Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Kuna siku nilienda semina wkt natafuta sehemu ya kulala ghafla nakutana na shemu wangu anatoka room teena mkoa ule ule nilipo ndiyo anaishi.

Akaanza kuniomba niwe mvumilivu guess what nilimwambia hapa tupo unyagoni/ jandoni hayatokagi ya kule poa moto ndugu yangu.
Daah ananiheshomu sana mpk kesho ila siri tunayo sisi wawili hivyo.
 
Tafuta namna ya kumwambia uokoe roho yake, uokoe mwili wake,uokoe maisha yake.
Maradhi ni mengi mno, ukimwi umetapakaa mno ni maumivu sana kusalitiwa, tafuta namna ya kumuokoa iwe tu indirect way hata direct way ikibidi, tulipofikia hakuna aliye salama ukimwi hauchagui.
Brother wangu aliambiwa sana mkewe anasaliti, hakuamini na akapuuza lakini leo hii na mke wote ni HIV+...inaumiza sana.
Sijaoa lakini huwa nawaambia rafiki zangu ikitokea umemuona mchumba yupo na mtu niambie, ili uokoe maisha yangu palipofikia tusioneane aibu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
hamishia huo ushahidi kwenye flash ,au tuma videos kwangu , nipe na address ya jamaa .ntazi-duplicate hizo flash ziwe 4 ,moja kwa rafiki ako , moja kwa huyo mke wake ,moja kwa mama akw na jamaa moja kwa ndugu wa mwanamke......baada ya apo kesi kwishaa ...njoo PM chapu

vigezo na masharti kuzingattiwa
Kama unaushahidi..nunua flashi..rekodi..mtume mtu asiemjua..ampe..alafu kaa kimya. Akiona yeye..ataaamua lililo sahihi..na wewe hutakuwa na lawama. Na hapo untakuwa umeiweka huru nafsi yako kuliko uivyo sasa.
 
Habari Wana jamvi,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Nina rafiki yangu ambaye ni Kama ndugu yangu kwa jinsi tunavyoishi na kusaidiana once changamoto za kimaisha zinapo arise.
Hamishia huo ushahidi kwenye flash ,au tuma videos kwangu , nipe na address ya jamaa .ntazi-duplicate hizo flash ziwe 4 ,moja kwa rafiki ako , moja kwa huyo mke wake ,moja kwa mama akw na jamaa moja kwa ndugu wa mwanamke......baada ya apo kesi kwishaa ...njoo PM chapu

vigezo na masharti kuzingattiwa
 
Habari Wana jamvi,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.
Hilo kundi la WhatsApp linaongelea aje masuala ya ndoa? Linahamasisha kuchepuka au kugeshimu ndoa au ni changamoto za ndoa?
Picha ya shemeji na video, ni kabla au baada ya ndoa na rafiki yako?

Ukweli utawaweka wote huru, kama imetokea umejua udhalimu unaoendelea, uweke wazi, Sidhani kama rafiki yako hatakuelewa nia yako ya dhati ya kumnusuru na majanga ya mkewe.
 
Hofu yangu ipo kwenye mapokeo ya jamaa maamuzi magumu yeyote yakitokea Mimi siwezi kuwa chanzo?
Chanzo ni mkewe, sio wewe! Mambo ya mapenzi, unaweza kweli ikakurudia wewe, ila baada ya muda wa kutulia, atavuna kujua wewe sio chanzo, bali mkewe.
 
Broo kabisa ukashindwa kumwambia ukamficha malaya
Maamuzi aliofanya ni sahihi kuliko kumwambia huyo bro! Angeishilia kuonekana mchawi tu 😅 the best decision ni aheri angemuita ashuhudie mwenyewe anakotoka mkewe
 
Hofu yangu ipo kwenye mapokeo ya jamaa maamuzi magumu yeyote yakitokea Mimi siwezi kuwa chanzo?
Kwanini usiwe chanzo wakati umepeleka umbeya! Cha kufanya mpe admin namba ya rafiki yako halafu amu add kwenye hilo group kimya kimya😅
 
