Naombeni ushauri ndugu zangu, seriously kabisa. Kuna sauti kila siku haiishi kuniambia kuwa mke niliye nae sio!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Ni mwaka wa 3 nipo na huyu mke na mtoto mmoja tayari; sijawahi kukamata sms ya ajabu wala kumkamata au kupata taarifa za kuchepuka kwake (labda watu wananiheshimu na hivyo hunistahi kwa kutoniambia), lakini pamoja na hayo nafsi yangu, katika kipindi chote, haiachi kuniambia kuwa hapa siyo sehemu sahihi.....nimepotea.

Kila nikijaribu kuipotezea sauti hii huwa inajiongeza hadi kufikia kuniamsha usingizini wakati mwingine.

Tuna viutofauti kadhaa, ndiyo, lakini mimi mwenyewe sijawahi kuvifanya kuwa hoja sana (kuvifikiria kupitiliza kiasi cha kupata hisia hizi hasi.....naona ni vitu vya kurekebishika vikidanyiwa kazi ipasavyo). Baadhi ya viutofauti gtetu ni hv hapa;

1. Kupenda kuvaa madera (mi si mfuasi wa madera),

2. Kulalamika lalamika ( sipendi makelele makelele miki),

3. Kuzoeana sana na mama yake,

4. Majibu ya jazba yanayopelekea ugomvi kati yetu,

5. Uchapakazi hafifu (si mwenye kuweza kulima ipasavyo),

6. Ucheshi unaompelekea kuzoeleka kirahisi (hii changamoto nayo wakati mwingine).

Uamuzi bora ni upi hapa wa kuchukua wadau?!!!

Sauti inaongezeka siku baada ya siku na hali ndo kama hivyo.
 
Back
Top Bottom