Naombeni ushauri mawazo yananitesa sana.

Naombeni ushauri mawazo yananitesa sana.

Mtaniwia radhi kwa uandishi wangu ndugu zangu,mimi siyo mwandishi mzuri sana ila nitajitahidi mnielewe.

Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, nipo katika mahusiano na binti mmoja mwenye miaka 25 na sasa huu ni mwaka wa nne tupo katika mahusiano na tunapendana.

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwani huyu mwanamke nimegundua siyo mwaminifu baada ya kukuta sms ktk simu yake akichat na mwanaume mwingine na huyo mwanaume akimuomba ampe tena penzi, (inavyoonekana tayari walishafanya kipindi cha nyuma). baada ya kuona sms hiyo nilimuuliza huyo mpenz wng mbona amenisaliti? alilia sana na akaniambia ni kwel amenisalit ila amefanya mapenz mara mbili tu na huyo mwanaume na hatarudia tena. Dah kiukwel niliumia sana kwa sababu toka nimekuwa naye kwenye mahusiano sijawahi kuchepuka hata siku moja. Alilia kwa siku tatu mfulilizo hadi nikamuonea huruma nikamsamehe ila bado moyo wangu unauma sana kila nikifikiria.


Huyu mpenz wang anafanya kaz mkoa mbali na niliopo na huwa tunaonana kila baada ya miez mitatu au minne wakat mwingine had mitano, kinachoniuma zaidi huyo jamaa aliyechepuka naye wanafanya kazi sehem moja na ana kitengo kikubwa kuliko yeye. Kwa sasa mpenz wng yupo huko kazn kwao ila roho inaniuma sana kila wakat nahis anachepuka na jamaa tu coz wapo sehemu moja.

Nilishamsamehe ila roho yangu inauma sana ndugu zangu naomben ushauri.Moyo unauma sana.
angalia namba 1 na 4
 
Kiukweli imebidi nicheke tu Kwasababu Kama anafanya kaz Sehem Moja na huyo Jamaa Aisee usjipe Moyo hata kidogo Jamaa anapiga mzigo unafki sio mzur
 
cheating is a decision/choice. Binafsi sinaga msamaha kwa msaliti ila ukiona nipo nae ujue ni kwa faida binafsi baada ya mda nasepa, naamini msaliti hawezi kuacha iyo dhambi ipo siku atarudia tu.
 
Ngoja roho imuume hadi apate akili.
Dawa ya mazuzu kama hawa ni kuwaletea nyuki, wamuume, maumivu ya kuumwa na nyuki ukiongeza maumivu ya kuumwa moyo, akili lazima zirudi mahali pake na utafanya maamuzi sahihi ya kiume
Duuuuh
 
Haha mkuu sio mimi kwakua tukio halikua huko boss mimi nipo Mzinga apa Morogoro
Unatafutwa mkuu umetembea na demu wa mtu Nipo hapa sinza jamaa ametukaja jina lako na tukio zima sasa nimeunga Doti ni ww kabsaa amepania kutoa marinda
 
Hee mtu upo mbali nae na anae chepuka nae yupo karibu yake

Hapo mkuu hata utumie ndumba bdo ataendelea kumegwa tuu
We jiongeze
 
Eti ameli siku tatu mfululizo, unawajua wanawake wewe? Haswa hawa wanaokimbilia machozi kama defencive mechanism.

Usichokijua ni kuwa: wanawake ni wasanii kuliko wasanii wa kaole na futuhi.
 
Angalia usalama kwanza. Hafu ukiona salama anza kamchezo kumla tu uku ukitafuta mwingine , Hit and run.
 
Back
Top Bottom