Naombeni ushauri wandugu

Embu rekebisha kauli yako daa angel sio ungemtwanga talaka ungeomba talaka na ni hiyari yake akupe au asikupe kama mimi ningekuwa mume wa huyo mdada nisingetoa talaka kwasababu hana udhibitisho kama nimetoka nje ya ndoa hii ndio tabu ya kuoa mwanamke aliekuzid kipato unakuwa hauna sauti kabisa ndani ya nyumba
we unadhani anaposema basi imetosha anasema kwa raha? Anaumia sana hasa akikumbuka alivyomlea huyo mme wake na familia yake km watoto hlf yy anamdharau anaenda kufanya uasherati, KM NINGEKUA MIMI NINGEMTWANGA TALAKA AENDE AKAPUNZIKE KWAO AJIFUNZE JINS YA KUISHI KWA UAMINIFU km atajirekebisha arudi km hawezi asirushe mguu kwangu. UKIMWI UNAUA ACHUKUE TAHADHARI
 
Robby mbona una haira!!??
dada ana uthibitisho wa maandishi yenye tarehe tofauti tangu miaka hiyo na picha za baadhi ya matukio
na nilivyokuja kupost huu uzi mimi ndie mtu wa kwanza kaniita na kuniambia..................
hajawahi hata siku moja kutumia kipato chake kumnyanyasa mumewe i wish ungekua unawafahamu hawa watu! hata baadi ya mambo mie mdogo mtu ndo leo nimeyajua

kwa kweli inauuuuuuuuuuuuuuuma sanaaaaaaaaa
 
Kwanza poleni na msiba wanajamii wenzangu.

Leo nina neno hapa linahitaji msaada wenu maana naona dada yangu naona anataka kutoa maamuzi magumu.
Ameolewa miaka karibia saba iliyopita na amekua akimpenda sana mumewe katika hali zote, Japo mwanaume hana uwezo amekua akimsaidia sana na kulificha hilon hata kuisaidia familia ya mwanaume na yakwake ili kujenga heshma ya mumewe na familia yake kama mwanamke mwenye hekima.
Kipato cha mwanaume ni kidogo sana hawezi hata kulipa ada za watoto achilia mbali chakula cha mwezi mzima ila dada yeye kwake hilo halikua tatizo kwani alkua na imani siku moja watafika wanakotaka,

Sasa hii leo amegundua kwamba mumewe huyo ana do nje ya ndoa kwa sana...... na kati ya wanawake anaoendeleza nao game na ma girlfriends zake wa zamani akiwa na uthibitisho wamekua wakifanya hayo tangu 2005 hadi sasa na uthibitisho anao.

Hana hasira na wala hajachanganyikiwa sana kwa hilo ila anasema tu basi imetosha...., basi imetosha..... basi imetosha........

Wenzangu wazoefu wa haya mambo nisaidieni ushauri gani nimpe? kuvunja ndoa ni kazi kubwa sana lakini kufanya mjinga miaka karibia saba pia inauma mno haswa ukiangalia walikotoka.

Shukrani

Kwa vyovyote utakavyofanya wewe hautokuwa umevunja ndoa! Ndoa kaivunja huyo bwana asiyejua maana ya ndoa ama kujiona kwamba yeye ni mwerevu!! haoneshi kuwa ana shukrani kwa mtindo wa aina yoyote hapo! mkimbize dada yako kupima kisha mwache aamue mwenyewe kipi ni bora katika maisha yake! Usijaribu kumwambia kwamba atoke kwenye ndoa, hilo mwachie mwenyewe. ila angalia pia usimzuie maamuzi yake kwa sababu ukifanya hivyo na kesho akipata ugonjwa unadhani ataanza kumlaumu nani?? Ongea na nduguyo na myakabili kwamba yaliyopo si mazuri nini kifanyike uamuzi ni wake but support her for whatever she decides! Damu ni nzito kuliko maji. mchana mwema
 
asante sana Kitope,
kweli ndoa anaivunja mwenyewe huyo bwana!
hivi ingekua mwanamke ndo kafanya hayo sijui ingekuaje
 
Embu rekebisha kauli yako daa angel sio ungemtwanga talaka ungeomba talaka na ni hiyari yake akupe au asikupe kama mimi ningekuwa mume wa huyo mdada nisingetoa talaka kwasababu hana udhibitisho kama nimetoka nje ya ndoa hii ndio tabu ya kuoa mwanamke aliekuzid kipato unakuwa hauna sauti kabisa ndani ya nyumba

Negative! Sio kweli. wako wengi wamewazidi kipato waume zao na bado wanaishi kama kawaida! Ila midume mingi huwa ikizidiwa kipato basi inakuwa haina amani kichwani!!! hapo ndipo kila linalotamkwa na mke linaonekana ni kwasababu anakipato cha juu kuliko mume!! wangapi wanawake hawana kipato zaidi ya waume zao lakini bado wao ndio wenye sauti na mume anasikiliza!! Hilo nalo mtalipa kisingizio kipi??! Limbwata??!?!?
 