Kuna jamaa walikuwa wanajua ya kwamba shemeji yao anamegwa na njemba fulani kutokana na urafiki wao wakawa wanumia sana wakamwambia muhusika na wakandaa mtego, cku ya cku muhusika akapigiwa cm mkeo agawa uroda njoo ushuhudie huku jamaa akafika chap kwa haraka, wakamwambia subili hapa maana wameingia gest, wakasubili muda wakawaona wanatoka huku wamekumbatia basi kwa kuwa ilikuwa ucku jamaa akawa anawafuatilia kwa nyuma bila wao kujua, kufika mbele wakasimama wakiongea mwanamke akasema ngoja nimuwai huyu bwege atakuwa amesharudi jamaa kusikia vile uzalendo ukamshinda akamchoma kisu mwanamme na kufa pale pale, mwisho mwanamme amefunga mgoni amekufa mwanamke ameolewa tena hukoooooooooooooooooooooooooo, marafiki wanajuta kwa walichokifanya.
Jamaa alikuwa na maamuzi ya hasira sana😅 dah haya maisha haya
 
Aisee ulifanya jambo la busara mkuu, japo inauma yaani unashuhudia Kaka yako akisalitiwa😪, ila sasa ukifikiria consequences baada ya kumwambia mmh, labda tu siku ungemchana huyo shemeji kwamba siku ile hukupenda alichokifanya na asirudie otherwise utamwambia Bro nadhani angeogopa na asingerudia.
Shemeji angekupa tunda ili ukaushe😅
 
Kafungue hata account fake umtumie ujumbe Facebook na number za huyo mtu umwambie afatilie huyo mwanamke. Ila huyo mwanamke kanisikitisha jinsi mumewe anavojitoa kwake then ana msaliti, si ajabu na watoto ni wamuchepuko
Kwa hizo hasara, machozi, jasho na damu jamaa akisikia huo upuuzi huyo mwanamke hawezi endelea kupumua ndani ya masaa 24 yajayo 😅😂😅
 
Kwa hizo hasara, machozi, jasho na damu jamaa akisikia huo upuuzi huyo mwanamke hawezi endelea kupumua ndani ya masaa 24 yajayo
Mwanamke mjinga huyu, jamani to jifunze kuheshimu wanaotujali kwenye shida na raha na kuepuka kuwaumiza maana tunawafanya waje kuwa katili
 
Habari Wana jamvi,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Nina rafiki yangu ambaye ni Kama ndugu yangu kwa jinsi tunavyoishi na kusaidiana once changamoto za kimaisha zinapo arise.

Nimeishi vizuri Sana na huyu rafiki yangu tena kwa ukaribu Sana tukiwa mtaa mmoja. lakini kwa Sasa tupo mbali kwa maana ya distance lakini urafiki wetu bado upo na unakua siku Hadi siku.

Huyo rafiki yangu ni mtumishi wa taasisi Y wakati mke wake naye ni mtumishi wa taasisi W (mwanamke ni mtu wa kusafiri Mara kwa Mara kwa nature ya kazi yao).

Sasa week chache zilizopita nikiwa kwenye Moja ya group la WhatsApp linalodeal na ndoa.

Ghafla nikaona picha ya Shemeji yangu akiwa huged na jamaa Fulani imetumwa kwenye group na jamaa.

Kwa Sababu namfaham nilishtuka Sana nikafuatilia vizuri nani ametuma Ile picha, nikapata kumfaham. nikiwa najiuliza maswali na kutafakari.

Moja ya member katika hilo group aliuliza kwa kumtag mtu aliyetuma Ile picha,,, Boss huyo mwanamke ni mkali Sana ni wa wawapi...?

Jamaa akajibu ni wa mkoa X, alipo taja mkoa kwangu maumivu makali Sana yalikuwa upande wangu as if Mimi ndiye nasaritiwa.

Why niliumia Sasa Mimi wakati sio mke wangu amefanya hivyo?

Kama nilivyosema awali mume wa huyo mwanamke ni rafiki yangu Sana na tumepitia mengi Sana pamoja so ni Kama ndugu yangu tu kwa Sasa.

Huyo Shemeji kabla ya kuwa na rafiki yangu alikuwa na mahusiano na jamaa mmoja ambaye alikuwa na kesi. Yule jamaa akamkopa mwanamke pesa akimuahidi atamrudishia kumbe dhamira yake ni kumtapeli mwanamke na kweli mwanamke alikopa pesa kwenye Vikoba na akachukua mkopo benk then akampa jamaa apeleke kwenye kesi aliyokuwa anakabiliwa nayo.

Kumbe jamaa alifake na kutengeneza matukio ili apate pesa Wala hakukuwepo na kesi halisia Bali ilikuwa ni mipango iliyofanywa na Wakili asiyekuwa mwaminifu.

Basi mgogoro mkubwa ukaibuka mpaka mahusiano yakavunjika.

