Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Pole sana. Hapa naona kuna bad planning with a combination of unfortunate events camouflaged in wrong believes! Mchawi wako ni mawazo yako mwenyewe. Hujalogwa lolote ila imani yako ndiyo imekuloga. Siku zote binadamu akikwama kimaisha jambo la kwanza kufanya ni kukimbilia kuangalia kitu kilichomkwamisha nje ya nafsi (utendaji) wake. Hapa ndipo kosa huanza kuzaa makosa, na makosa yanazaa makosa zaidi na zaidi. Kwa mfano wewe umeshaona kuwa masahibu yako ni kwa sababu ya kulogwa. Hili litakufanya uendelee kufanya makosa kwa kila kitu utakachoamua kukifanya kwa sababu hujataka kukubali kuwa wewe ndiyo chanzo cha kukwama ili ujirekebishe.
 
Sawa mkuu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Unaposema akiba akiba unayoweka huioni kwamba inavapour au??
Yaani umeweka pesa mpesa, tigo pesa au benki, mwisho wa siku huikuti??

Kwenye kuku usimamizi wako ukoje, kwa mimi nadhani hakuna uchawi ni vile tu kipindi uko job hukuona mapungufu kwakua mshahara ulikuweka mjini na faida ya hiyo miradi hukuihitaji sana kama unavyoihitaji sasa.
 
ni ngumu kuelewa kama hayajakukuta

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Nakushauri kimbilia kwa mwamposa haraka sana ukapate mafuta na maji
 
Sitaki niseme yalionifika lakini miaka 3 nyuma nimekutana na mambo mengi tu. Hasa kwenye kipato na biashara imeyumba sanaa. Nilichofanya kila nikipata hela natoa sadaka kwa mwezi naweza toa sadaka hata ya 100,000. Mwenyezi Mungu anapokupa neema yake, nawe toa sadaka kwa ajili yake.
 
Kuna kipindi chaa kushuka, unapigika mpaka laki unaipata kwa manati, ukivuka hapo utatoboa mazima. Hizi ni ups and down za maisha na hata ukiroga kuondoa mikosi utapata nafuu ya mda kisha unarudi mle mle so vumilia uvuke hicho, kipindi kesho ni nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…