Dah,...
mwambie achukue likizo fupi for sometime aondoke hapo
ili apate mda wa kutafakari vizuri.

Sijui nimshauri nini kwa sasa,akili yangu kama iko likizo hivi toka jana.
 
Kuhusu tatizo la dada yako, ni kweli tutashauri mengi ila yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ila atulize kichwa kabla ya maamuzi.

1. Suala la kuwa yeye ndie ame-support familia kifedha kwa muda mrefu nadhani ni kusaidiana. Ndiyo kama mumewe hakuwa na na uwezo au kipato kidogo, yeye kama mkewe kusaidia ni vyema kwa vile ni wanandoa. Sidhani kama dada yako anatakiwa kuhesabu hili suala kama vile ametumiwa. Yes, inauma sana maana atakuwa anawaza kuwa mumewe alikuwa anatanua nje huku yeye akipiga kichwa kuhakikisha familia inakidhi mahitaji muhimu na mumewe akiwa priority.

2. Mume amecheat, je amewahi kumdhalilisha kwa aina yoyote? kama kumletea mwanamke hapo nyumbani, kupeleka mambo ya nyumbani kwa wanawake wengine au kumfumania? Sasa, ameona alivyoona na ushahidi anao basi mwambie aongee na mumewe na kuweka wazi kuwa anafahamu kila kitu halafu aone reaction ya mumewe. Inauma sana kama alimwamini sana mumewe na kukutana na alivyokutana.

3. Kuachana na mumewe: Hili suala afikirie kwa makini sana. Inaweza ikawa ni solution kwake? ina maana mpaka ana wazo la kuachana na mumewe kuna vitu vingi vimemkera na hawezi kuvumilia. sasa basi, hapo yeye dada ndie muamuzi wa mwisho. Msikilize dada yako, atavyoamua uwe nae bega kwa bega. Asikae na kisirani/mawazo moyoni maana hayo yanaweza kumuumiza zaidi.

Mpe pole na hakika duniani kuna changamoto nyingi ikiwemo za kwenye ndoa.
 
Huyo mwanaume ana tatizo la kisaikolojia. Linatokana na kwamba hatimizi majukumu yake kama mwanamume, badala yake mke ndo anafanya majukumu hayo, hivyo anadhani njia ya kujiona kidume ni ku do mitaani. Mshauri dada yako a take easy, ajifanye kama hajali, najua ni ngumu lakini jamaa akijua kwamba waifu anajua lakini anauchuna tu, atajiona mjinga.
 
Dah,...
mwambie achukue likizo fupi for sometime aondoke hapo
ili apate mda wa kutafakari vizuri.

Sijui nimshauri nini kwa sasa,akili yangu kama iko likizo hivi toka jana.

Kweli mkubwa. huu msiba umefanya hata uwezo wetu wa kufikiri umepungua.
 
asanteni clemmy na belinda

bendewe hilo la kukaa kimya sijui kama linawezekana si unajua maisha hayawezi kwenda kama zamani maana maumivu ni makali kwa kweli
 
AshaDii unaweza kupredict majibu (hypothesis), kama leo tukiafanya research ya kuangalia ni wanandoa wangapi wanaishi kwa sababu wanapenda na wanahitajiana na ni wangapi wanaishi kwa sababu tu wananhitajiana ila hawapendani? Can you predict the proportion? And why?

In Blue; Tunapozungumia wangapi kwa ile idadi ya haraka haraka.... Wanaohitajiana wanashika hatamu kuliko wanaopendana. However Tuko kuna utofauti... Kuna wale ambao wahitajiana, na waheshimiana kua huyo alonae ndio anastahili heshima yake na attention yake yote - to the extent hata mmoja wao itokee ka cheat, ni maybe yupo na mtu ambae sio serious.. thou kuna wengine anakua nyumba ndogo kabisa. Na mara nyingi ndoa ambazo watu wahitajiana kuliko hata kupendana zina uhai mrefu kuliko hata zile ambazo basis ni kupendana. Hivo basi Tuko a six year relationship iko level nyingine kabisa!

In Red; I can not predict the exact proportion because it is not that simple.....