Ndipo huyo mwanamke akaanza mahusiano na rafiki yangu, kwa Sababu rafiki yangu ni ndugu yangu the way tulivyishi akamtambulisha kwangu yule mwanamke then maisha yakaendelee.

Ila kabla hatujua kuwa mwanamke alikotoka alikuwa na mzigo wa mikopo.

Kuna siku nilimuuliza rafiki yangu unaijua background ya huyo mwanamke ? Akasema hapana hakujua nilimshauri afuatilie kweli anagundua kuwa mwanamke yupo single kwa siku 25.

Hiyo taarifa ilinishtua kidogo na kunipa maswali inawezekanaje mwanamke aliyeumizwa Sana hajapata muda wa kutafakari anaanzisha mahusiano mapya ndani ya muda mfupi hivyo?

Seriously nilihisi hapo Kuna kitu zaidi kinatafutwa sio upendo, nikutaka kumhoji Sana rafiki yangu nilimwambia tu awe makini sana, Basi maisha yakaendelea Kama kawaida.

Miezi kadhaa badaye nikaona rafiki yangu anahangaika Sana kutafuta pesa ikionyesha ana uhitaji mkubwa Sana wa pesa isivyo kawaida yake.

Kama tujuavyo ukitaka kumjua mtu kaa karibu naye so kwa ukaribu niliokuwa nao kwa rafiki yangu niligundua jamaa ana matatizo.

Nikaomba kuongea naye bila hiana akafunguka yote A to Z kuhusu Shemeji na mikopo aliyochukua benk na kwenye vikobo ilikuwa mikopo iliyokuwa kiasi kwamba mshahara wote ulikuwa unakatwa huko huko, huku wa Vikoba nao wakiwa wanamsumbua sana.

Basi nikaingiwa na hurumu Sana kumuona rafiki yangu anateseka vile Kuna kiendo tulinunua eneo la pamoja kwa lengo la kujenga fremu za biashara Kisha tugawane fremu.

Rafiki yangu akaniomba kuuze ili ipatikane pesa ya haraka kuclear mikopo ya Shemeji.
nampenda Sana rafiki yangu, nilikubali kufanya hivyo.

Tukauza tukaclear mikopo yote ya Shemeji maisha yakaendelee.

Mimi nikapata Safari ya kikazi kwenda nje ya Tz. Wakati nasafiri rafiki yangu alikuwa kwenye process za mwisho kabsa za kumuoa huyo Shemeji yangu.

MUNGU saidia kweli alifanikisha na Mambo yalienda vizuri kabisa thou niliumia kutohudhuria harusi ya rafiki yangu lakini sikuwa na namna majukumu ya kazi yalinibana Sana.

Yapata miaka miwili Sasa sijaonana live na rafiki yangu japo tunawasiliana vizuri na Kama Kuna changamoto tunashirikishana ingawa Kuna mazingira nakuwa nipo mawasiliano yanakuwa hamna kabisa mwezi mzima au zaidi.

Mpaka hapa mtakuwa mmeelewa kwanini naumia Sana kuona huo usariti.

Sasa turudi kwenye group la WhatsApp,

Baada ya kuona Ile picha ya mke wa rafiki yangu nikataka evidence juu ya lile Jambo, kweli nilipata evidence zote zikiwemo videos.

Kumbe Mwanamke anamuaga Mwanume kuwa waenda kikazi kwenye mkoa huo lakini kumbe anaenda kwa mwanaume mwingine(mchepuko).

Kusema kweli tangu nione usariti ule nimejikuta sipo sawa kabisa naumia Sana maana rafiki yangu amehangaika Sana na kuhairisha Mambo yake mengi ili tu kuweza kumsaidia mwanamke pamoja na familia ya mwanamke.

Hapa napambana na nafsi mbili

Moja inaniambia nimwambie rafiki yangu ....na nafsi nyingine inasema nisimwambie ...

Tafadhali naombeni ushauri wenu wana jamvi nifanye nini nampenda Sana rafiki yangu

Nakuja kwenu kupata ushauri mpana zaidi.
Hapa ni kumwambia tu rafiki yako ukweli mapema ili asije pata maradhi. Kuna wanawake wengine ni mizimu/majini kisirani haipaswi kuolewa hata kidogo.
 
Mwanamke mjinga huyu, jamani to jifunze kuheshimu wanaotujali kwenye shida na raha na kuepuka kuwaumiza maana tunawafanya waje kuwa katili
Umeongea point, huyu dada yenu anawatia doa wanawake wote na kuonekana kama Kajala na mwanaye asiyependa shule.
 
Back
Top Bottom