Naombeni ushauri tafadhali

Naombeni ushauri tafadhali

wana jamvi mimi ni kijana nina 27 yrs, tatizo langu ni kwamba nilikuwa na girlfriend wangu ambaye tulipendana saana!!
Mpenzi wangu huyu nilikutana naye kipindi nikiwa nahitimu chuo mwaka 2011, sio siri nilimpenda na nilimuona kila kitu kwangu kwa ukweli hata yeye anajua nilimpenda naye pia!
baadhi ya ndugu zangu walimfahamu na pia ndugu zake walinifahamu!!!
kila mmoja wetu alipopata shida tulisaidiana!!! tulikuwa tukitembeleana mara kwa mara kwani yeye alikuwa iringa na mimi dar!!! mwanzoni mwa mwaka Jana nilisafiri kuja mikoa ya kanda ya ziwa!! hivyo tukawa mbali mbali zaidi kuliko ilivyokuwa awali! Tulipanga Dec mwaka Jana tungeenda kutambulishana lakini nikashindwa kwenda kutokana na majukumu niliyonayo huku nilipo! ulizuka ugomvi mkubwa! mpenzi wangu yule alinikatia mawasiliano!
hapo nilijitahidi saana kutafuta suluhu lakini nilishindwa. mwisho ikawa ni january mwishoni mwaka huu akaniambia nitafite mwanamke mwingine! alijaribu kunihesabia yale tuliyotofautiana toka tunaanza mahusiano! nilihuzunika saana toka hapo hapokei simu wala kujibu msg zangu. najihisi kuchanganyikiwa sielewi nifanye nini, nimekata tamaa ya maisha! naomba kama kuna mtu anaweza kunisaidia kisaikolojia ani-pm

Jibu rahisi ni kutafuta mwanamke mwingine bt jaribu kumchunguza tabia na usipende sura utaendelea kulia sana, pia usipende kupitiliza hawa viumbe hawatabiriki, maandiko yanasema" ishinao kwa akili"
 
Yani umempa mwenzio matumaini kuwa ungeenda kujitambulisha halafu umepotelea hewani? si ndo kutiana aibu huko mtu ukute kashawapanga wazazi wajiandae kupokea posa halafu we unaleta story za majukumu. ukimpata mwingne usimuahidi vitu ambavyo huna uwezo wa kuvitimiza!
 
Pole sana najua una wakat mgumu sana,ila zingatia ushauri uliopewa na pia huyo mwanamke hafai tena kwan kwa majibu yake tayari kuna mtu anamgegeda,hivyo kama uko tayar kula ukoko,endelea kulazimisha
 
Acha utoto waza kuongeza kipato chako , tafuta hela kijana tafuta hela , nafasi ya kukaa na kuanza kumuwaza itumie kuwaza mbinu na ujanja wa kuongeza cash ! Its a perfect cure to ur disease believe me ....

"From tz with true luv"
 
naombeni mnielewe ndugu zangu! mnajua hayo mengine ni nature yanakuja automatically, najitahidi kukaa na marafiki, kuwa busy lakini nashindwa kumsahau kila mara namkumbuka

dah! Ndg yangu nataman sana kukupa roho kama yangu! Nikweli mapenz yanaumiza lakin jaribu kuwa na roho au moyo wa uso wa dagaa, kuwa na roho ngumu ya kiume isiyoruhusu mateso ya mapenz..... Mm binafsi yalinikuta kama hayo lakin nashukuru ndio yalionipa juhudi ya kufanya kaz na usiriaz wa mambo yangu kuachwa kulinifanya nifanye juhudi ya maendeleo ili siku moja nikionana na yule aliyenitosa ajutie kwann aliniacha....... Kaka ww ni mtoto wa kiume piga kaz kama utaishi milele lakin ishi kama unakufa kesho.... Ukijikeep busy utamsahau tu. Lenga zaidi kwenye malengo na mafanikio yako..... Utampata anayekupenda na utakuja kufurahia kaka. Fight hard
 
yeah, but najiona nina tatizo la psychology nahitaji mnipe ushauri utakaoniwezesha kukubali hali

Amini kila kitu kinatokea kwasababu, huwezi jua Mungu kakuepusha na nini. Kubaliana kwamba sio wako tena jiweke bize na mambo yako itafika kipindi utaona kawaida tu.
 
yeah, but najiona nina tatizo la psychology nahitaji mnipe ushauri utakaoniwezesha kukubali hali

tunajua mapenzi yanauma vibaya ila at the end yuo HAVE TO MOVE ON
The first step to get over this is to accept it. Just accept that she dumped you.
A year from now, you will look at it and feel nothing. Trust me. I was once in the same situation also

dont feel bad cos you cant force someone to have a relationship with you at least she was honest,
you will go through relationships in life, you will meet someone else i know it dosen't feel like it but you
will at the moment u need to be surrounded by good friends who can cheer u up and have a good laugh.

it just wasnt meant to be, i know it hurts but you WILL meet another lovely girl.
 
Pole sana najua una wakat mgumu sana,ila zingatia ushauri uliopewa na pia huyo mwanamke hafai tena kwan kwa majibu yake tayari kuna mtu anamgegeda,hivyo kama uko tayar kula ukoko,endelea kulazimisha

daaaah mkuu ni kweli lakn inauma kweli!
 
daah sijui unanikejeli au vp?
sipendi hii hali mimi! lakini ni nature! mimi sio wa kwanza watu kibao yamewakuta!!
nipo hapa kuomba msaada wenu! ni kweli nipo katika hali ya kuchanganyikiwa nilitamani hata niende kwa kalumanzila mpnz wangu huyu arudi

Nikukejeli ili iweje?

Anyway' kisicho liziki hakiliki na kama ipo ipo tu its just a matter of time!! Sasa huyo kama ni liziki yako basi huenda hayo ni mapito tu na ipo siku mtaweka mambo sawa!! Kwaupande mwingine kama sio liziki yako basi your westing your time!!

Don't bother about her' time will tell!
Kila lakheri!!!
 
tunajua mapenzi yanauma vibaya ila at the end yuo HAVE TO MOVE ON
The first step to get over this is to accept it. Just accept that she dumped you.
A year from now, you will look at it and feel nothing. Trust me. I was once in the same situation also

dont feel bad cos you cant force someone to have a relationship with you at least she was honest,
you will go through relationships in life, you will meet someone else i know it dosen't feel like it but you
will at the moment u need to be surrounded by good friends who can cheer u up and have a good laugh.

it just wasnt meant to be, i know it hurts but you WILL meet another lovely girl.

thanks
 
Back
Top Bottom