B2T

Sikutaja mume kumhitaji mke wa mama D kama kigezo hasa cha msingi.... Tuko kumbuka kua kuna kuhitaji na kuhitajiana... Hayo mambo inabidi yawe reciprocated katika uhitaji wenyewe for it to work. For instance mume angekua anaprovide 50% ya mahitaji na mke anaprovide the same (hata ikiwa 40%/60%) sio mbaya. In this case yaonesha katika provision mwanaume ategemea more than 75-80% kwa mke.... Mke uhitaji wa mume uko more katika ile mapenzi ya dhati na uwepo wake kama baba na mume.... Hawa watu nature ya kuhitajiana kwao kidogo ni tatizo... Na that is why nikaigusia....
 
ni kweli Angela inauma sana,
asante kwa ushauri

mama D, pole sana kwa yaliyomkuta dada yako. Mimi namshukuru Mungu kwa mambo mengi ambayo nimekutana nayo katika maisha yangu. Kuna siku nilikaa chini nikaamua kufanya reserch kwa nini mambo mengi yanatokea? Ki ukweli wanawake ni vyanzo viikubwa vya wanaume kwenda nje ya ndoa zao at the same time waname ni vyanzo vikubwa kwa wanawake kwenda nje ya ndoa zao.

Je huyo ndugu yako ameshakaa kujiiuliza kwa nini mumewe anafanya hayo yote? Ebu muulize ni lini alikaa na kufanya special Prayers kwa ajili ya mumewe? Hiyo anayosema imetosha mwambie aifute kichwani kwame, badala yake aanze mkakati wa kuangalia kwa nini yote hayo yanatokea. Kuna sehemu anachemka, amekwenda tofauti na maadili.

Angalizo: mwambie ajiandae sana kama anaachana na namewe ahakikishe roho mtakatifu amemshukia ili asiwe na tamaa za kutafuta wanaume wengine siyo rahisi kiasi hicho.

Thats my opinion.
 
Mpe pole sana...kwamba mwanaume kipato chake ni kidogo haimfanyi wala kumlazimisha kuwa mtakatifu au mwaminifu sana.

Uaminifu ni tabia inayokuwepo kutokana na hofu ya Mungu, mapenzi kwa mwenzi wako na familia,kuridhika na yule uliyenaye na kumthamini yeye na familia, na mwisho kujipenda na kujiheshimu wewe mwenyewe.

Pamoja na makosa ya shemeji yako, ni vizuri dada yako akatulia na kuzungumza na mumewe,pengine kutokana na kutokuwa na kipato au kwasababu nyingine ipo sehemu yeye amekosea kama mke, na mumewe akaenda nje ya ndoa...kabla ya maamuzi magumu wazungumze....wakati mwingine sisi wanawake tunakuwa na kiburi, jeuri na dharau, na trust me kuna wanaume wanatafuta tu mwanamke wa kumheshimu alivyo huko nje ya ndoa.

Kumuacha iwe option ya mwisho kabisa, anao uwezo wa kubadilika akiamua huyo mwanaume, na hata kipato wakisaidiana na kushirikiana kinaweza kuwa bora zaidi....Kuachana na mume kuna consequence nyingi kwake na mtoto, asione wepesi katika hili.

All in all, mazungumzo iwe hatua ya kwanza kati yake yeye na mumewe...mwisho wa siku Mungu ampe hekima ya kuamua lililo sahihi.
 
Kwanza naomba umpe pole. Then, si vibaya mkafanya mashauriano pamoja na familia za pande zote mbili. Pia sio mbaya akaulizwa kwenye kikao hicho kama yupo tayari kuacha uchafu wake huo. Na hii itadhihirisha he is sorry kama atakiri huo uchafu wake. Kama amekubali basi my advise will be to give him a second chance. Otherwise he is not worth a lady like your sis.

No problem can be solved from the same consciousness that created it.
 
Pole kwa yaliyomkuta dada yako.
Je wanavyoishi kuna friendship and romantic flow between them?.
labda mme bado anatafuta more romantic relationship na anaipata from previous affairs ambayo kwasasa haipati...

Sorry this is my view
 
kwanza pole sana dada yangu ilakuna jambo moja lazimaulitazame inawezekana katika hili na wewe unahusika kwa mumeo kutoka enje kwa miaka hiyo yote wengi hapa wamelaumu upande mmoja tu lakini katika ndoa kuna mambo mengi yanayo changia inawezekana wakati wewe unatoa hiyo misaada ulijisahau na ukashidwa pengine kumheshemu mumeo ukadhani kutoa pesa ndiyo mapenzi au ulichukulia kwa kuwa hana kipato basi atalazimika kukupenda tu ukiwa wewe ndiyo unatoa kila kitu utanisamehe kama nitakukwaza hapa najaribu kubalance maana wengi tunalaumu upande mmoja tu wakati wanawake wakiwa na pesa kuliko mwanaume zalau huongeka huu ni mtazamo wangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom