Naombeni ushauri mawazo yananitesa sana.

Mkuu kuna makosa ya kusamehe kabla ya ndoa lakini la usaliti sio kosa la kisamehe..
Kama kakusaliti kabla ya kumuoa unategemea nini miaka 10 baada ya ndoa akishapata mtoto na kuzoea show zako?

Usaliti unaweza kuvumiliwa kidogo baada ya ndoa sababu ya viapo vya shida na raha lakini sasa hivi nakushauri uachane na huyo mwanamke umove on mapemaaa kabla hatujaanza kutoa rambirambi kwa ajili yako.

Mwanamke anayekucheat sasa hivi atacheat tena ..tena inawezekana sasa hivi na hiki ki baridi jamaa yuko anapiga bao la asubuhi halafu wewe unakaa kama ndezi ndezi..

Halafu usidanganywe na machozi ya mwanamke ukahisi eti yuko serious anajuta kwa alichokifanya..
Mwanamke anaweza kulia kisa kapoteza elf 50 ..kwahio machozi sio kigezo cha kujuta...wewe mpige chini uanze upya
 
Mtaniwia radhi kwa uandishi wangu ndugu zangu,mimi siyo mwandishi mzuri sana ila nitajitahidi mnielewe.

Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, nipo katika mahusiano na binti mmoja mwenye miaka 25 na sasa huu ni mwaka wa nne tupo katika mahusiano na tunapendana.

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwani huyu mwanamke nimegundua siyo mwaminifu baada ya kukuta sms ktk simu yake akichat na mwanaume mwingine na huyo mwanaume akimuomba ampe tena penzi, (inavyoonekana tayari walishafanya kipindi cha nyuma). baada ya kuona sms hiyo nilimuuliza huyo mpenz wng mbona amenisaliti? alilia sana na akaniambia ni kwel amenisalit ila amefanya mapenz mara mbili tu na huyo mwanaume na hatarudia tena. Dah kiukwel niliumia sana kwa sababu toka nimekuwa naye kwenye mahusiano sijawahi kuchepuka hata siku moja. Alilia kwa siku tatu mfulilizo hadi nikamuonea huruma nikamsamehe ila bado moyo wangu unauma sana kila nikifikiria.

Huyu mpenz wang anafanya kaz mkoa mbali na niliopo na huwa tunaonana kila baada ya miez mitatu au minne wakat mwingine had mitano, kinachoniuma zaidi huyo jamaa aliyechepuka naye wanafanya kazi sehem moja na ana kitengo kikubwa kuliko yeye. Kwa sasa mpenz wng yupo huko kazn kwao ila roho inaniuma sana kila wakat nahis anachepuka na jamaa tu coz wapo sehemu moja.

Nilishamsamehe ila roho yangu inauma sana ndugu zangu naomben ushauri.Moyo unauma sana.

mapenzi ya kisha kuwa na umbali sio mapenzi
 
Hivi kumbe kuna wanaume wasiochepuka...hongera sana mkuu...huyo mpenzi wako ameokota dhahabu ila hajui Kama ni dhahabu..Mimi ningekuwa yeye nisingechepuka hata kwa bahati mbaya.
 
Mtaniwia radhi kwa uandishi wangu ndugu zangu,mimi siyo mwandishi mzuri sana ila nitajitahidi mnielewe.

Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, nipo katika mahusiano na binti mmoja mwenye miaka 25 na sasa huu ni mwaka wa nne tupo katika mahusiano na tunapendana.

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwani huyu mwanamke nimegundua siyo mwaminifu baada ya kukuta sms ktk simu yake akichat na mwanaume mwingine na huyo mwanaume akimuomba ampe tena penzi, (inavyoonekana tayari walishafanya kipindi cha nyuma). baada ya kuona sms hiyo nilimuuliza huyo mpenz wng mbona amenisaliti? alilia sana na akaniambia ni kwel amenisalit ila amefanya mapenz mara mbili tu na huyo mwanaume na hatarudia tena. Dah kiukwel niliumia sana kwa sababu toka nimekuwa naye kwenye mahusiano sijawahi kuchepuka hata siku moja. Alilia kwa siku tatu mfulilizo hadi nikamuonea huruma nikamsamehe ila bado moyo wangu unauma sana kila nikifikiria.

Huyu mpenz wang anafanya kaz mkoa mbali na niliopo na huwa tunaonana kila baada ya miez mitatu au minne wakat mwingine had mitano, kinachoniuma zaidi huyo jamaa aliyechepuka naye wanafanya kazi sehem moja na ana kitengo kikubwa kuliko yeye. Kwa sasa mpenz wng yupo huko kazn kwao ila roho inaniuma sana kila wakat nahis anachepuka na jamaa tu coz wapo sehemu moja.

Nilishamsamehe ila roho yangu inauma sana ndugu zangu naomben ushauri.Moyo unauma sana.
Mkuu mimi naona kosa unalo wewe moja ya kosa lako ni nikukaa mbali na mchumba na afazali muwe mnaonana hata mwezi mara moja ila unakaa mpk miezi 4 ndio mnaonana unategemea nini kama wewe unaweza kukaa miezi yote hiyo bila kufanya kwa nini umtese mwenzako muhimu muowe kisha umlete kwako achana na mapenzi ya kukaa mbali mbali labda kwa zarura tu
 
Broo Akilitime maneno umeyamaliza kaka, na asikie mwenye kusikia.
Ni wachache sana kwenye dunia ya sasa wenye kumudu long distance relationship, karibia kusema ni hakuna kabisa.
 
Mkuu nimejaribu kuvaa viatu vyako.

Nakushauri,huyo mwanamke muache
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom