Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,003
2,000
Binafsi huwa naona SI SAWA KUMWAMBIA MWENZA BAADA YA KUMFUMA MWINGINE.. Kama kweli unataka kujenga, mwambie huyu shemeji yako kuwa anayoyafanya siyo, na aache Mara moj...!! Najua huyo shemeji anaweza kukusingizia jambo kwa jamaa, wewe tunza ushahidi...!! Hasa kwamba unamtaka kimapenzi

Ila kwa upande mwingine, jiandae kuvunja urafiki wenu.
Chukuwa ushauri huu.
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,833
2,000
Mmh usije ukawa chanzo cha ugomvi wao mkuu , ingekua mimi ningekausha tu.
Kabisa ni kuchuna tu,atakuja kujua mwenyewe ,
Nilimfumania mke wa bro live kabisa anapapaswa na njemba buguruni huko.
Nimeshuka kituoni pale sokoni kuna bar na lodge pembeni.
Nikaona ngoja nikapige supu humo,
Hamad shemu huyu hapa tena anapapaswa kabisa kakumbatiwa anachekacheka tu.
Aliponiona alishtuka sana,kama aje anisalimie,
Nilipita nikatokea mlango mwingine huyo nikatimka.
Nilishika cm km mara 3 nimpigie bro
Badae nikaona achana nao hao wameoana na wana mtoto mdogo.
Sikuwai kumwambia bro mpk anakufa.
Maana nae namjua,angembatua mtu leo yuko jela.
 

Cole Williams

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
34,163
2,000
uphaller mwingine,

kosa la kwanza mwanamke kaisaliti ndoa yake, kosa lingine kubwa zaidi ni kwenda kumsaliti mumewe kwa takataka moja isiyojielewa inayopost picha za ushahidi pamoja na video kwenye group, huku ikijua kabisa huyo ni mke wa mtu (hata ingekuwa hajaolewa bado siyo busara)..!

Watakushauri wenye busara zao mingi, me nimemaindi tu vile hao wachepukaji wote ile namna hawajielewi, mtseeeuuw' zao...!
Kwahiyo bora kimya kimya eti eeeh?
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
1,538
2,000
Unajua ndgu zangu kuna namna mnazoeana na rafiki yako.
Ndio hapa wadau wengine wanasema mwambie wengine wanasema kausha iyo ni vile wao wanawachukilia rafiki zao wao na sio urafiki wako na jamaa.
Je kwenye upande wa mahusiano wewe na rafiki yako mko vipi??,Huwa mnashirikiana au ni kibiashara na mambo mengine tu??

Mzebaba akili kumkichwa mapenzi kushaurika huwa ni kazi sana hasa kwa mtu aliewekeza kama rafiki yako.
Mi ushauri wangu kwako ni kumwambia tu jamaa amchunguze mke wake basi , izo info nyingine atafute mwenyewe.

Ama lah kama vipi unaweza kuweka rehani urafiki wenu, ukimpasukia iyo ishu basi jua urafiki uko mashakani.
 

kagwima

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
794
1,000
Kwa uandishi huu si ajabu ni ww maana umeandika kwa uchungu saana
Na huyo mke ni wako unashindwa ufanye nn
huna uwezo wa kuachana na huyo mwanamke japo evidence zipo za kutosha
 

mweusi asili

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
1,139
2,000
Hiyo mwanamke sijui shemeji yako yuko desperate Sana alafu either ni Malaya au hana mapenzi na mskaji wako pia huyo mskaji wako naye zuzu anapenda kiboya lakini na wewe inaonekana unamtaka huyo demu ndio maana unamfuatilia so kikawaida ushauri wa mahusiano ya kimapenzi ni utata Cha msingi angalia wao wanamsimamo gani Kama wanafuraha na maisha yao achana nao utaonekana mnoko
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
11,001
2,000
Kabisa ni kuchuna tu,atakuja kujua mwenyewe ,
Nilimfumania mke wa bro live kabisa anapapaswa na njemba buguruni huko.
Nimeshuka kituoni pale sokoni kuna bar na lodge pembeni.
Nikaona ngoja nikapige supu humo,
Hamad shemu huyu hapa tena anapapaswa kabisa kakumbatiwa anachekacheka tu.
Aliponiona alishtuka sana,kama aje anisalimie,
Nilipita nikatokea mlango mwingine huyo nikatimka.
Nilishika cm km mara 3 nimpigie bro
Badae nikaona achana nao hao wameoana na wana mtoto mdogo.
Sikuwai kumwambia bro mpk anakufa.
Maana nae namjua,angembatua mtu leo yuko jela.
Aisee ulifanya jambo la busara mkuu, japo inauma yaani unashuhudia Kaka yako akisalitiwa😪, ila sasa ukifikiria consequences baada ya kumwambia mmh, labda tu siku ungemchana huyo shemeji kwamba siku ile hukupenda alichokifanya na asirudie otherwise utamwambia Bro nadhani angeogopa na asingerudia.
 

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,815
2,000
Nini mkuu, je ukisema afu hasira zake akamuua huyo mwanamke utajisikiaje wewe uliyepeleka taarifa, je ukisema then kwa mshtuko huyo mume akapata presha na maradhi ya moyo, je ukisema asipokuamini wewe akahisi ni mchonganishi tu huoni itakua mwisho wa urafiki wenu?
Na je ukikaa kimya rafiki yako aje afe na ukimwi utakuwa umemsaidia?
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
11,001
2,000
Na je ukikaa kimya rafiki yako aje afe na ukimwi utakuwa umemsaidia?
Dah sawa ila labda umwambie indirectly amchunguze mkewe ila si kumwambia nimeona picha na videos mkeo anakusaliti, ama umface huyo mwanamke umwambie umeuona huo upuuzi anaoufanya na muoneshe na hizo picha then mchimbe mkwara kwamba unampelekea mumewe aone. Hapo ataogopa na atajirekebisha
 

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,815
2,000
Dah sawa ila labda umwambie indirectly amchunguze mkewe ila si kumwambia nimeona picha na videos mkeo anakusaliti, ama umface huyo mwanamke umwambie umeuona huo upuuzi anaoufanya na muoneshe na hizo picha then mchimbe mkwara kwamba unampelekea mumewe aone. Hapo ataogopa na atajirekebisha
Yeah at least ufanye kitu kuliko kujifanya rafik afu unamficha rafik yako jambo kama hilo. Mimi kama mimi ningependa rafik yangu aniambie tu direct ntamthamin sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom