Naombeni ushauri ndugu zangu,rafiki zangu

Naombeni ushauri ndugu zangu,rafiki zangu

Nimeishi nae kama mume na mke uyu binti kwa miaka minne sasa,elimu yake ni kidato cha nne ivyo hakubahatika kuendelea na shule,ni mama wa nyumbani

Mimi nimebahatika kidogo nna kadegree japo kamoja na kakazi ka kujishikiza kidogo

Ndani ya miaka minne tumebahatika kununua gar na kujenga kabanda japo kadogo

Baada ya miaka minne ya kuishi nae sasa nataka kufanya maamuzi ya kufunga nae ndoa,lakini moyoni bado nna kitu kinanisumbua sana kitu chenyewe ni hiki

Wakati Mimi naaangaika na shule kwa ajili ya maisha ya baadae mwenzangu alikua anaangaika na mapenzi,starehe nyingi na out kibao na watu wazima

Jambo jingine ni kua yeye ni Mama wa nyumbani na Mimi ndo mtafutaji pekee kwaiyo maendeleo niliyokua Nayo sasa nahisi yangekua mbali zaidi kama ningekua naishi ma mfanyakazi mwenzangu kuliko uyu tegemezi

Pia umri wetu karibia sawa maana nimemzidi mwaka mmoja,hapa shida ni kua kwa nini nisiwe na kabinti kadogo kazuri kenye maisha yake kuliko uyu mtu mzima Mwenzangu alie ona mapenzi ni bora kuliko shule

Nawakilisha

Avatar yako ' imekuokoa ' dhidi ya ' shombo ' zangu hivyo ngoja tu ninyamaze Mwana CCM mwenzangu.
 
Nimeishi nae kama mume na mke uyu binti kwa miaka minne sasa,elimu yake ni kidato cha nne ivyo hakubahatika kuendelea na shule,ni mama wa nyumbani

Mimi nimebahatika kidogo nna kadegree japo kamoja na kakazi ka kujishikiza kidogo

Ndani ya miaka minne tumebahatika kununua gar na kujenga kabanda japo kadogo

Baada ya miaka minne ya kuishi nae sasa nataka kufanya maamuzi ya kufunga nae ndoa,lakini moyoni bado nna kitu kinanisumbua sana kitu chenyewe ni hiki

Wakati Mimi naaangaika na shule kwa ajili ya maisha ya baadae mwenzangu alikua anaangaika na mapenzi,starehe nyingi na out kibao na watu wazima

Jambo jingine ni kua yeye ni Mama wa nyumbani na Mimi ndo mtafutaji pekee kwaiyo maendeleo niliyokua Nayo sasa nahisi yangekua mbali zaidi kama ningekua naishi ma mfanyakazi mwenzangu kuliko uyu tegemezi

Pia umri wetu karibia sawa maana nimemzidi mwaka mmoja,hapa shida ni kua kwa nini nisiwe na kabinti kadogo kazuri kenye maisha yake kuliko uyu mtu mzima Mwenzangu alie ona mapenzi ni bora kuliko shule

Nawakilisha
Rangi ya kijani imekuvuruga..mviuuu
 
Huyo msomi unayemtaka alibakwa udom walipofukuzwa vilerzer
 
Yaani una mke mzuri nyumbani unataka utafute huko nje
Kwani hiyo miaka minne mliyokuwa mnaishi pamoja (ingawa si kwenye ndoa) alikuwa hajatulia?

Kwa nini umuache baada ya kumpotezea miaka minne ya maisha yake?

Nani kakwambia kwamba ukimuacha huyu ukaenda kwa aliyesoma ndio maisha yako yatakuwa bora?

Wewe mwanaume kwa nini usimuwezeshe mke wako?

Tamaa hizi zinawacost sana watu, kutamani vya nje
Jifikirie mara mbili mbili mkuu
Yawezekana ilikuwa sio chaguo sahihi kutokana na mitihani ya hapa na pale katika maisha,ila kama kunA unafuu flani ulionao kwa sasa,we muachie nyumba,cjui usafiri na biashara itayo muingizia pesa ya kula na mafuta then wewe kaendelee na Ligi ndogo lakini pia huduma kwa watoto usiche hata kidogo tena itakubidi uparticipate sehemu kubwa as a father..hapo cdhani kama kutakua na kwere
 
Sema tu ukweli kwamba umesha pata mwanamke mwingine na huyo humtaki tena. Maisha ni ya watu wawili wanao pendana bila kujali hayo mengine....na bila kuyapuuzia pia.
 
Hv wanaume mnakuaga na mashetani gani? Ukishafanikiwa ndo unamwona mwenzio hafai
Sasa leo ndo unajua hajasoma
 
Tafuta mwingine mkuu, ila usisahau kuja kutuletea mrejesho wa yatayokupata
 
tatizo lako nimeshalijua, sio mkeo ni hiko CHAMA. hama CHAMA hutaona kasoro kwa mamsapu.
 
Mkuu nakushauri usikilize moyo wako unasemaje aseeee
 
Kweli kuna watu wana roho ngumu huku duniani kiukweli.
Kakuvumilia toka huna kitu asa hivi umepata maendeleo unaona hafai kweli?
Ety unataka mwenye maisha yake kumbuka huyo unayemtaka kuna waliochangia kumfikisha hapo kama mkeo alivyokusupport hadi hapo ulipo.
Unachokitafuta utakipata soon jichanganye watoto wa mjini wakuonyeshe kazi.
Ushauri:
Kama unaona anakas bure na hana mchango wowote kwanini usimuwezeshe au wewe mbinafsi hutaki mwenzio aendelee?
Mtafutie biashara au mfungulie kamradi utaiona juhudi yake acha kumdharau.
Nikwambie tu unaweza uoe huyo msomi unayemtaka na hata senti kumi yake usiione katika kuendeleza maisha yenu.
Husomagi humu watu wanalia wana wake wanafanya kazi lakini hawachangii chochote katika familia na bado wanaomba pesa kwa waume zao.
Well said,,,, inaonekana kumbe yeye ndo mzinifu, anajua huyo mke atadai wagawane izo Mali .
Hakuna SBB ya maana aliyoitoa mm kama Mchungaji namshauri ubaki na mkeo na huyo ndo anaekufaa
 
Wewe ulibaki kwenye "njia kuu" muda wote huo hukuchepuka hata mara moja? Miaka 4 si haba mmejuana zaidi, cha msingi ni kila mmoja kuwa muwazi kwa mwenziwe, mmoja akienda nje ya mstari aambiwe. Hako kadogo ukatakako unawezajuta baadaye!
 
Kumbuka kuoa mwanamke mwenye kazi ni sawa na kuwa na serikali mbili kwenye nchi moja
 
mie ndo maana nikasema kitu cha mwisho kununua ndani ni glass na sahani...
yakifikia kama ya mtoa mada navunja naondoka zangu.
Wanaume wa namna hii huwa wananishangaza sana,
Unaamini kwamba waliomaliza chuo ndiyo wenye mafanikio zaidi?
huyo wako unashindwa kumshape na kumtengenezea mazingira ya kuleta maendeleo?
Huyo utakaemuoa na fedha zake unaamini unaweza ukaitumia kuleta maendeleo?
Bora ni kile ulichonacho mkononi.
 
Aiseee!!wanaume mna maneno ya kuumiza!

eti wakati we unahangaika na shule yy alikua anahangaika na mabwana loooh!

Nkuulize huo unasema ni mama wa nyumbani hana kazi,unajipikia,unajifulia,unalala peke yako usiku!???

Hvyo vyote ullivyovifanya hajawahi kukushauri kizuri hata kimoja?!!


Mkiwa mnataka kutuacha msiwe mnatudhalilisha hvyoo jamani!!

Mungu ukimuacha huyoo akupe janamke Bomu ka nyuklia!

Dah umeandika mpaka moyo wangu umeniuma!
 
Kiufupi na wewe unapenda kulelewa kama huyo binti! mfanya kazi unamtakia nini? umemsomesha wewe ili ujipange kutafuna salary yake hivyo? wakati unasoma anapika anafua n.k sasa mlipe penssion yake ndipo umuache maana alikuwa mfanyakazi wako. Angekuwa mkeo usingehesabu hayo! hawa wanaume masikini ni hatari zaidi ya cimbra akipata tu utakiona WAEPUKENI SANA
 
Mkuu nikuambie sasa u kweli ni wanawake wachache wenye kazi huchangia maendeleo ya familia. .. wengi tunaishia kushindana tu na minor issues. . Mwanamke bora ni yule anayekuelewa na kukupa nafasi ya kufanya maendeleo.. msomi mnaweza ishia kugombana tu
 
Mapenzi yanazidi kupotea kwa kasi, inamaanisha kipindi chote hicho umeishi nae hukuwa ukimpenda
Baada ya kumchoka sasa unahitaji kitu kingine!!! Sio fair hata kidogo
 
Mpaka miaka minne imepita ndio amekuwa mtu mzima?? Tena umesema mwenyewe mmeishi kama mke na mume,nendeni tu mkabariki ndoa yenu ambayo mmeianzisha miaka minne iliyopita. Ungelijua mapema usingekaa nae miaka yote hiyo.. Huyo binti unayemtaka nae baadaye utasema bora niishi na mtu mzima mwenzangu. What goes around comes around,mwache mtu kwa sababu validy.
 
Back
Top Bottom