Mkuu labda naweza kukubaliana kwenye suala la fast charging tu tena ni kwa simu za high end na mid-range chache zenye hiyo capability, anyway let us take it as it's, suala la memory card kwangu sio hoja maana kuna choice ya iPhone yenye 128GB, 256GB, sasa ukiwa na simu moja kati hizo memory card ya nini!?, pia hasa sisi wabongo tumekuwa na tabia ya kujinunulia tu memory card bila kujali uwezo wa memory card kwenye data ready and write sequential mwisho wa siku unakuta unaathiri performance ya simu bila kujua, kuhusu suala la QHD display ni hujajua kuwa ukubwa wa pixels kwenye simu ni directly proportional na matumizi ya battery, yaani matumizi ya kioo cha QHD na HD kwenye simu zenye display size moja na ukubwa wa battery unaolingana ni tofauti kabisa ingawa processor ina mchango mkubwa pia kwenye matumizi ya battery ndo maana ukichukua iphone ambazo huwa hazizidi 2000mAh na ukichukua Android phone zenye 3000mAh utaona ukaaji wa battery hauna tofauti, simu ikiwa na HD Au FHD display inatosha kabisa hasa kwa hizi simu zenye 4.7', 5' 5.5', QHD zinatakiwa kuelekezwa kwenye TV
Pia ukaaji wa battery unategemea na eco system ya OS. Mfano mzuri nimekupa hapo juu, na ukaaji wa battery unachangiwa na factors nyingi na si kila simu ya android inakaa na battery kwa mda mrefu
Kuhusu camera usitake kuaminisha watu kuwa kila Android phone ina camera nzuri kuliko iphone, mtu anayemtoa jasho Apple kwenye suala la camera ni Samsung akifuatia na LG, kidogo juzi Google kaja kutoa upinzani na simu yake pixel. Lakini bado Apple anatengeneza simu zenye camera nzuri tu tena zenye ushindani wa hali ya juu