Naona aibu kuzaliwa Mnyamwezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona aibu kuzaliwa Mnyamwezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by domokaya, Oct 3, 2011.

 1. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,120
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Kwetu Tabora, Mkoa Mkubwa pengine kuliko wote nchi hii ndiko kunakoweza kuwa na watu waliolala kuliko mkoa wowote Tanzania.

  Mkoa uliokuwa na shule muhimu kabisa katika nchi hii lakini mkoa uliotoa wasomi wachache ukilinganisha na idadi ya watu wake. Mkoa wenye asali na misitu asili, wenye tumbaku na mbegu ya ku ya iana ya kipekee duniani, moa wenye ng'ombe na mali asili nyingi, mkoa wenye watu warefu waliojaza misuli wake kwa waume lakini sina hakika sana na uwezo wa ubongo wetu.

  Tabora isiyokuwa na barabara ya kutufikisha makao makuu ya mkoa kutoka popote pale duniani, mkoa wenye uwanja wa ndege wa matope. mkoa wenye mji wenye mtaa mmoja, mkoa ambao majumba yake yanazidi kwisha na kumongonyoka badala ya kushamiri. Mkoa ambao watu wake wanaogopa kujenga na hat akurudi kwao kwa kuogopa kulogwa.

  Mkoa wa Tabora wenye wabunge wasiofanya lolote lakini wanoheshimiwa na kuabudiwa. Mbunge mmoja maarufu sana ana aliwahi kuwa na cheo kikubwa labda kidogo afadhali yeye maana akiendakwao huwanunulia wananchi wake maji madogo ya kilimanjaro, angalau wenye bahati hunywa maji ya kilimanjaro angalau mara moja kwa mwaka.

  Hebua angalia wabunge wa bunge lilopita walifanya nini. Hebu Munagalie mnyamwezi yule aliyekuwa Igunga kabla hajajing'atua? Muangalia yule aliyekuwa bosi wa Bunge wamaifanyia nini tabora? Leo wanyamwezi eti wamemchagua mnyamwezi mwenzao muonesha bastola na almanusura nzega nao wamchague mnyamwezi mwezao yule mtoto wa kisomali lakini wakaishia kumchagua mnyamwezi mwenzao mrundi andrea.

  Wanyamwezi bado hatujui mkoa wetu unaelekea wapi, hatuna elimu hatuna chochote. Mimi huwa najiuliza hao wanaosema wanyakyusa na wahaya walipata vyeo eti kwa kuwa mikoani kwao kulikuwa na shule kila siku huwa najiuliza kulikuwa na shule ngapi kushinda mkoa wa Tabora? Kagera nimefika na kuishi, Mbeya nimefika na kuishi lakini kila nikiangaza kulinganisha na Tabora sioni.

  Inawezekana kumbe siyo uwepo wa shule ndio unaofanya watu waelimike kumbe hata uwezo wa ubongo. Sasa sishangai kuwa kila nikijaribu kufanya jambo sifanikiwi, inawezekana wanyamwezi tuna matatizo ya kurithi katika vichwa vyetu.

  Hebu fikiri miaka hamsini kila siku mtu anakuahidi kukujengea lambo la maji na wewe unamkubalia tu eee, eti iko siku atalijenga!
   
 2. Jidulamabambase

  Jidulamabambase Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chief Domokaya pole,
  Mimi kwetu ni Shinyanga lakini hatuko hivyo, leo ninaona aibu sana hata mood ya kazi imetoka, ninaingia kila chumba cha offisi kwa rafiki zangu na ninawauliza hivi kwa nini wana Igunga wamechagua CCM? Nijuavyo mimi hawana sababu hata moja ya kuchagua CCM! Inawezekana wanaridhika na maisha yaliyopo kwa kuwa maisha yao yote yako hivyo na hawajawahi kuwa na maendeleo. Siamini kama hao ni wasukuma waliopitisha hiyo chama tena!
   
 3. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kumbe siyo uwepo wa shule ndio unaofanya watu waelimike kumbe hata uwezo wa ubongo. Sasa sishangai kuwa kila nikijaribu kufanya jambo sifanikiwi, inawezekana wanyamwezi tuna matatizo ya kurithi katika vichwa vyetu.

  Hebu fikiri miaka hamsini kila siku mtu anakuahidi kukujengea lambo la maji na wewe unamkubalia tu eee, eti iko siku atalijenga!

  Pole Domokaya, maana umefika mbali!
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jiue basi!
   
 5. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mie juzi nilikuwa huko msibani! si tu nyumba zinamomonyoka badala ya kushamiri bali pia watu pia wanakwisha kwa ngoma! nimezaliwa Isebya nimekulia na kusoma gongoni yani kila niliyemuulizia keshakwenda mbele ya haki town inazidi kuwa kama kazaroho yani japo nikwetu wiki moja ya mziba nilipata msiba mwingi kwa jinsi hali ilivyo. Hakuna uchumi kabisa watu ni ngono tu wanawaza duh! inabidi turudi tuuokoe mkoa wetu.
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Msula EVE;
  Mbona mie nimetembea sana tu hadi nje ya Tanzania na NINALINGIA KUWA MNYAMWEZI?

