Naombeni ushauri ndugu zangu,rafiki zangu

Naombeni ushauri ndugu zangu,rafiki zangu

naliwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
484
Reaction score
1,074
Nimeishi nae kama mume na mke uyu binti kwa miaka minne sasa,elimu yake ni kidato cha nne ivyo hakubahatika kuendelea na shule,ni mama wa nyumbani

Mimi nimebahatika kidogo nna kadegree japo kamoja na kakazi ka kujishikiza kidogo

Ndani ya miaka minne tumebahatika kununua gar na kujenga kabanda japo kadogo

Baada ya miaka minne ya kuishi nae sasa nataka kufanya maamuzi ya kufunga nae ndoa,lakini moyoni bado nna kitu kinanisumbua sana kitu chenyewe ni hiki

Wakati Mimi naaangaika na shule kwa ajili ya maisha ya baadae mwenzangu alikua anaangaika na mapenzi,starehe nyingi na out kibao na watu wazima

Jambo jingine ni kua yeye ni Mama wa nyumbani na Mimi ndo mtafutaji pekee kwaiyo maendeleo niliyokua Nayo sasa nahisi yangekua mbali zaidi kama ningekua naishi ma mfanyakazi mwenzangu kuliko uyu tegemezi

Pia umri wetu karibia sawa maana nimemzidi mwaka mmoja,hapa shida ni kua kwa nini nisiwe na kabinti kadogo kazuri kenye maisha yake kuliko uyu mtu mzima Mwenzangu alie ona mapenzi ni bora kuliko shule

Nawakilisha
 
Kweli kuna watu wana roho ngumu huku duniani kiukweli.
Kakuvumilia toka huna kitu asa hivi umepata maendeleo unaona hafai kweli?
Ety unataka mwenye maisha yake kumbuka huyo unayemtaka kuna waliochangia kumfikisha hapo kama mkeo alivyokusupport hadi hapo ulipo.
Unachokitafuta utakipata soon jichanganye watoto wa mjini wakuonyeshe kazi.
Ushauri:
Kama unaona anakas bure na hana mchango wowote kwanini usimuwezeshe au wewe mbinafsi hutaki mwenzio aendelee?
Mtafutie biashara au mfungulie kamradi utaiona juhudi yake acha kumdharau.
Nikwambie tu unaweza uoe huyo msomi unayemtaka na hata senti kumi yake usiione katika kuendeleza maisha yenu.
Husomagi humu watu wanalia wana wake wanafanya kazi lakini hawachangii chochote katika familia na bado wanaomba pesa kwa waume zao.
 
Kwani huo uhuni wake wa kitambo hujawahi msamehe? Kama jibu ni ndio, je huyo binti mdogo utakayemuoa atakuwa bikra au hatakama ni bikra, je hatakukosea/kukusaliti na kuhitaji msamaha wako? Kama jibu ni ndio kwanini ung'ang'anie kutazama yaliyopita na sio sasa na yajayo, je huyo msomi mwenzako unayetaka kumuoa ana SPIRITUAL LINK ya maendeleo au unafikiri maendeleo ni kuoa msomi mwenye ajira? TULIA KIJANA SAFARI BADO.
 
ushaharibu ulikurupuka at the begining hii game ngumu sasa wacha ikuonyeshe
 
Yaani una mke mzuri nyumbani unataka utafute huko nje
Kwani hiyo miaka minne mliyokuwa mnaishi pamoja (ingawa si kwenye ndoa) alikuwa hajatulia?

Kwa nini umuache baada ya kumpotezea miaka minne ya maisha yake?

Nani kakwambia kwamba ukimuacha huyu ukaenda kwa aliyesoma ndio maisha yako yatakuwa bora?

Wewe mwanaume kwa nini usimuwezeshe mke wako?

Tamaa hizi zinawacost sana watu, kutamani vya nje
Jifikirie mara mbili mbili mkuu
 
Aiseee!!wanaume mna maneno ya kuumiza!

eti wakati we unahangaika na shule yy alikua anahangaika na mabwana loooh!

Nkuulize huo unasema ni mama wa nyumbani hana kazi,unajipikia,unajifulia,unalala peke yako usiku!???

Hvyo vyote ullivyovifanya hajawahi kukushauri kizuri hata kimoja?!!

Mkiwa mnataka kutuacha msiwe mnatudhalilisha hvyoo jamani!!

Mungu ukimuacha huyoo akupe janamke Bomu ka nyuklia!
 
1475257617914.jpg
 
Nimeishi nae kama mume na mke uyu binti kwa miaka minne sasa,elimu yake ni kidato cha nne ivyo hakubahatika kuendelea na shule,ni mama wa nyumbani

Mimi nimebahatika kidogo nna kadegree japo kamoja na kakazi ka kujishikiza kidogo

Ndani ya miaka minne tumebahatika kununua gar na kujenga kabanda japo kadogo

Baada ya miaka minne ya kuishi nae sasa nataka kufanya maamuzi ya kufunga nae ndoa,lakini moyoni bado nna kitu kinanisumbua sana kitu chenyewe ni hiki

Wakati Mimi naaangaika na shule kwa ajili ya maisha ya baadae mwenzangu alikua anaangaika na mapenzi,starehe nyingi na out kibao na watu wazima

Jambo jingine ni kua yeye ni Mama wa nyumbani na Mimi ndo mtafutaji pekee kwaiyo maendeleo niliyokua Nayo sasa nahisi yangekua mbali zaidi kama ningekua naishi ma mfanyakazi mwenzangu kuliko uyu tegemezi

Pia umri wetu karibia sawa maana nimemzidi mwaka mmoja,hapa shida ni kua kwa nini nisiwe na kabinti kadogo kazuri kenye maisha yake kuliko uyu mtu mzima Mwenzangu alie ona mapenzi ni bora kuliko shule

Nawakilisha

hahahaha, nimecheka eh. Akili kichani, husiishi kwa akili za kupewa, fuata moyo wako.

Unaweza kuona msichana mdogo na kashamaliza wanaume 2000, na ana degree 2, na anamshiko wa mapene.

Unaangalia past ya mtu au future ya mtu?
unaangalia elim ya mtu au akili ya mtu?
unaangalia uchumi wa mtu au mapenzi?
 
nini nisiwe na kabinti kadogo kazuri kenye maisha yake kuliko uyu mtu mzima Mwenzangu alie ona mapenzi ni bora kuliko shule
We nawe utajiita msomi?ni mawazo gani haya.
Unataka mke uliyempenda,au mfanyakazi mwenzako? Huo utuuzima wake ndo umeuona sasa hivi?hako ka gari ndo kanakutia kibur eeh..
Kua makini mkuu shetani anakutembelea
 
Back
Top Bottom