Naombeni ushauri: Rafiki yangu amehamia kwangu na mabegi

Asitegemee fadhila kwamba mwamba akitoboa basi anaweza kumpiga tafu baadae hilo sahau.. washkaji wengi ni masnich wkt wakiwa na shida vichwa vinakuwa chini akitoboa mabega yanakuwa juu na kusahau waliowasaidia....

Uamuzi ni wako akidha asepe au abaki.
 
Mtu unaweza muona rafiki yako kumbe siyo, anajua huna mishe lakini ataamka kanuna bila sababu
 
Umesema ni rafiki yako! Then nashauri ongea nae mueleze ukweli kwamba huna nafasi.
 
Maisha ni fumbo kubwa sana hakuna ajuaye kesho yake na kamww kwwnye maisha usimdharau mtu kila jambo hutokea kwa sababu ..... ngoja nikupe ushuhuda wangu wa kweli kipindi na kuja dar nlifikia kwa mshkaji wangu flani maeneo ya keko sikuwa na kazi inshort sikiwa na mbele wala nyuma mshkaji alinivumilia kwa mda kuna wakati tililala njaa ngoja ni fupishe maisha yaliendelea kibishi ... nikajaga kupata kazi mahali tangu sikuile mambo yakawa tofauti .... alikuja kufukuzwa kazi kodi nikawa na lipia mmi ....... nikaja kumunganisha kwwnye kampuni mjoa ya kichina Leo kila mtu ana maisha yake na tuna wasiliana ........ KATI YETU HAKUNA AJUAYE KESHO .....LEO UTA MKAZIA LAKINI KESHI NDO ATAKAYE KUSAIDIA ...
 
Kuna mawili .
1. Usimfukuze akae hata mwezi
2. Muulize mipango yake hadi lini atasepa au nini kinaendelea .
3. Muulize kuhusu huyo mjomba wake
4. Kwa maisha haya huwezi jinsia moja kuishi pamoja huna raha yaani .
5. Maisha yakutegemeana ni mbaya sana.
6. Nani mwenye ufunguo na ameenda wapi na ni either ni usiku au mchana, na hayupo karibu unapiga simu hadi unazima . Sipendagi ni kero sana
 
Usimfukuze, mshirikishe kwenye mishe za kutafuta hela ili mtafute wote. Siku atakapotengamaa kiuchumi atatafuta chumba chake. Hii ndio maana halisi ya UPENDO na MAISHA
 
Mkuu usikurupuke kumfukuza au hata kumwonesha vitendo vya wazi kuwa hupendi uwepo wake, jipe muda endelea na mishe zako tu kwani ye sio mtoto mdogo useme utamwachia nani.
 
Mtoa post nafikiri ushauli huu unakufaa huwezi jua kesho yako au yake Mungu ni mwema kwa waja wake.
 
Pole umenikumbusha mbali.
Nilimkaribisha rafiki yangu kwangu,aliomba akae wiki mbili tu ila alikaa zaidi ya miezi mitatu.
Changamoto kubwa ilikua aina ya maisha yetu ni tofauti kabisa,
Nikaamua kuondoka na kumuachia chumba.
Ni vyema uongee nae kwanza,muelewane pamoja na urafiki ila atambue apo ni kwako.
Ukikaa nae ndipo utamjua ni mti wa aina gani.
 
sijakataa lakini angetumia ustaarab
 
Mm wala sio mnafiki,toka nimeanza kuishi gheto nimeishi na washkaji kibao mpaka nimekuja kuoa na wengine mpaka leo mazaga yako kama zipo kwangu,sijawahi kuishi pekee yangu gheto toka nimeanza kujitegemea
ukweli wangu ningemuuliza ana mpango wa kukaa muda gan halaf kuna ule urafiki unajua huyu mwana huwez mtupa kuna wale wa ku pass by aje anikere sasa mimi nasemea huyu wapili wa kupita,aje anikere bure? kwa nn tuje kukerana kama anakaa wiki wiki mbili its okay shida iwe ni gea ya kuingilia azidishe miez ubaya aanze kua sio wa kujiongeza ukirudi unakuta na boxer zako zimevaliwa
 

Mtafutie chumba cha Giza ni elfu 30, lipia miezi mitatu. Nunulia Godoro na shuka kule tandale. Nunua unga na dagaa, sufuria na sahani. Na jiko la Mkaa la elfu tatu.
Jumla 300k mpe elfu 50.
Kisha mwambie kila la kheri
 
Kulikuwa na maana gani ya kutumia neno rafiki yangu,at the same time unalalamika acha ubinafsi-sasa kama MTU ni rafiki yako unashindwaje kumpa hifadhi.
 
Mtafutie chumba cha Giza ni elfu 30, lipia miezi mitatu. Nunulia Godoro na shuka kule tandale. Nunua unga na dagaa, sufuria na sahani. Na jiko la Mkaa la elfu tatu.
Jumla 300k mpe elfu 50.
Kisha mwambie kila la kheri
unahisi huyu mtoa mada anazo hizo hela?? kumbe watu wa jf ni matajiri hivi
 
Wewe mwenyewe hauna kazi umesema umemaliza chuo, halafu hali ya mwenzako unaisema kuwa naye yeye ni jobless....

Mkuu urafiki wenu wa chuo ulikuwa wa namna gani tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…