  Wee umevuta NSANSA badala ya Bange mkuu.....Siku zote, majani yaliyombali ndiyo huwa ya KIJANI.

  Kuna sababu nyingi zimechangia Tabora kuwa hivyo na si UJINGA wa watu.Jaribu kufuatilia na ujuwe Chief Lugusha wa Sikonge, aliyewahi kuwa Mbunge na alisoma na Nyerere, kwanini alikuwa na kifungo cha Nyumbani pale Sikongee na alikuwa hawezi kufika kwenye mikutano ya watu wengi bila ya kutoa habari Polisi?Fuatilie ujuwe kwa nini Chief Fundikira alikimbilia Kenya kwa miaka mingi?Kwa nini Kasanga Tumbo alikuwa na yeye ana kifungo huko Ipole?Pia kumbuka, Tabora ni mkoa ulioko ndani ya nchi. Ni tofauti na mikoa iliyopo mipakani kama hiyo yote uliyosema. Hebu nipatie Mkoa hata mmoja wa ndani uliochangangamka kutuzidi sisi na wao hawana hata barabara zinazopita kwenda sehemu nyingine.

  Tabora, Singida, Dodoma, Tanga, Lindi, Mtwara, Iringa, Rukwa ni chambio la Mafisadi. Dodoma wanatuzidi tu kwa sababu ni Capital City. Rukwa vimadini kidogo vinasaidia pia Shinyanga vimewapa hadi mwamko. Kigoma ni Rumba tu kama sisi. Tanga, Lindi na Mtwara na ka BAKWATA kanasaidia sana kushusha maendeleo na mwamko ambayo ni sawa kabisa na Tabora. Tena kwa Tabora ni mbaya zaidi maana kuna ka kuabudu ngozi nyeupe sana. Sasa akija Mwarabu, sisi hoi.Si unaona hata mtoto mweupe anaozwa kwa ng'ombe wengi? Kadili Kapeee ni Mwanzo wa matatizo ya Mnyamwezi. Ila siyo sababu ya kukata tamaa na kuanza kujiona wewe hufai. Mbona mie kimaisha nawazidi Wachaga wengi tu. Nawazidi Wahaya wengi tu, Wa-Mbeya pia wengi nawapiga bao, sasa kwa nini nione AIBU kusema mie Mnyamwezi na tena WA SIKONGE?

  Nyanda, lekaka veve......
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Pole sana inaonekana una machungu sana...
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tabora tunapandana sana na kuzaana kama Panya. Acha tupungue kidogo............
   
 9. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umesahau na Issue ya Malima alivyonyotolewa roho!
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Rudia kusoma ulichokiandika!
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  waache walale siku wakiamka watajutia hilo!
   
 12. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,216
  Trophy Points: 280
  Pole,mimi nilitaka kuolewa chabutwa huko sikonge.Nilisemwa mno kwa nini naolewa kwa maskini?nataka kuleta maskini kwenye ukoo?Thank God sikuolewa huko
   
 13. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ujapenda wewe ni hizo mshindo zako tu zilikuwa zinakusumbua labda jamaa alikuwa anajua kukubutua lakini hana kisu!
   
 14. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,369
  Trophy Points: 280
  Yana mwisho, siku inakuja Wadakama wataamka na hutoona aibu tena
   
 15. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  makabila mengine ni kichefuchefu
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu, tafadhali nikumbushe. Malima yupi unayemsema hapa? Samahani ila nimeshindwa kuunganisha dots.

  Wee ndiyo urudie kusoma nilichokiandika.

  Wee sasa ulikuwa uolewe na familia gani? Mbona pale kuna Yongolo Family wapo poa sana kipesa na kishule? Mwisho naona hukupenda. Sijui ningelikuwa mie bado ungeligoma :) Mie pia somehow natoka Chabutwa.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Koma ukomae, Msusa wa Maharage. Mtu hata Laptop huna watumia Mobilephone ila matusi kibao.
   
 18. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Dogo kuna laptop za laki na nusu,, unajua bei ya windowphone wewe?
   
 19. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kaka Mimi ni Mzaliwa wa Tabora, ISEVYA barabara moja inayoitwa KANONI, MNYAMWEZI MKONONGO wa asili. Nachoweza kukueleza ndugu yangu ni kuwa Mkoa wa TABORA UMEROGWA!!!! Hebu tuwaache kwanza wasote hadi hapo watakapopata akili vichwani mwao.
   
 20. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Badakama mmetuaibisha. Mnaotetea fikirieni uduni wa maisha wa wanaigunga! Mara mia hata sisi tulioamua kumpa mzee cheyo na sio magamba. Potelea mbali jimbo letu magamba hayatii miguu.
   
Loading...