Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Hili la sadaka nitalifanyia kazi, Japo hujasema, imeona mabadiliko yoyote baada ya kuanza kutoa sadaka?

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Kuna kipindi chaa kushuka, unapigika mpaka laki unaipata kwa manati, ukivuka hapo utatoboa mazima. Hizi ni ups and down za maisha na hata ukiroga kuondoa mikosi utapata nafuu ya mda kisha unarudi mle mle so vumilia uvuke hicho, kipindi kesho ni nzuri
Ni kweli mkuu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona kama una makasiriko?
 
Ushauri ni acha tamaa ya mafanikio ya haraka. Acha tamaa na kiraluralu cha kutaka kuwaoneshea watu umefanikiwa.
 
Ushauri wangu nenda kwa Mwamposa umerogwa ndg yangu.
 
Hili la sadaka nitalifanyia kazi, Japo hujasema, imeona mabadiliko yoyote baada ya kuanza kutoa sadaka?

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Mkuu nakupa short story nimepitia mtihani mkubwa sana, hela kwangu na furaha tokea udogoni ndio maisha yangu.
Sasa kulitokea mambo flani ya kifamilia, sikutegemea maishani kama yangetokea. Nilipitia magumu sana sana furaha na hela ilipotea, mzee wangu akanambia mwanangu sadaka ni kinga ya mabaya.

Toa sadaka na muombe Mungu akulinde na akufanyie wepesi mambo yako. Mkuu hapa nilipo furaha ninayo tena sana tu hela inakuja kidogo dogo sio kama mwanzo.
Lakini najua kutokana na uchumi ulivyo ndio maana, ukichanganya najua nitafanya makubwa kuliko mwanzo. Ushauri wangu kwako toa sadaka unapo toa sema nia yako ya kutoa sadaka hio.
 
Asante sana mkuu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Hili la sadaka nitalifanyia kazi, Japo hujasema, imeona mabadiliko yoyote baada ya kuanza kutoa sadaka?

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Eneo hilo la sadaka ni MUHIMU sana mkuu usidharau wala usisahau hapo ndipo baraka zako zilipo mkuu haiwezekani uwe na mtaji wa 30ml nk. Afu usitoe sadaka mkuu ni kosa kubwa sana unajua matajiri wengi wanatoa sana sadaka ndio mafanikio yao hukua zaidi.
 
Sijaelewa mkuu, nieleweshe zaidi, nipo tayari kukusikiliza

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Maoni yangu madogo
Biashara ya nafaka ni biashara nzuri sana ukiwa na mtaji mkubwa kama huo wako unapata urahisi wa kuzungusha
Nina uzoefu na mchele
Unaweza kununua mpunga ukaja kukoboa na kuuza mchele au unaweza tu kununua na mchele na kuuza
Soma soko la eneo ulilopo wanakula zaidi mchele gani bei zao utapata pa kuanzia
Kwa kipindi hiki mchele ipo ni fursa ukiwa na mtaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…