwa kweli mambo ya kushikilia Magamba wanaidodesha wilaya ile. Pole shemeji kaza roho kaza buti safari inaendelea nimeongea na dada yako tutafute hata kakiwanja pale Ipuli tuweke kakibanda tukichoka na vurugu za humu mjini tunasogea kwenda kula embe Tobora!!!!!Haaaahaaaahaaahaaahaa!!!Kwetu Tabora, Mkoa Mkubwa pengine kuliko wote nchi hii ndiko kunakoweza kuwa na watu waliolala kuliko mkoa wowote Tanzania.
Mkoa uliokuwa na shule muhimu kabisa katika nchi hii lakini mkoa uliotoa wasomi wachache ukilinganisha na idadi ya watu wake. Mkoa wenye asali na misitu asili, wenye tumbaku na mbegu ya ku ya iana ya kipekee duniani, moa wenye ng'ombe na mali asili nyingi, mkoa wenye watu warefu waliojaza misuli wake kwa waume lakini sina hakika sana na uwezo wa ubongo wetu.
Tabora isiyokuwa na barabara ya kutufikisha makao makuu ya mkoa kutoka popote pale duniani, mkoa wenye uwanja wa ndege wa matope. mkoa wenye mji wenye mtaa mmoja, mkoa ambao majumba yake yanazidi kwisha na kumongonyoka badala ya kushamiri. Mkoa ambao watu wake wanaogopa kujenga na hat akurudi kwao kwa kuogopa kulogwa.
Mkoa wa Tabora wenye wabunge wasiofanya lolote lakini wanoheshimiwa na kuabudiwa. Mbunge mmoja maarufu sana ana aliwahi kuwa na cheo kikubwa labda kidogo afadhali yeye maana akiendakwao huwanunulia wananchi wake maji madogo ya kilimanjaro, angalau wenye bahati hunywa maji ya kilimanjaro angalau mara moja kwa mwaka.
Hebua angalia wabunge wa bunge lilopita walifanya nini. Hebu Munagalie mnyamwezi yule aliyekuwa Igunga kabla hajajing'atua? Muangalia yule aliyekuwa bosi wa Bunge wamaifanyia nini tabora? Leo wanyamwezi eti wamemchagua mnyamwezi mwenzao muonesha bastola na almanusura nzega nao wamchague mnyamwezi mwezao yule mtoto wa kisomali lakini wakaishia kumchagua mnyamwezi mwenzao mrundi andrea.
Wanyamwezi bado hatujui mkoa wetu unaelekea wapi, hatuna elimu hatuna chochote. Mimi huwa najiuliza hao wanaosema wanyakyusa na wahaya walipata vyeo eti kwa kuwa mikoani kwao kulikuwa na shule kila siku huwa najiuliza kulikuwa na shule ngapi kushinda mkoa wa Tabora? Kagera nimefika na kuishi, Mbeya nimefika na kuishi lakini kila nikiangaza kulinganisha na Tabora sioni.
Inawezekana kumbe siyo uwepo wa shule ndio unaofanya watu waelimike kumbe hata uwezo wa ubongo. Sasa sishangai kuwa kila nikijaribu kufanya jambo sifanikiwi, inawezekana wanyamwezi tuna matatizo ya kurithi katika vichwa vyetu.
Hebu fikiri miaka hamsini kila siku mtu anakuahidi kukujengea lambo la maji na wewe unamkubalia tu eee, eti iko siku atalijenga!