Naombeni ushauri mawazo yananitesa sana.

Naombeni ushauri mawazo yananitesa sana.

Sasa we jamaa? Miaka minne upo nae why hujamuoa na mkafunga ndoa? Nan alkwambia fimbo ya mbali inaua nyoka?
Fanya mchakato umsogeze karibu kama una uwezo mhamishe kazi aje ulipo wewe
Hakika nakwambia yuko mbion kukuacha na ataolewa na huyohuyo jamaa.
Kwanza inaonekana we ndo unampenda ila yeye hakupendi ni bas tu huenda wewe alshakufanya kama source nyingine ya income.
Ni kwel nampenda na yeye pia ananipenda, na kuhusu suala la kiuchumi wote tunasaidiana na wala hanitegemei sana japo huwa namjali pia.
 
Mkuu kuna makosa ya kusamehe kabla ya ndoa lakini la usaliti sio kosa la kisamehe..
Kama kakusaliti kabla ya kumuoa unategemea nini miaka 10 baada ya ndoa akishapata mtoto na kuzoea show zako?

Usaliti unaweza kuvumiliwa kidogo baada ya ndoa sababu ya viapo vya shida na raha lakini sasa hivi nakushauri uachane na huyo mwanamke umove on mapemaaa kabla hatujaanza kutoa rambirambi kwa ajili yako.

Mwanamke anayekucheat sasa hivi atacheat tena ..tena inawezekana sasa hivi na hiki ki baridi jamaa yuko anapiga bao la asubuhi halafu wewe unakaa kama ndezi ndezi..

Halafu usidanganywe na machozi ya mwanamke ukahisi eti yuko serious anajuta kwa alichokifanya..
Mwanamke anaweza kulia kisa kapoteza elf 50 ..kwahio machozi sio kigezo cha kujuta...wewe mpige chini uanze upya
Ahsante kwa ushauri mzur mkuu.
 
Hivi kumbe kuna wanaume wasiochepuka...hongera sana mkuu...huyo mpenzi wako ameokota dhahabu ila hajui Kama ni dhahabu..Mimi ningekuwa yeye nisingechepuka hata kwa bahati mbaya.
To be honest, kuchepuka sijawahi. na sitarajii, I can't.
 
Mkuu mimi naona kosa unalo wewe moja ya kosa lako ni nikukaa mbali na mchumba na afazali muwe mnaonana hata mwezi mara moja ila unakaa mpk miezi 4 ndio mnaonana unategemea nini kama wewe unaweza kukaa miezi yote hiyo bila kufanya kwa nini umtese mwenzako muhimu muowe kisha umlete kwako achana na mapenzi ya kukaa mbali mbali labda kwa zarura tu
asante kwa ushaur
 
Kafanya mapenz mara mbili tu ila hatorudia tena?

Kwann hakufanya nae mara moja tu?

Ivi nyie vijana wenzangu kwann tusijikite kwenye mirad yetu ya kutuingia pesa?

Love affairs ni very complicated hamjui tu.
 
Kosa la usaliti huwa msamaha wake ni mgumu sana, anyway nawewe tafuta mke mwingine, aje ajue then utaishi na huyo mpya! Hapa amani ya moyo utaipata!
Dah, sitak nilipe ubaya kwa ubaya mkuu, Nitafanya kitu kimoja tu. Nategemea kumtembelea hivi karibuni kazn kwake then nitamweleza yote kuwa nimeshindwa kuishi kwa aman kutokana na lile kosa lake la usalit... then nitamuomba tusitishe mahusiano kiroho safi, najua atalia sana ila ndoivo nimeshafanya maamuzi.
 
Kwenye movie yake ya Moses kuna sentensi Marehemu Kanumba aliitoa akasema.

'NEVER TRUST A DISABILITY DOG OR A CRIED WOMAN'

Jiongeze mkuu achana nae move on with your pride, not every loss is a loss.
asante kwa ushaur mkuu
 
Mchiti na wewe mkuu.
Muende sawa!!!
Maana hicho ndio kinachofanya moyo ukuume.
Balance equation tu.
nishawaza sana kucheat mkuu ila moyo wng umekuwa mgum kufanya hivyo.
 
Pole mkuu Mapenzi yanaumiza sana ila fanya moyo wako ukubali kuwa Hakuna uaminifu dunia ya leo. Kuvamiwa kama hivyo ni jambo la kawaida sana kwa sasa. Jitahidi moyo ukubali hali ikiwezekana Mkapime kwanza
Nashukuru kwa ushaur mkuu
 
So sad ivi bado kuna watu wanaimani na mapenzi ya kuwa mbali mbali?
 
nashukuru sana mkuu kwa ushaur, tulipanga tuoane mwakan lkn ndo nawaza kusitisha.coz sina aman ya moyo
Amani ya moyo wako ni muhim sana mkuu usikimbilie kuoa matatizo, Mungu amekuonesha kitu ili ujue n kip cha kufanya kabla hamjafunga pingu za maisha

NB:kuumizwa huwa n mara moja ukiumia tena unayataka mwenyew hayo maumivu
 
Mtaniwia radhi kwa uandishi wangu ndugu zangu,mimi siyo mwandishi mzuri sana ila nitajitahidi mnielewe.

Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, nipo katika mahusiano na binti mmoja mwenye miaka 25 na sasa huu ni mwaka wa nne tupo katika mahusiano na tunapendana.

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwani huyu mwanamke nimegundua siyo mwaminifu baada ya kukuta sms ktk simu yake akichat na mwanaume mwingine na huyo mwanaume akimuomba ampe tena penzi, (inavyoonekana tayari walishafanya kipindi cha nyuma). baada ya kuona sms hiyo nilimuuliza huyo mpenz wng mbona amenisaliti? alilia sana na akaniambia ni kwel amenisalit ila amefanya mapenz mara mbili tu na huyo mwanaume na hatarudia tena. Dah kiukwel niliumia sana kwa sababu toka nimekuwa naye kwenye mahusiano sijawahi kuchepuka hata siku moja. Alilia kwa siku tatu mfulilizo hadi nikamuonea huruma nikamsamehe ila bado moyo wangu unauma sana kila nikifikiria.


Huyu mpenz wang anafanya kaz mkoa mbali na niliopo na huwa tunaonana kila baada ya miez mitatu au minne wakat mwingine had mitano, kinachoniuma zaidi huyo jamaa aliyechepuka naye wanafanya kazi sehem moja na ana kitengo kikubwa kuliko yeye. Kwa sasa mpenz wng yupo huko kazn kwao ila roho inaniuma sana kila wakat nahis anachepuka na jamaa tu coz wapo sehemu moja.

Nilishamsamehe ila roho yangu inauma sana ndugu zangu naomben ushauri.Moyo unauma sana.
Ukiona Bado una kinyongo inamaanisha Bado hujamsamehe kutoka moyoni mwako.
 
Hapa kinacho kusumbua nikwamba umejua jitahidi usijue hata ukipata mwingine hayo mambo yapo tu na huo ndio ukubwa wenyewe hata wewe ipo siku utasaliti tu
 
Pole mkuu Mapenzi yanaumiza sana ila fanya moyo wako ukubali kuwa Hakuna uaminifu dunia ya leo. Kuvamiwa kama hivyo ni jambo la kawaida sana kwa sasa. Jitahidi moyo ukubali hali ikiwezekana Mkapime kwanza
Unatafutwa mkuu umetembea na demu wa mtu Nipo hapa sinza jamaa ametukaja jina lako na tukio zima sasa nimeunga Doti ni ww kabsaa amepania kutoa marinda
 
Back
Top Bottom